DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
"Ni ubatili na dharau kubwa kwa Watanzania kuyaita maridhiano sasa katika mazingira ambapo serikali iliamua kwa makusudi kuwapuuza wananchi, vyama vya siasa na wadau wa demokrasia juu ya hitaji la nchi kuhusu mabadiliko (reforms) ya mifumo ya uchaguzi nchini."
"Hiki kinachoitwa maridhiano, kinatamkwa tamkwa katika mazingira ambayo serikali inaendelea na uchunguzi chini ya tume iliyokataliwa na wananchi kufanya uchunguzi wa matukio ya Oktoba 29, 2025. Watanzania wanaona hiki ni kiini macho tu"
"Ni wazi kabisa, hakuna maridhiano bila haki, na hakuna haki bila uwajibikaji. Maridhiano yanageuzwa kuwa wito wa kusonga mbele baada ya kuamua kwa makusudi kuwapuuza wananchi juu ya madai ya msingi waliyoyatoa na tahadhari walizozitoa awali"-John Heche, Makamu Mwenyekiti CHADEMA bara.