Pre GE2025 Heche amchana RC Chalamila, kisa kauli ya mjamzito anayegoma kununua gloves, adai wamejisahu kwasababu ya shibe ya kijinga

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sasa kutokana na hata ARVs na dawa za TB kua zinaletwa na USAID na PEPFAR ndiyo sababu Tz inazitoa bure hizi kwa waathirika. Trump ambavyo ana mpango wa kujitoa na hizi dawa zisipokuja means itabidi Serikali inunue na iweke utaratibu wa wananchi kuchangia hii huduma.

Ni wakazi wangapi wa Mpwimbwi wanajua kua dawa zinaweza kusitishwa na mbadala ni wao kuchangia? Vipimo vya Malaria na dawa vyote vilikua bure, chanjo za watoto hadi neti. Ikifika muda mbadala ni kuchangia pekee hapo sasa ndiyo moto utawaka na itabidi waambiwe ukweli
Ila misaada mingine kwa kweli ilikuwa inaliaibisha Taifa. Fikiria shule inajengewa matundu kumi ya Choo kwa msaada wa Watu wa Marekani. Halafu unakuta bango kubwa limebandikwa karibu na Choo hicho " Matundu haya ya Choo yamejengwa kwa Msaada wa Watu wa Marekani'' yaani hata "shitholes" tunashindwa kujenga hadi kuhitaji msaada wa hao jamaa. What a shame? Trump katuaibisha na inabidi tuchutame maana kiukweli katuvua nguo.
 
Mimi nataka kuuliza kidogo! Hivi inchi zilizoeneelea gharama za huduna za Afya na elimu mfumo wa kulipia upoje? Analipa nani?
Maana huko ndio tunakoamini wamestarabika.
He ikiwa kila huduma serikali ilipe free, kweli itaweza?
 
Kiukweli kuna vitu vilikua ni aibu. Zamani ilikua inatumika nguvu kazinya wanakijiji na serikali katika vitu kama hivyo
 
Kwa ambao mmewahi kufanya kazi mazingira ya hospitali mtakubaliana na Chalamila ila hamtakubaliana na maneno aliyotumia.

Wananchi wanapotoshwa mno na siasa. Mwanasiasa anamwambia mwananchi mzee, mtoto chini ya miaka 5 na mama mjamzito anahudumiwa bure kabisa.

Mzee anakuja hospitali, ana kitambulisho cha wazee ambacho kinacover vitu vichache akija kuambiwa vingine anatakiwa kulipia anampigia simu Diwani kulalamika.

Diwani anaside na mwananchi. Bila kukumbuka hospitali ikishindwa kujiendesha yeye diwani amechangia katika level hiyo.

So, kiukweli Chalamila alikua na ujumbe mzuri ila uchaguzi wa maneno ndiyo changamoto
Asante kwa ufafanuzi.ila huna akili
 
Mimi nataka kuuliza kidogo! Hivi inchi zilizoeneelea gharama za huduna za Afya na elimu mfumo wa kulipia upoje? Analipa nani?
Maana huko ndio tunakoamini wamestarabika.
He ikiwa kila huduma serikali ilipe free, kweli itaweza?
Swali Gani hili??kwani huko Kuna wezi wa Mali ya uma kama cccccmmm??
 
Kwa ambao mmewahi kufanya kazi mazingira ya hospitali mtakubaliana na Chalamila ila hamtakubaliana na maneno aliyotumia.

Wananchi wanapotoshwa mno na siasa. Mwanasiasa anamwambia mwananchi mzee, mtoto chini ya miaka 5 na mama mjamzito anahudumiwa bure kabisa.

Mzee anakuja hospitali, ana kitambulisho cha wazee ambacho kinacover vitu vichache akija kuambiwa vingine anatakiwa kulipia anampigia simu Diwani kulalamika.

Diwani anaside na mwananchi. Bila kukumbuka hospitali ikishindwa kujiendesha yeye diwani amechangia katika level hiyo.

So, kiukweli Chalamila alikua na ujumbe mzuri ila uchaguzi wa maneno ndiyo changamoto
Wallah bilai watalai wewe Mtanzania umesema kweli
 
Nchi ambazo zipo sirias zinajali sana uzazi kwa sababu ndio huleta nguvu kazi ya taifa. Mbona nchi nyingine mtu akizaa analipwa kabisa. Ni kwa sababu watu wasipozaa nchi itakuwa na wazee! Sasa Tanzania uhangaike na mimba, kulea mtoto halafu mtoto akija kuwa potential mf mwanasayansi nguli anaanza kuambiwa awe mzalendo na nchi yake wakati hakuhudumiwa na serikali kipindi cha utotoni
Kushika mimba na kujifungua siyo suala la dharura, wazazi tunapaswa kuchangia huduma za kujifungua
 
Unahangaika na mimba kwa uzembe wako maana si lazima ushike mimba kama hujajiandaa kuitunza. Watanzania tupo wengi sana usilinganishe na nchi zenye watu milioni nne eti wanalipwa wakijifungua. Tuache ujanja ujanja, kushika mimba ni suala la hiari na serikali imeweka mazingira mazuri ya watu kuishi kwa kujiachia ili mradi huvunji sheria.
 
Sasa kutokana na hata ARVs na dawa za TB kua zinaletwa na USAID na PEPFAR ndiyo sababu Tz inazitoa bure hizi kwa waathirika. Trump ambavyo ana mpango wa kujitoa na hizi dawa zisipokuja means itabidi Serikali inunue na iweke utaratibu wa wananchi kuchangia hii huduma.

Ni wakazi wangapi wa Mpwimbwi wanajua kua dawa zinaweza kusitishwa na mbadala ni wao kuchangia? Vipimo vya Malaria na dawa vyote vilikua bure, chanjo za watoto hadi neti. Ikifika muda mbadala ni kuchangia pekee hapo sasa ndiyo moto utawaka na itabidi waambiwe ukweli
Wananchi kwa kiwango cha kodi na tozo tunazolipa, hakuna ulazima wa kuchangia huduma za hospitali!!
Serikali inatakiwa kufanya reallocation ya revenue expenditure kutoka kwenye matumizi ya anasa kwenda kwenye matumizi ya lazima!
Punguzeni mishahara na posho za wabunge : acheni ununuzi wa magari ya anasa na punguzeni safari zisizokuwa za lazima! Fedha itatosha kuwapa wananchi huduma za lazima.
 
Mkuu kwa kukisia kwako ni wananchi wangapi wanaexploit loopholes ili wasilipe kodi?
 
Wananchi wengi sana hawalipi kodi kwa makusudi! Wanafanya hivyo kwasababu wanaona serikali ya Samia inatumia vibaya hiyo wanayokusanya! Serikali inatumia kodi kwa matanuzi na sio maendeleo; mfano kununua land cruisers latest models zenye bei mbaya kwa matumizi ya viongozi ; safari za viongozi kwenda ughaibuni kwenda kubembea kama Samia alivyochukua familia yake kwenda marekani akiwemo mke wa Mchengerwa waziri wa Tamisemi.
Haya yote ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi. Na Ndio maana hivi sasa ofisi za TRA zinachomwa as a sign of protest!! The tax regime is very oppressive .
 
Ok sawa.

So katika haya maelezo ni unakubali kwamba wananchi wengi hawalipi kodi.

Pia unakisia Tz ina hospitali ngapi na shule ngapi zinazohudumiwa 100% serikali?
 
Back
Top Bottom