Hekaheka Uzeeni

mara anainua kama vile anaita yani alikuwa anapata taarifa nje ya basi na yeye alifikisha ujumbe kwa dereva kwa kupiga dashboard, kuinua kiganja na kuita kwa kiganja.
Mkuu eneo hilo ni hivi, kuita kwa kiganja ni pale anapopishana na gari nyingine so akimpa ishara ya kuita ni anamruhusu anayepishana naye kuwa aendeshe bila wasiwasi hakuna shida aendapo.

Na kupiga dashboard ni ishara kwa dereva waliye naye akanyage pedo/mafuta mbele kweupe, nk.
 
MSIMU WA PILI
Season II

Hekaheka
Uzeeni

(i). Ugomvi, Suluhu, Faida.

Ilikuwa siku ya alhamisi mchana Hamida alipokuja kunipokea Ubungo bus terminal. Nikiwa mwenye furaha ya kumuona mke wangu lakini yeye alikuwa amenuna njia nzima tulipokuwa tunaelekea Kariakoo kumsindikiza Bosio hoteli ambayo aliambiwa na wakala wake afikie. Aliendesha Nadia yake kwa kasi ingawaje foleni za hapa na pale zilikuwa zinamzuia asikimbie kwa muda mrefu.

“Atafikia Sleep inn hotel ya Kariakoo…” nilisema wakati mwendo wa gari ulikuwa umekolea baada ya kupita taa za mtaa wa Msimbazi na Morogoro rd.

Ni kwa bahati tu taa nyekundu zilituzuia kuendelea lakini dalili za kulala na speed zote niliziona. Baada ya taa kuruhusu alikunja kuingia barabara ya Lumumba, njia ilikuwa na magari mengi hivyo hakuweza kulipelekesha gari.

“Ingia mtaa wa Mahiwa..” nilimuelekeza Hamida.

Mbele kidogo jirani kabisa na mtaa wa ‘jiwe linaloishi’ akapaki na Bosio akashuka na kushukuru kwa lifti.

“Merci Papaa pulabalade…” Alisema akimaanisha anashukuru kwa lift.

Nikafunga mlango na kurudi kwenye siti yangu na kufunga mlango na mkanda, mara nikasikia..

“Mercii ya nyoko!”

Nikamwangalia wife kisha nikatikisa kichwa na kukaa kimya. Safari iliendelea hadi tulipofika nyumbani tukiwa kama mabubu maana niliamua nijizuie kusema lolote. Nyumbani nikashusha mizigo vizuri na begi langu yeye akiwa bado amenuna na kuelekea jikoni.

Uzuri wa Hamida ni kwamba, hata kama amenuna huduma zingine zote anakupatia vizuri tu, hivyo sikuwa na wasiwasi wa kunyimwa huduma za nyumbani.

Baada ya kuoga kuliko nichukuwa muda mrefu, nikajiandaa na kuelekea sehemu ya maakuli ambako nilikuta ameniandalia chakula changu pendwa kama kawaida. Nikakaa chini ‘mkekani’ na kuanza kula peke yangu.

Baada ya chakula nikapitia mitandao ya kijamii kidogo kisha nikaenda kijilaza chumbani. Saa kumi na mbili kasoro hivi niliamshwa kwa voice call ya whatsapp kutoka kwa Janeth.

“Du hekeheka uzeeni hizi…”, nilijisemea.

“Halo, habari, ulifika salama?” ilikuwa sauti ya Janeth akiongea.

Nilimjibu na kuongea naye mawili matatu, mara Hamida akaingia na kukaa jirani huku akisikiliza. Ila nyie wanawake, Mungu anawaona. Muda wote mko na hisia hisia tu. ‘Anyway’ (siyo ‘anyways’), ndivyo jinsi mlivyoumbwa.

“Hii simu ni kutoka nje ya nchi, ni familia iliyonifadhili kule Kigali wakati wa ‘lockdown’ wanataka kujuwa kama nilifika salama…” nilijitetea baada ya kukata simu.

“Enhe, hebu niambie, yule mwanamke tuliye mshusha kule hotelini ni nani!” aliuliza Hamida kwa hamaki.

Ikanichukuwa muda mrefu kumuelezea kuanzia pale mpakani Gatuna jinsi tulivyokutana na safari yetu hadi tulivyofika na kwamba hakuna kinachoendelea. Baada ya majibizano ya muda mrefu hatimaye alikubali kushuka chini na kuomba afungue mizigo yangu akague. Ila wanawake! Nimewavulia kofia.

Akajifanya anatenganisha nguo chafu na safi na kuziweka sehemu zake, akakung’uta begi kuhakikisha hakuna kitu kilichobaki kisha akahamia kwenye mzigo mwingine ambao ndani kulikuwa na vitenge vyake.

