Cute Wife
Platinum Member
- Nov 17, 2023
- 3,054
- 8,449
Wakuu,
Siglada kama Siglada, ila SISIEMU
haya sasa vikao vyote vitakuwa vinarekodiwa, mkileta maigizo watu wanawatolea kanda muwaoneshe steling alisimama wapi.
====
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mhe. John Heche amesisitiza umuhimu wa kutanguliza nidhamu mbele kwa Wanachama wote wa Chadema pale wanaposhiriki kwenye ujenzi wa Chama hicho, akiwataka kujiepusha na upandikizaji mkubwa wa chuki unaofanywa ndani ya Chama hicho na baadhi ya Maafisa wa Vyombo vya Dola.
"Nyumba isiyo na nidhamu haiwezi kufanya mapambano makubwa tulinayo, tuna mapambano ambayo tukicheza tutauwawa wote na tukiruhusu miongoni mwetu watu wasiokuwa na nidhamu, watu wasiokuwa na uadilifu, wasiokuwa wakweli, watakuwa sehemu ya kutuumiza.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Tutasimamia nidhamu bila kumuonea mtu, bila kumuogopa mtu. Ndiyo hulka yetu na tutataka watu ambao wanajua kweli wanawiwa kupigania maisha ya watoto wao wasijekuishi mabaya kama haya." Amesema Mhe. Heche akizungumza na Wanachama wa Chadema wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Akizungumzia madai ya kushambuliwa kwa Mwenezi wa Baraza la Wanawake wa Chadema Sigrada Mligo aliyeshambuliwa na anayedaiwa kuwa mlinzi wake Mkoani Njombe, Heche ameagiza kuwa vikao vyake vyote vya ndani vitakuwa vinarekodiwa ili kutunza kumbukumbu na kujiepusha na wale watakaoingia kwenye mtego wa kutumika na wasioitakia mema Chadema kwaajili ya kupandikiza chuo na kutengeneza kesi dhidi ya Viongozi na wanachama wa chama hicho akidai kuwa wapo watu wanaotumia mifumo ya dola kupandikiza chuki Chadema.
Siglada kama Siglada, ila SISIEMU
haya sasa vikao vyote vitakuwa vinarekodiwa, mkileta maigizo watu wanawatolea kanda muwaoneshe steling alisimama wapi.====