Heche: Mzee Wasira Lissu sio saizi yako, Lissu atashughulika na Rais

comte

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
9,019
Reaction score
6,825
“Nimemuona Mzee Wasira, amekuwa Serikalini kwa zaidi ya miaka sitini sijui sabini tangu akiwa na miaka sijui ishirini mimi sijazaliwa, anataka atengeneze kwamba anataka kutengeneza kama mabishano flani na Mwenyekiti wetu wa Taifa, kwamba Wasira amshughulikia Lissu, Mzee Wasira Lissu sio saizi yako, Lissu atashughulika na Rais” Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, John Heche leo Makao Makuu ya CHADEMA, Mikocheni Dar es salaam.​
==============
Heche : Mzee Wasira unatakiwa kuelewa, Lissu sio size yako, anakuja kushughulika na Samia sio wewe hatuna muda na wewe, hatuwezi kufundisha Mbwa Mzee Mbinu mpya za kuwenda

Wewe unachojua ni kutoka serikali na kurudi, umeanza kulipwa mshahara na serikali ukiwa na miaka 20 mpaka leo, kwa miaka 60 unalipwa na serikali umeshiba hauna cha kuambia Gen ZNdio maana Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, ambaye amejaa shiba kama Wasira , mwenye BIMA inalipwa na Wananchi, anapigiwa Simu na mama mwenye ujauzito anamjibu nenda mumeo akakusaidia kujifungua kwa kukukata na mikasiHuyu ni mteule wa Rais, kauli yake ni kauli ya Rais.

Tutaongoza wananchi kurudisha heshima ya wananchi, ila wabunge na viongozi wakisimama wawe wanasema kwamba tunawashukuru wananchi, na sio kusema tuna mshukuru Rais maana yeye sio wa kutoa fedha ni nyie
 
Attachments

  • 1738150597636.png
    1738150597636.png
    2.6 MB · Views: 5
Kwa mtazamo wangu CCM wamemteua Wassira baada ya kuona CHADEMA wanakuja na Heche. Walijua siasa ngumu wanazokuja kufanya kina Lissu na Heche zitawabadili Watanzania waanze kuendana na tabia za watu wa kanda maalumu.

Pamoja na kwamba Wassira ni mzee na anaweza kushindwa kuendana na speed ya hawa miamba, nia ilikuwa ni hiyo. Nashindwa kufunguka zaidi ila ukitafakari nilichoandika unaweza kunielewa.

Nadhani tunarudi kwenye kipindi cha Magufuli cha CCM na Serikali kutumia nguvu kupitiliza kudhibiti wapinzani.
 
Kama kweli na hamtaki kuwaona anzanei na baba na mama zenu kwani baada ya hapo hamtamhurumia mzee yeyote
Kwenye siasa hakuna cha huruma , utabagazwa kadri utakavyokuja, so mzee atelie, G Z sio wakati wake
 
Kwa mtazamo wangu CCM wamemteua Wassira baada ya kuona CHADEMA wanakuja na Heche. Walijua siasa ngumu wanazokuja kufanya kina Lissu na Heche zitawabadili Watanzania waanze kuendana na tabia za watu wa kanda maalumu.

Pamoja na kwamba Wassira ni mzee na anaweza kushindwa kuendana na speed ya hawa miamba, nia ilikuwa ni hiyo. Nashindwa kufunguka zaidi ila ukitafakari nilichoandika unaweza kunielewa.

Nadhani tunarudi kwenye kipindi cha Magufuli cha CCM na Serikali kutumia nguvu kupitiliza kudhibiti wapinzani.
Manguvu watumie ,ila wajiandae kufika ICC this time
 
“Nimemuona Mzee Wasira, amekuwa Serikalini kwa zaidi ya miaka sitini sijui sabini tangu akiwa na miaka sijui ishirini mimi sijazaliwa, anataka atengeneze kwamba anataka kutengeneza kama mabishano flani na Mwenyekiti wetu wa Taifa, kwamba Wasira amshughulikia Lissu, Mzee Wasira Lissu sio saizi yako, Lissu atashughulika na Rais” Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, John Heche leo Makao Makuu ya CHADEMA, Mikocheni Dar es salaam.​
==============
Heche : Mzee Wasira unatakiwa kuelewa, Lissu sio size yako, anakuja kushughulika na Samia sio wewe hatuna muda na wewe, hatuwezi kufundisha Mbwa Mzee Mbinu mpya za kuwenda

Wewe unachojua ni kutoka serikali na kurudi, umeanza kulipwa mshahara na serikali ukiwa na miaka 20 mpaka leo, kwa miaka 60 unalipwa na serikali umeshiba hauna cha kuambia Gen ZNdio maana Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, ambaye amejaa shiba kama Wasira , mwenye BIMA inalipwa na Wananchi, anapigiwa Simu na mama mwenye ujauzito anamjibu nenda mumeo akakusaidia kujifungua kwa kukukata na mikasiHuyu ni mteule wa Rais, kauli yake ni kauli ya Rais.

Tutaongoza wananchi kurudisha heshima ya wananchi, ila wabunge na viongozi wakisimama wawe wanasema kwamba tunawashukuru wananchi, na sio kusema tuna mshukuru Rais maana yeye sio wa kutoa fedha ni nyie

View: https://www.instagram.com/reel/DFbDyn8iUHw/?igsh=eGtma3Byc2pqbTN0
 
Back
Top Bottom