Kwenye ule mzigo, vile vitenge vya dola 50 hamsini niliviweka juu na vile vya dola 80 themanini niliviweka chini. Sasa alivyoanza kufungua ule mzigo akaanza kusasambua na kuvirusha kitandani…

“Hivi si ni sawa tu na vya Kitumbini! Wala hakuna tofauti yoyote..” alikuwa aking’aka kama vile bado ana kitu rohoni.

Mara paap akavifikia vile wax orijino! Nikaona tu anatabasamu na kusema…

“Hivi sasa ndio vitenge…”

Aliendelea kuvichambua vyote na kuishia kusema vizuri sana, ahsante! Akanikumbatia pale kisha akaviweka vizuri.
===

Usiku ule ulikuwa murua kwani nilifanya zoezi la kilimo cha umwagiliaji na kufanikiwa kama wafanyavyo wakulima wa Kinyarwanda lakini nilibandikwa maswali ambapo majibu yake ndiyo yaliyoleta ugomvi na kusameheana baadaye.

Ni kwamba Hamida alikuwa anamfahamu Janeth na familia yao kwakuwa tulikuwa tunawasiliana kwa ‘video call’ na alikuwa ameongea na watu wote ndani ya ile nyumba (Kigali), lakini hakuwa amedhani kwamba nimechepuka na mmoja wao hadi aliponibana kwenye kilimo cha umwagiliaji.

Ilikuwa ni ulimaji tofauti na aliouzoea, tulio uzoea!, ingawaje hata kabla ‘kilimo kwa kumwagilia’ kilikuwa kunafanyika. Sasa hii ‘pro max’ aliona ni tofauti sana na kunibana nimueleze nilipojifunzia. Nikaamua kusema ukweli kuwa Janeth alinifundisha. Mama yangu! Kilichofuata hakiandikiki.

Lakini mwisho wa yote vile vitenge vilimpooza na kumwambia vile vya ziada yeye aamue nani ampe na nani asimpe lakini kali kuliko yote alitaka tena kumwagilia bustani.

Baada ya kuridhika kuwa bustani imelowana maji vya kutosha akatulia na kusema…

“…lakini tamu…” Nimekusamehe, lakini utanipeleka ‘shopping’ ninapopataka mimi kama fidia.

Kusikia hivyo mzee mzima nikataka sasa nipeleke moto ile kibongobongo lakini mjamaa kichwa wazi ‘akazila’ kabla hata moto haujakolea, nikajikuta tu nasema hii sasa ni hekaheka uzeeni. Ilibidi kuahirisha zoezi na kupisha mwili na akili vikae sawa hadi kulivyokucha asubuhi.

ITAENDELEA...
 

Attachments

  • BOSIO1.jpg
    25.6 KB · Views: 69
  • Janeth1.jpg
    64.4 KB · Views: 79
Mkuu ni fupi sana,achana nahao wanaokomaza mafuvu mara ndefu sana nyenye nyenye nyingi..tupia ndefu bna.
 
(ii). Kazini tena, ‘Connection’, Fadhila.

Ugomvi uliisha kabisa nyumbani nikabakiwa na deni la kumpeleka ‘shopping’ Hamida ambako bado alikuwa hajapataja, ni kwa sababu ya uviko19 na mazuio ya kuingia baadhi ya nchi bila shaka. Maisha yaliendelea kama kawaida.

Bosio alifanikiwa kutoa kontena lake badarini, lakini baada ya kuingilia kati na kujikuta nakuwa wakala asiye rasmi kumsaidia ili ‘asipigwe parefu’. Ni kwamba alitakiwa kulipia ushuru zaidi ya milioni mia tatu kana kwamba mzigo utaishia Tz (hata kama) na bado mawakala aliowatumia (wakongoman wenzake walio lowea Dar) walikuwa wamemuwekea gharama nyingine zisizo na kichwa wala miguu. Alivyonieleza kuwa kupitisha mzigo Tanzania ni ghali mno kuliko Kenya au Kinshasa kwa ndege na kuonesha hali ya kukata tamaa ndipo nikaomba nyaraka zake ili nizipitie.

Salaleee!, alikuwa anapigwa parefu! Ni kweli kuwa kupitisha mzigo wa vitenge bandari ya Dar es Salaam ni ghali kulinganisha na nchi jirani na hata ambazo zipo ‘landlocked’ lakini ile ilikuwa imezidi. Baada ya wale mawakala wake kuona mimi nimeingilia kati zoezi lile ‘walisusa’ kumhudumia wakitaka mimi niifanye kazi ile kwani nimeingilia kazi za watu.

Mzee mzima nikaingia ‘front’ na kuwakabili watoza ushuru na kuanza kukubaliana nao. Nilikuta wameshawalisha watoza ushuru ‘maneno’, lakini niliwapa ‘fact’ za ushuru kwa mzigo kama huo kwa bandari ya Mombasa, Msumbiji na hata Zambia lakini cha ajabu hata bandari ya Unguja bei haikuwa juu kiasi hicho, na zaidi ya yote mzigo ni wa 'transit'.

