John Manoni
JF-Expert Member
- Sep 5, 2020
- 612
- 382
Wakuu, Uchaguzi mkuu utagharimu mabilioni ya walipa kodi katika nyakati ambazo wananchi wanakosa dawa hospitalini na watoto kukalia dawati shuleni ni utajiri.
Kwahiyo maigizo ya 4R (cosmetics reforms) yanayotangazwa huko CCM hayafai na wa Tanzania wote wapaze sauti kuyakataa..
Hoja ya uchaguzi ambao wananchi wanahaki ya kuamua hatima ya kura zao kulingana na katiba ya nchi ibara ya 8, imefafanuliwa vema na CHADEMA.
Mhe.Heche kwanza nampongeza sana,pamoja na wanachadema walioko mstari wa mbele kwenye mabadiliko,bila kumsahau mhe. Lissu aliyeko kizuizini,hii No reforms No election imebeba hoja za watanzania.
Kuumiza watu na kupata uongozi kwa damu za watu waliopigwa na kutekwa na kuuawa,ni kukosa maadili,wala siyo maadili ya watanzania, lakini kwanini CHADEMA wanaotaka mabadiliko kwenye sheria mbovu wanawindwa na kuonekana wanavurugu ila wanaotaka tuendelee kuuharibu uchaguzi kwa faida ya watawala kupata ushindi wanalindwa.
Yupo mwanaccm anasema kwamba mabadiliko ni baada ya uchaguzi,kusema mabadiliko ni baada ya uchaguzi ni kutambua elimu inayotolewa na mhe. Heche au labda uroho wa madaraka umeshupaza shingo.
Fikiria mtu anaambiwa kupiga kura ni haki ya kikatiba,anapanga foleni juani na kunyeshewa mvua,kumbe msimamizi anaye mshindi mfukoni,anasaidiwa na polisi kuingiza kura bandia na kumtangaza ambaye hakushinda wa chama tawala CCM. Mpinzani bila vita hawezi kutangazwa,rej.uchaguzi wa 2010 kumtangaza Mhe.Wenje,mhe.Heche...2015 mhe.Lijualikali n.k.
Fikiria nchi yenye utajiri kila mahali, viongozi wanaoapa kwa vitabu vya Dini wanapatikana kwa wizi wa kura. Ndio maana wananchi ni masikini na elimu ni matope kwani mfumo wa kupata viongozi umetekwa na wezi na waroho wa madaraka.