Heche: Kauli ya Katambi kusitisha mikutano ya kisiasa si ya kisheria

Heche: Kauli ya Katambi kusitisha mikutano ya kisiasa si ya kisheria

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche amekosoa kauli ya Waziri Patrobas Katambi, akidai kuwa haina msingi wa kisheria na kwamba hana mamlaka ya kufuta mikutano ya vyama vya siasa.

Kuhusu katazo la mikutano ya kisiasa, soma Waziri Katambi apiga marufuku mikutano ya siasa kwa vyama vyote


Heche amesema
"Kwanza kauli aliyoitoa Patrobas Katambi sio kauli ya kisheria. Kwa sababu nchi hii unapotoa kauli kama waziri au kama kiongozi wa aina yoyote, lazima iwe based kwenye sheria zetu, iwe inaongozwa na sheria.

Kwa hiyo hata tamko lake alilolitaja, hajazungumza kitu chochote kuhusiana na sheria gani inamwelekeza kuwa na mamlaka hayo. Na kama ni mamlaka ya kutangaza hali ya hatari kwenye nchi, hiyo mamlaka iko kwa mujibu wa katiba ni mamlaka ambayo imetolewa kwa kiongozi wa nchi tu. Kwa hiyo hiyo kauli ya Patrobas sisi tunaichukulia kama ni mtu alikuwa anajifurahisha, ametoka nyumbani kwake amekula ugali ameshiba, akaenda kutoa hiyo kauli. Hilo la kwanza.

La pili: inathibitisha kwamba sasa hii nchi ni shamba la wanyama, ambako kila mtu anajitamkia anachotaka. Pengine huko ndio kuna rule of the jungle au survival of the fittest ambako mnyama simba anaweza kuamua tu akamtafuna swala kwa sababu anamzidi nguvu bila sababu na haulizwi na mtu yeyote.

Sasa kwa binadamu, tulishaondoa free will, tumejiwekea utaratibu wa kisheria. Na sheria ya vyama vya siasa, katiba ya nchi, sheria ya jeshi la polisi inaelekeza kwamba mikutano ya vyama vya siasa inafanywaje, utaratibu wake ukoje na haimpi mamlaka yoyote anayejiita waziri au waziri halali kufuta hiyo mikutano.

Kwa hiyo nafikiri ni jambo ambalo sisi hatukubaliani nalo, na ni jambo ambalo Watanzania wanapaswa wasikubaliane nalo kwa sababu hii tabia ya kila mtu kujiamulia anavyojiamulia, matokeo yake inafundisha nchi kuwa lawlessness ambako sasa hata watu wakigoma kulipa kodi kwa mfano, watu wakiamua ukikamatwa na polisi ukatae, watu wakiamua wakipelekwa wasiende mahakamani au wasisikilize hukumu za mahakama, sasa hiyo itakuwa nchi ya aina gani? Nchi ambayo watu hawana utaratibu kila mtu anajifanyia anavyotaka? Ndio wanachofundisha lakini sisi hatutakubali, na nafikiri na wadau wengine wote wa demokrasia duniani, vyama vya siasa, wasikubaliane na uhuni huu wa Patrobas Katambi.
 
Jambo Zuri na mwenge unaotumika kwa CCM usitishwe maana kauli zao sijui wanaangalia nini.Na waziri mkuu na wizara zake kusema chama cha mapinduzi kimefanya waache.Yule katambi hii wizara sijui kama anaelewa nafasi hii
 
Back
Top Bottom