mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 20,458
- 36,481
Wakuu,
Heche amesema hayupo tayari kusimamia uongo, kama wanasema chama kitakufa na kife lakini sio kuendeleze uongo wa CCM!
Safari hii mama anaupiga mwingi mtanyooka! Wanatetemeka huko waliko, mwengo wa kutafuta kiki za kupuuzi kututoa kwenye reli, safari hii mtaisoma namba kama nyimbo yenu inayvyosema!
====
"Maadili gani hayo tukasaini? wanatutishia kuwa Chadema itakufa isiposhiriki uchaguzi, uchaguzi gani? Chadema itakufa hii? na ife kama tutasimamia jambo la kweli na watu wasijue kama tunasimamia ukweli na ife kama tunasimamia uongo, Kuliko kuwa na chama tunachosimamia uongo, tuko tayari sisi wengine kuacha hizi siasa.
"Kama mnataka mimi Heche na Lissu tusimamie uongo mimi sipo tayari sehemu ambayo na-risk maisha yangu, wakati wote nawindwa! halafu nasimamia uongo ninaoukataa CCM, mimi nina uwezo wa kwenda CCM na nikapata nafasi." - Heche Makamu Mwenyekiti CHADEMA leo Aprili 12, 2025 Mkoani Mbeya.
Ilishakufa mbona???
Siku alipochaguliwa tundu chadema ilikufa
