PreGE2025 Heche awashukia G 55, awashangaa kwenda kulamba matapishi ya mtesi wao

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
John Heche ameonesha kuchukizwa na waliokihama chama hiko wakati kama huu, ilhali watu wengi wamekufa na kuteseka ili kuwapambania wawe wabunge.

"Wengine tulipigwa risasi, tukafungwa jela kwa sababu ya kuwapambania wao wawe wabunge. Leo wameingia kwenye kitanda na wamejifunika shuka moja na mtu aliyedhulumu uhai wa Akwilina, mtu aliua watu waliompigania yeye awe mbunge'' - John Heche

Lengo eti wapate MAOKOTO,hawamuoni ZZK,pamoja na kwamba MAOKOTO anayapata kutoka chamadola,lakini moyo unamsuta kwa anachokifanya.Hela zipo tu.
 
Heche Bwana,

Aquilina alikufa akipigania nini?
Mtoto wa watu alikuwa na mishe zake tofauti, haya mambo haya.mm

Amesahau huu mchezo wa kususa ndio ulifanya taifa tukakosa katiba mpya?
Wataondoka wote subir bunge livunjwe
 
Kwa hiyo ukiwa na mishe zako tofauti na siasa ni halali kuuawa kwa risasi?
 
Heche Bwana,

Aquilina alikufa akipigania nini?
Mtoto wa watu alikuwa na mishe zake tofauti, haya mambo haya.mm

Amesahau huu mchezo wa kususa ndio ulifanya taifa tukakosa katiba mpya?
Wataondoka wote subir bunge livunjwe
Wote kina nani? Huko bungeni si kabakia Aida peke yake. Hao covid 19 walishafukuzwa zamani sana.

Tatizo hamuelewi chama ni wafuasi sio wabunge!! Sasa chadema kimeshatengeneza wafuasi mamilioni ambao majority hata kadi hawana ila wanaikubali moyoni. Sasa hao huwezi kuwabadili kisa Mrema kahama!!

Mimi napoishi huku, mstaafu wa JWTZ ndio analipia pango la ofisi ya chadema kata. Na wafanya biashara kibao wana Lodge, hardware hapa ndio wafadhili wa mikutano yote ya chadema ila hawana kadi wala huwezi waona kwenye mikutano yetu!!

Chadema is that powerful so sahauni kufa
 
John Heche ameonesha kuchukizwa na waliokihama chama hiko wakati kama huu, ilhali watu wengi wamekufa na kuteseka ili kuwapambania wawe wabunge.

"Wengine tulipigwa risasi, tukafungwa jela kwa sababu ya kuwapambania wao wawe wabunge. Leo wameingia kwenye kitanda na wamejifunika shuka moja na mtu aliyedhulumu uhai wa Akwilina, mtu aliua watu waliompigania yeye awe mbunge'' - John Heche

View attachment 3345112
Akwilina hakuwa anapigania lolote. Hakuwa katika shughuli za kisiasa alipouawa. Huo ufadhili wa Chaumma mbona haueleweki? Maana mara tunaambiwa ni Mbowe mara ni CCM.
Heche hachapigania chama chake zaidi ya Ruge na Kiwanga ambao pengine wamepigwa na kulala lock up kuliko hata yeye.
Tofauti yao na yeye ni kuwa hawakutaka kuburuzwa. Wameuliza maswali ambayo mpaka leo hajayajibu. Maswali kama: watazuiaje uchaguzi, wataendesha vipi chama bila ruzuku, watawaambia nini wanachama wao ambao mpaka hivi karibuni waliaminishwa kuwa watagomea kupitia kikao chao cha watia nia!
Walaghai ni wao, sio wakina G-55.

Amandla...
 
Uchaguzi 2020 ulibakwa 100% wagombea walipoteza Mali/pesa,muda na wanachama wa kawaida pia walipoteza pesa,muda na maisha Yao kuwa hatarini kwa vipigo na kulala lock up.

Unataka mwaka huu 2025 watu waingie kwenye uchaguzi wenye ubakaji na maumivu kwa watu??

No reforms no election
 
Kwa hiyo utazuia watu kuumizwa na kulala lock up kwa kuhakikisha hawapigi kura? Na kuwa mtashinda uchaguzi kwa kugoma kushiriki kwenye uchaguzi?
Make it make sense.

Amandla...
 
Back
Top Bottom