Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, amedai kuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi, ametumwa kutengeneza propaganda za uongo ili kupata sababu za kisheria za kukifungia chama hicho kufanya mikutano ya hadhara.
Pia soma Kihongosi na CCM achaneni kuwasingizia Chadema, angalieni muungano unavunjika. Sikia maneno ya sheikh
Heche ametoa kauli hiyo jana, Juni 13, 2026, alipokuwa akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara mkoani Iringa, akijibu madai yaliyotolewa na chama tawala kuwa upinzani unaratibu vikao vya siri vya kuhamasisha vurugu nchini kupitia maandamano.
Namnukuu
"Tunaojua, Kenani Kihongosi ni spika tu, unaambiwa ng’ata au sing’ata. Kama ametoka kuzungumza, kuna waliomtuma kufanya hivyo. Wamefungia chama chetu siku mia tatu na tisa hatukufanya mkutano, tulipotoka moto ndio huu hapa, huu hapa!
Hapa hakuna aliyesombwa, hakuna aliyelipwa. Imeambiwa spika tu Heche anakuja, mwembe togwa imetapika hapa! Tuliwaambia hawana kifua cha kushindana na sisi, watapasuka! Wewe unaenda kwenye mikutano ya... unatumia milioni sitini, mimi nakuja na spika tu. Sasa ukishindana na mimi, na kuanzia wiki inayokuja tulikuwa tunaanza mikutano wilaya kwa wilaya, sasa wamegundua huu moto hawauwezi, wanatumia Kihongosi kama spika ili wafungie CHADEMA mikutano. Mnataka kuanzisha fujo nyingine.
Natumia nafasi hii, Samia nchi hii ni ya vyama vingi tangu mwaka 92. Usichochee machafuko kwenye nchi hii. Usilete vurugu. Wewe umejiweka madarakani kwa nguvu za bunduki.
Free Tundu Lissu. Lissu awe huru. Ya pili, katiba mpya. Masuala sijui ya nini na nini... ndio maana hata waandishi waliponiuliza mimi... Msigwa yule alikuwa rafiki yangu sana. Baadaye akawa adui yangu kidogo, amerudi ndio naanza kumzoea zoea kidogo. Hata waandishi waliponiuliza kuhusu Msigwa, nimewaambia atajitetea mwenyewe. Ajenda ya chama chetu ni ngapi? Mbili! Free Tundu Lissu, katiba mpya. Full stop. Na tuna sababu kwa nini tunayataka hayo, nitaeleza. Nitaeleza.
Hilo ni la kwanza nilitaka niliseme. Anachokisema kiongozi, kifua chao kinataka kupasuka, huu moto tunaowapelekea sio wa kitoto. Yaani wewe kiongozi, polisi wasijue, wewe ndio ujue kwamba CHADEMA inapangia hiyo fujo wapi? Huu mkutano wa hadhara ni fujo hii?
Waliofanya fujo ni wale watu waliouwa watu ili wajitangaze kwenye uchaguzi ambao hawakushinda wala hawakuchaguliwa. Hao ndio wanaofanya fujo kwa Watanzania. Sisi ni chama cha amani, na ni chama cha haki."