Kwa ambao mmewahi kufanya kazi mazingira ya hospitali mtakubaliana na Chalamila ila hamtakubaliana na maneno aliyotumia.
Wananchi wanapotoshwa mno na siasa. Mwanasiasa anamwambia mwananchi mzee, mtoto chini ya miaka 5 na mama mjamzito anahudumiwa bure kabisa.
Mzee anakuja hospitali, ana kitambulisho cha wazee ambacho kinacover vitu vichache akija kuambiwa vingine anatakiwa kulipia anampigia simu Diwani kulalamika.
Diwani anaside na mwananchi. Bila kukumbuka hospitali ikishindwa kujiendesha yeye diwani amechangia katika level hiyo.
So, kiukweli Chalamila alikua na ujumbe mzuri ila uchaguzi wa maneno ndiyo changamoto