Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kaimu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche akihojia na kituo cha Redio cha VOS Juni 25, 2026 amesema "Walioitisha Maandamano Julai 7 wana haki, CHADEMA tukiitisha tutatangaza hadharani."
Heche ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti CHADEMA, Bara amefafanua kuwa haki ya kukusanyika na kuandamana imeainishwa kisheria kuanzia kwenye Katiba ya nchi, sheria ya vyama vya siasa, hadi sheria inayoratibu jeshi la polisi (The Police Services and the Auxiliary Act).
Alitolea mfano wa kihistoria kuwa hata Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kuongoza maandamano mwaka 1954 kupinga ukoloni, akisisitiza kuwa jamii isijaribu kupaka matope au kufanya maandamano kuonekana kama ni jinai au kitu kibaya, kwani ni njia halali ya kisheria inayotumiwa na raia, asasi za kiraia, na makanisa kufikisha ujumbe maalum.