Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche amesema wapo baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaounga mkono kauli ya chama hicho ya bila mabadiliko hakuna uchaguzi inayojulikana kama 'no reforms no election'.
Akizungumza katika mahojiano na chombo kimojawapo cha habari nchini Heche amesema kwamba baadhi ya wana CCM hawapendi mfumo uliopo wa uchaguzi hivyo kuamua kuunga mkono mabadiliko ya mfumo huo kama ambavyo vyama upinzani vimekuwa vikisisitiza.
"Hakuna mtu nchi hii ambae hajui kwamba mfumo wetu wa uchaguzi ni mbovu, hata watu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ukiongea nao utasikia mtu anasema yaani mambo yanayofanyika mpaka naona aibu, wapo wanaotuunga mkono" amesema Heche.
CHANZO: Nipashe