- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- John Heche ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Taifa. Heche na viongozi wengine wa chama hiko wanaendelea na kampeni yao ya No reforms No election katika mikoa mbalimbali nchini.
Madai
Katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo faceebook kuna kipande cha video kinachomuonesha makamu mwenyekiti wa Chadema taifa, john Heche akitamka maneno yanayoashiria kuwa kampeni ya ‘no reforms no election’ ni ya kijinga. Maneno yanayosikika katika video hiyo ni;
“Tuko kwenye opersheni ya chama inaitwa na reforms no election ni ya kijinga sana, operesheni ya hovyo, operesheni gani hii. Mimi nawauliza nyinyi kuna akili hapo?”
Uhalisia wa video hiyo
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa kipande hiko cha video kimehaririwa kwa kuungwa kwa vipande vidogo vidogo kutoka kwenye video halisi ili kupotosha uhalisia.
Kipande cha video kinachoonekana kumuonesha John Heche kimetoka kwenye video ya hotuba yake aliyoitia Same alipokuwa katika uendelezo wa ziara yao ya ‘No reforms No election’ Mei 31, 2025 na kurushwa chaneli mbalimbali za You tube ikiwemo Mwanzo TV.
View: https://www.youtube.com/watch?v=UMzfAUOeRIg
Katika video halisi Heche alizungumzia kuwa wapo kwenye kampeni ya ‘No reforms no election’ na pia akagusia namna elimu ya Tanzania ilivyo na madhaifu kwani haimfundishi mtu “Critical thinking” na kipande hiko akisema elimu ni ya kijinga ndicho kilichounganishwa na kipande kingine ili kupotosha.
Heche alisema, “tupo kwenye operesheni ya no reforms no election, bila mabadiliko hakuna uchaguzi. Na watu wote wamepanda hapa, wote wanazungumza kuhusu uchaguzi, uchaguzi, uchaguzi. Na CCM kwa sababu pia elimu yetu ni ya kijinga sana, miongoni mwa nchi ambazo zina elimu ya hovyo ambayo haifundishi watu wake critical thinking” Tazama video hiyo hapa