SI KWELI Heche amesema 'Haki haijawahi kupatikana kwa kuiba mali za wengine'

SI KWELI Heche amesema 'Haki haijawahi kupatikana kwa kuiba mali za wengine'

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
HAKI.jpg
 
Tunachokijua
John Heche ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye alichaguliwa kutumikia nafasi hiyo Januari 21, 2025 akichukua nafasi ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Tundu Lissu ambaye alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho.

Kupitia makamu mwenyekiti wake John Heche, CHADEMA Novemba 19, 2025 ilitoa msimamo wake kuhusu tume iliyoandaliwa kuchunguza “matukio ya uvunjifu wa amani” baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025.

Ikumbukwe kuwa Novemba 18, 2025 Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka alitoa taarifa kwa umma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, aliunda Tume ya kufanya uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea nchini wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 29 Oktoba, 2025.


Madai

Kutokana na mkutano wa Heche na waandishi wa habari kumekuwepo na taarifa inayosambazwa mtandaoni ikitumia utambulisho wa Jambo TV ikimtaja makamu mwenyekiti huyo kuwa amesema 'Haki haijawahi kupatikana kwa kuiba mali za wengine'

Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia marejeo ya video umebaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli, ni ya kutengenezwa kwani Kauli hiyo haikutolewa kabisa na Heche alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Aidha kupitia video iliyochapishwa kwenye 'Channel' ya CHADEMA MEDIA TV akihitimisha hotuba yake Heche alisema
"Ujumbe wetu uko wazi na thabiti, Hakuna amani bila haki. Hakuna uhalali bila ridhaa ya wananchi. Mtuhumiwa hawezi kuwa mwamuzi wa uhalifu alioufanya."

Vilevile grafiki iliyotumika kusambaza taarifa hiyo ni ya kughushi kwani haijachapishwa katika kurasa rasmi za Jambo TV.
​
Back
Top Bottom