Heka kumi za bangi zateketezwa Arusha

Heka kumi za bangi zateketezwa Arusha

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema kuwa limefanikiwa kuteketeza dawa za kulevya aina ya bhang hekari kumi Pamoja na kukamata maguni themanini ya dawa hizo huku Jeshi hilo likibainisha kuwa litaendelea na operesheni kali ya kuwasaka wale wote walio kimbia na wanaojihusisha na biashara hiyo haramu.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema mafaniko hayo yametokana na operesheni iliyofanyika mei 26,2024 huko katika maeneo ya kisimiri Wilaya Arumeru Mkoa wa Arusha dhidi ya dawa za kulevya.

Kamanda Masejo amewataka Wananchi wa Mkoa huo kuachana na biashara hiyo haramu ya dawa za kulevya ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo halito mwonea muhari mtu yeyote atakaye bainika kutumia pamoja na kujihusisha na biashara hiyo.

SACP Masejo amewaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo kwa kutoa taarifa za baadhi ya watu wanaojihusisha na matumizi Pamoja bishara hiyo.
 
Ila kuna watu wachawi alooo....😜
Maana jamaa anatisha hadi mkoa mzima unatikisika...🤣
Na migambo wanakanyagana, wanaruka kinyama..😝
 
Hahaha aisee cha arusha kitaadimika. Heko Makonda
 
Back
Top Bottom