Heche: ICC imeingizwa kurasa 82 zinazoeleza kwamba watu hawa waliua watu zaidi ya 3000

Heche: ICC imeingizwa kurasa 82 zinazoeleza kwamba watu hawa waliua watu zaidi ya 3000

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Makamu Mwenyekiti wa Bara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, John Heche, wakati akizungumza na umati wa wanannchi katika mkutano wa hadhara Mkoa wa Mbeya Juni 23, 2026, alieleza kuhusu kesi iliyofikishwa Mahakama ya uhalifu ya Kimataifa (ICC) kuhusu mauaji ya raifa yaliyofanyika wakati na baada ya siku ya uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025.

Aidha, aliongeza kuhusu uwasilishwaji wa Dada yake Polepole na Mke wa Tundu Lissu mbele ya Bunge la Ulaya, kwenye Tume ya Haki za Binadamu ambapo walieleza hali ya wananchi kufuatia mauaji, utekaji na ukamataji.

Soma pia

"Kwa taarifa yenu, leo nimesoma hapa nikiwa nimekaa hapa, kesi ya ICC, Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa, zimeingizwa kurasa 82 zinazoeleza kwamba watu hao waliua watu zaidi ya 3,000.

Kwa hiyo haiwezekani ukaua watu, dunia inakuambia acha kuua watu, unasema hayo ni mambo yetu ya ndani. Mauaji sio mambo yetu ya ndani, ni mambo yako na polisi na vyombo vyako ulivyovituma kuua watu, uongo kweli? Dunia haitanyamaza. Dunia haitanyamaza!

Jana mke wa Mheshimiwa Tundu Lissu na mdogo wake Polepole wamezungumza kwenye Bunge la Ulaya, kwenye Tume ya Haki za Binadamu ya Bunge la Ulaya. Na mke wake Lissu ametema Kizungu kubwa, sema Kizungu kubwa! Dunia haitanyamaza, sawa sawa?

Kwa hiyo sisi tutapiga ndani, na wengine wanapiga kule nje. Ukisimama mshale, ukikaa mshale, ukituchuma mshale"
 
Back
Top Bottom