Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche amedai kuwa jumla ya viongozi 51 wa chama hicho wamekamatwa na Jeshi la Polisi ndani ya siku mbili katika kanda tatu nchini na kubambikiziwa kesi za ugaidi.
Akitoa takwimu hizo, Heche amebainisha kuwa waliokamatwa ni pamoja na viongozi 23 kutoka Kanda ya Victoria, viongozi 17 kutoka Kanda ya Serengeti (inayojumuisha mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu), pamoja na viongozi 11 kutoka Kanda ya Nyasa.