- Source #1
- View Source #1
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la machapisho mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii. Mojawapo ya machapisho hayo linadai kuwa Heche na Golugwa wamejihusisha na ubadhirifu wa fedha ndani ya Chadema.
Chapisho hilo, ambalo limesambazwa katika vikundi na kurasa mbalimbali za Facebook, linadai kuwa viongozi hao wamejilimbikizia fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 250.
Je, upi ni uhalisia wa madai hayo yanayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii?

- Tunachokijua
- Kumekuwa na nakala ya kinachoonekana kuwa ni gazeti ikiwa na Taariafa yenye kichwa "Heche na Gulogwa wapiga mamilioni, CHADEMA yashtuka dakika za jioni", huku ndani ikielezea zaidi taarifa hiyo.
Uhalisia wa Taarifa hiyo
Baada ya ufuatiliaji imebainika kuwa Taarifa hiyo ni ya kubuni na haina uhalisia wowote kama inavyoelezwa.
Hakuna chanzo cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo, aidha hakuna taarifa yoyote rasmi kutoka katika chama hicho ikionesha kuwatuhumu viongozi hao kwa ubadhilifu huo.
Hata hivyo taarifa hiyo haitaji zaidi ni wapi walipoipata taarifa hiyo ama vyanzo walivyotumia kupata hizo taarifa ili kuongeza uzito wake.