SI KWELI Heche amesema Passport yake imekwisha muda ndiyo maana imechukuliwa?

SI KWELI Heche amesema Passport yake imekwisha muda ndiyo maana imechukuliwa?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Heche.jpg
 
Tunachokijua
Oktoba 18, 2025 akiwa mpakani mwa Tanzania na Kenya kuelekea kwenye mazishi ya Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga, Makamu mwenyekiti wa CHADEMA alizuiwa na idara ya uhamiaji kuvuka mpaka na Pasport yake kushikiliwa na idara hiyo.

Madai

Kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook Oktoba 19, 2025 kumekuwa na grafiki inayosambazwa ikiambatana na nukuu inayodaiwa kuwa ni ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche akieleza kuwa sababu ya Passport yake kuchukiwa ni kuisha muda.

Uhalisia wa taarifa hiyo

JamiiCheck imefuatilia na kujirirdhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.

Ufuatiliaji kwa njia ya maneno muhimu umebaini kuwa hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichochapisha nukuu hiyo inayodaiwa kutolewa na kiongozi huyo.

Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao kupitia ukurasa wa X wa Heche umebaini kuwa hajachapisha pia wala kutoa taarifa hiyo kama inayvyodaiwa na taarifa hiyo inayosambazwa.

Aidha JamiiCheck imejirirdhisha kuwa taarifa hiyo ni ya kughushi kwani haijachaoishwa na Mwanananchi kama inavyoonekana. Grafiki iliyoambatanishwa na taarifa hiyo pia ni ya kughushi huku ikiwa na mapungufu kadhaa ikiwemo kutumia aina tofauti ya mwandiko.

Idara ya uhamiaji katika taarifa yake ya Oktoba 18, 2025 iliyotolewa na msemaji wake SSI, Paul Mselle hawajaeleza sababu zilizopelekea Passport ya John Heche kushikiliwa.
Back
Top Bottom