Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche amesema Chama hicho hakitokubali kuona Mwenyekiti wao Tundu Lissu anahukumiwa kwa kesi za kutengenezwa.
Heche ameyasema hayo leo Septemba 8 baada ya kuahirishwa kwa kesi ya uhaini inayomkabili Lissu ambaye tayari leo amewasilisha mapingamizi mawili katika kesi hiyo inayotarajiwa kuendelea tena kesho Septemba 9, 2025.
"Kwa upande wa Chama ni kwamba hakuna ubishani kwa wale tuliokuwa Mahakamani kwamba nyaraka aliyopewa Tundu Lissu na ile iliyokuwa kwenye rekodi ya Mahakama ni nyaraka mbili tofauti na amesema yeye mwenyewe, nani aliyempelekea Tundu Lissu hizo nyaraka ambazo zipo katika mfumo wa Mahakama na alipeleka kwa sababu zipi?"