GE2025 Heche: Vyombo vya ulinzi, Mahakama msiondoe imani yenu kwa umma

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Kwa matukio ambayo wanayoyafanya polisi hakika wananchi wameishiwa pawa ya kuwaamini tena na wameshatengeneza uadui mkubwa katika siku za usoni, mahakama nayo dalili zote zinaonyesha wanafanya mambo yao kwa maagizo!
===================
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara John Heche Akizungumza na wanahabari kwenye viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam muda mfupi baada ya kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Tundu Lissu kuhairishwa leo, Alhamisi Septemba 18.2025 ametoa wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama na Mahakama nchini kuzingatia weledi na kuhakikisha imani yao waliyoitengeneza kwa umma kwa muda mrefu haifutiki kwa Watanzania

Katika maelezo yake, Heche amesema ni jambo ambalo halitengenezi taswira nzuri kuona wananchi wakianza kunyooshea vidole taasisi hizo, na nyingine zinazosimamia masuala ya haki nchini hivyo mara zote zinapaswa kusimamia misingi yake ya kitaaluma na kisheria kwa kutanguliza haki.
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…