Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu eneo hilo ni hivi, kuita kwa kiganja ni pale anapopishana na gari nyingine so akimpa ishara ya kuita ni anamruhusu anayepishana naye kuwa aendeshe bila wasiwasi hakuna shida aendapo.mara anainua kama vile anaita yani alikuwa anapata taarifa nje ya basi na yeye alifikisha ujumbe kwa dereva kwa kupiga dashboard, kuinua kiganja na kuita kwa kiganja.
Nikienda ku nya nikirudi takuta ume summarize au..?Mmeanza,imepigwa bandika bandua ambayo huwa mnataka,sasa unadai usummaraiziwe pim bi w e w
sIo lazima kila mtu asome,kama huwez ka n y e
Ahsante sana mpendwa nimeisoma yote nashukuru sana Bosia wangu AntonniaAsante sana mkuu Hebu nitulie nisome vizuri!!
Lovelovie Bantu Lady Tayukwa leadermoe moneytalk Unforgettable
Yt5<81d,Sammary kwa maneno yasiyopungua 150...
DfY5<81d,*DfYt5<81d,
Vipi na weye umeimalizaPamoja sana mkuu Enjoy the story!!✌️✌️
Bado hata episode ya pili sijaianza eti!!Vipi na weye umeimaliza
Jitahidi umkute Bosia mwenzakoBado hata episode ya pili sijaianza eti!!
Mkuu ni fupi sana,achana nahao wanaokomaza mafuvu mara ndefu sana nyenye nyenye nyingi..tupia ndefu bna.MSIMU WA PILI
Season II
Hekaheka Uzeeni
(i). Ugomvi, Suluhu, Faida.
Ilikuwa siku ya alhamisi mchana Hamida alipokuja kunipokea Ubungo bus terminal. Nikiwa mwenye furaha ya kumuona mke wangu lakini yeye alikuwa amenuna njia nzima tulipokuwa tunaelekea Kariakoo kumsindikiza Bosio hoteli ambayo aliambiwa na wakala wake afikie. Aliendesha Nadia yake kwa kasi ingawaje foleni za hapa na pale zilikuwa zinamzuia asikimbie kwa muda mrefu.
“Atafikia Sleep inn hotel ya Kariakoo…” nilisema wakati mwendo wa gari ulikuwa umekolea baada ya kupita taa za mtaa wa Msimbazi na Morogoro rd.
Ni kwa bahati tu taa nyekundu zilituzuia kuendelea lakini dalili za kulala na speed zote niliziona. Baada ya taa kuruhusu alikunja kuingia barabara ya Lumumba, njia ilikuwa na magari mengi hivyo hakuweza kulipelekesha gari.
“Ingia mtaa wa Mahiwa..” nilimuelekeza Hamida.
Mbele kidogo jirani kabisa na mtaa wa ‘jiwe linaloishi’ akapaki na Bosio akashuka na kushukuru kwa lifti.
“Merci Papaa pulabalade…” Alisema akimaanisha anashukuru kwa lift.
Nikafunga mlango na kurudi kwenye siti yangu na kufunga mlango na mkanda, mara nikasikia..
“Mercii ya nyoko!”
Nikamwangalia wife kisha nikatikisa kichwa na kukaa kimya. Safari iliendelea hadi tulipofika nyumbani tukiwa kama mabubu maana niliamua nijizuie kusema lolote. Nyumbani nikashusha mizigo vizuri na begi langu yeye akiwa bado amenuna na kuelekea jikoni.
Uzuri wa Hamida ni kwamba, hata kama amenuna huduma zingine zote anakupatia vizuri tu, hivyo sikuwa na wasiwasi wa kunyimwa huduma za nyumbani.
Baada ya kuoga kuliko nichukuwa muda mrefu, nikajiandaa na kuelekea sehemu ya maakuli ambako nilikuta ameniandalia chakula changu pendwa kama kawaida. Nikakaa chini ‘mkekani’ na kuanza kula peke yangu.
Baada ya chakula nikapitia mitandao ya kijamii kidogo kisha nikaenda kijilaza chumbani. Saa kumi na mbili kasoro hivi niliamshwa kwa voice call ya whatsapp kutoka kwa Janeth.
