DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
John Heche, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, amekuwa mstari wa mbele katika mijadala ya kisiasa kwa njia ya mtandao, akizungumza kwa uwazi kuhusu masuala ya demokrasia, haki za binadamu, na mustakabali wa vyama vya upinzani nchini Tanzania.
Akizungumza kwa njia ya mtandao leo Septemba 19, 2025 kwa njia ya mtandao na Chama cha Safina nchini Kenya kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea nchini. Heche amesema kuwa Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imewazuia viongozi wote wa chama hicho kusafiri kwenda nchi zingine hivyo kushindwa kuungana nao uso kwa uso.
Unakijua chama cha Safina?
Safina ni miongoni mwa vyama vya siasa nchini Kenya ambacho kimejipambanua kupigania haki za kijamii, usawa na uwajibikaji wa viongozi wa umma. Chama hiki kwa sasa kinaongozwa na Jimi Wanjigi, ambaye amekuwa akisisitiza mageuzi ya kijamii na kisiasa pamoja na kuhamasisha vijana kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kidemokrasia.