John Heche ni makamu mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye alianza kuitumikia nafasi hiyo mara ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika mnamo Januari 21, 2025. Pia
aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini kuanzia mwaka 2015 mpaka 2020.
Mara nyingi kumekuwapo upotoshaji unaowahusisha viongozi mbalimbali wa CHADEMA ambao umekuwa ukisaambazwa kupitia mitandao ya kijamii, rejea
hapa, hapa na
hapa.
Kumekuwapo na
chapisho linalosambazwa katika mtandao wa Facebook lililotumia utambulisho wa Ngoma Media likiwa na kichwa cha habari 'Heche asema CHADEMA imekosa ushawishi kwa wananchi' likirejelea
chapisho linaloonekana kuchapishwa kuchapishwa na John Heche kupitia mtandao wa X.
Je, ni upi uhalisia wa chapisho hilo?
Ufuatiliaji wa uliofanywa na JamiiCheck ukihusisha utafutaji wa kimtandao umebaini kuwa hakuna ukurasa rasmi katika mitandao ya kijamii unaotoa habari ukijulikana kama
Ngoma Media bali Chapisho hilo limetengenezwa na wapotoshaji wakitumia utambulisho wa ukurasa ambao haupo.
Aidha chapisho linaloonekana kuchapishwa na Heche kupitia mtandao wa X si la kweli, bali limetengenezwa na wapotoshaji kwani halikuchapishwa katika
ukurasa huo.
Mnamo tarehe 10 Machi 2025 Heche alifanyiwa mahojiano na Charles William katika kipindi cha 'One On One' kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Wasafi TV ambapo
aligusia imani ya wananchi kwa chama hicho hususani katika kampeni yao ya 'Tone Tone' kuchangia fedha ili kuwezesha utendaji wa shughuli za chama.
"Tumefurahishwa na jinsi ambavyo watanzania wanatuunga mkono... mtu anayetuchangia maana yake moyo wake upo CHADEMA."