“Du hekeheka uzeeni hizi…”, nilijisemea.
“Halo, habari, ulifika salama?” ilikuwa sauti ya Janeth akiongea.
Nilimjibu na kuongea naye mawili matatu, mara Hamida akaingia na kukaa jirani huku akisikiliza. Ila nyie wanawake, Mungu anawaona. Muda wote mko na hisia hisia tu. ‘Anyway’ (siyo ‘anyways’), ndivyo jinsi mlivyoumbwa.
“Hii simu ni kutoka nje ya nchi, ni familia iliyonifadhili kule Kigali wakati wa ‘lockdown’ wanataka kujuwa kama nilifika salama…” nilijitetea baada ya kukata simu.
“Enhe, hebu niambie, yule mwanamke tuliye mshusha kule hotelini ni nani!” aliuliza Hamida kwa hamaki.
Ikanichukuwa muda mrefu kumuelezea kuanzia pale mpakani Gatuna jinsi tulivyokutana na safari yetu hadi tulivyofika na kwamba hakuna kinachoendelea. Baada ya majibizano ya muda mrefu hatimaye alikubali kushuka chini na kuomba afungue mizigo yangu akague. Ila wanawake! Nimewavulia kofia.
Akajifanya anatenganisha nguo chafu na safi na kuziweka sehemu zake, akakung’uta begi kuhakikisha hakuna kitu kilichobaki kisha akahamia kwenye mzigo mwingine ambao ndani kulikuwa na vitenge vyake.
Kwenye ule mzigo, vile vitenge vya dola 50 hamsini niliviweka juu na vile vya dola 80 themanini niliviweka chini. Sasa alivyoanza kufungua ule mzigo akaanza kusasambua na kuvirusha kitandani…
“Hivi si ni sawa tu na vya Kitumbini! Wala hakuna tofauti yoyote..” alikuwa aking’aka kama vile bado ana kitu rohoni.
Mara paap akavifikia vile wax orijino! Nikaona tu anatabasamu na kusema…
“Hivi sasa ndio vitenge…”
Aliendelea kuvichambua vyote na kuishia kusema vizuri sana, ahsante! Akanikumbatia pale kisha akaviweka vizuri.
===
Usiku ule ulikuwa murua kwani nilifanya zoezi la kilimo cha umwagiliaji na kufanikiwa kama wafanyavyo wakulima wa Kinyarwanda lakini nilibandikwa maswali ambapo majibu yake ndiyo yaliyoleta ugomvi na kusameheana baadaye.
Ni kwamba Hamida alikuwa anamfahamu Janeth na familia yao kwakuwa tulikuwa tunawasiliana kwa ‘video call’ na alikuwa ameongea na watu wote ndani ya ile nyumba (Kigali), lakini hakuwa amedhani kwamba nimechepuka na mmoja wao hadi aliponibana kwenye kilimo cha umwagiliaji.
Ilikuwa ni ulimaji tofauti na aliouzoea, tulio uzoea!, ingawaje hata kabla ‘kilimo kwa kumwagilia’ kilikuwa kunafanyika. Sasa hii ‘pro max’ aliona ni tofauti sana na kunibana nimueleze nilipojifunzia. Nikaamua kusema ukweli kuwa Janeth alinifundisha. Mama yangu! Kilichofuata hakiandikiki.
Lakini mwisho wa yote vile vitenge vilimpooza na kumwambia vile vya ziada yeye aamue nani ampe na nani asimpe lakini kali kuliko yote alitaka tena kumwagilia bustani.
Baada ya kuridhika kuwa bustani imelowana maji vya kutosha akatulia na kusema…
“…lakini tamu…” Nimekusamehe, lakini utanipeleka ‘shopping’ ninapopataka mimi kama fidia.
Kusikia hivyo mzee mzima nikataka sasa nipeleke moto ile kibongobongo lakini mjamaa kichwa wazi ‘akazila’ kabla hata moto haujakolea, nikajikuta tu nasema hii sasa ni hekaheka uzeeni. Ilibidi kuahirisha zoezi na kupisha mwili na akili vikae sawa hadi kulivyokucha asubuhi.
ITAENDELEA...