“…uliyoyasema ni kweli lakini sasa sisi tuna miongozo na ndiyo tunayoifuata…” alisikika mtoza ushuru mmoja ingawaje alionekana kuelewa na kuonesha dalili za ‘kuzungumzika’.

Kama kuna sehemu Serikali yetu inapoteza mapato basi ni pamoja na ushuru wa forodha, maana kwa viwango vilivyowekwa ambavyo havilipiki, kwa maana ya kwamba ukilipa huko mtaani kwenye biashara yenyewe sasa unaangukia pua, inaweka nafasi ya ‘mazungumzo’ kati ya afisa mhusika / wahusika na mfanya biashara moja kwa moja ama kupitia wakala wake.

Ilibidi kutumia upenyo huo kupunguza hayo mamilioni na kufanikiwa kulipa kadhaa na kadhaa kupotelea mifukoni mwa watu. Bosio alinishukuru sana baada ya kuona mzigo hatimaye umepata ‘release!’ kwa gharama chini ya nusu ya iliyotakiwa kutumikwa mwanzo.

Kwa msaada wa kaka zake Janeth tukapata lori la kubeba kontena ambalo lilikuwa la Rwanda na linakaribia kuingia Dar kurudisha kontena lingine. Ule mzigo tuliutoa yard ya bandani na kuuweka nje jirani tu bandaridi kwa kuegesha kimtindo kwenye kichanja (lori) ambacho tulikodi, ili asipate gharama za ziada, nilikweka ulinzi wa kuaminika na baada ya siku moja tu lile lori likawa tayari kubeba mzigo ule. Bosio alifurahi kwa juhidi zote nilizofanya na mie sikumuacha kwa maneno ya kumkumbusha…

“Unakumbuka ulisema mimi sijui kupiganisha kutosha mizigo kule Mtukula?” nilisema huku natabasamu.

“Papaa uko bien! Umefanya kazi ya mingi sana, merci Papa…” alisema kwa unyenyekevu tulipokuwa tumeliacha lile lori likianza safari kuelekea Burundi kisha Bukavu na sisi tukawa tunarudi hotelini kwake kutafakari zoezi zima na kuagana.

Kumbuka msomaji kipindi hicho hali ya uvoko19 ilikuwa mbaya sana na mipaka ya nchi jirani ilikuwa imefungwa.

“Sasa nitaondoka aee kwenda kumwetu…” “..sipandi malori tena niko nachoka sana…” alisema Bosio akiomba ushauri jinsi ya kufika Burudi halafu Bukavu.

Nikamwambia atapanda ndege hadi Kigoma, pale atakamata ‘mchomoko’ (gari ndogo) hadi Manyomvu na kuvuka mpaka kuingia upande wa Burundi hapo atapata usafiri hadi Bujumbura ambako atapata usafiri wa kufika Bukavu kwa urahisi. Alikubaliana na lile wazo na akili yake sasa ikawa imetulia. Harakati zote za kumsaidia Bosio, Hamida alikuwa anajuwa lakini hakutaka Bosio aje nyumbani sijui alikuwa anahisi nini.

Baada ya hesabu zake pale hotelini Bosio alinipatia ahsante ya hela kadhaa ambazo kwa kweli sikuzikataa maana nilimuokoa pakubwa na pia hali yangu ya kifedha ilikuwa ya kuunga unga kuliko nilivyokuwa kazini. Nilimshukuru na kumwambia akiagiza mzigo mwingine anijulishe ili wakati wa kuandaa ‘bill of lading’ nijuwe ‘A to Z’ kabla haijatumwa ‘kunako’ kwa ‘Zakayo’ kutoka huko ughaibuni.

Katika maongezi tukajikuta tumegusa suala la uhusiano (neno mahusiano si sahihi kwenye Kiswahili sanifu). Akaniambia moyo wake umekufa juu ya mapenzi…

“Mapenzi! Mtima umekufa Papaa, situmikishi tena mambo ya mapenzi, juu yanini kuumiza mtima wangu…” akimaanisha hataki kusikia kuhusu mapenzi kwani alishaumizwa. Alifunguka simulizi yake ambayo tutaiona huko mbele.

Aliyesema kuwa mwanamke na mwanaume wote wakiwa na afya njema lakini si ndugu wasikae pamoja kwa muda mrefu bila kuwepo na mtu mwingie yupo sahihi. Sijui kilitokea nini lakini alijikuta akilia na kuniegamia wakati akiendelea kusimulia stori yake. Ibilisi akatupitia, tukabembelezana kwa mara ya kwanza na ya pili kujaribu kufanya kilimo cha bustani kwa kumwagilia lakini kisima hakikuwa na maji ya kutosha ingawaje bustani ilipata maji.
===

Niliporudi nyumbani nilimkabidhi Hamida zile hela nikamwambia ni moja ya sehemu ya kwenda kufanya ‘shopping’ huko atakako na kwamba nimepata kibarua kingine cha ku ‘clear’ mizigo bandarini kwa ujira mzuri na kwamba inabidi kesho tukamsindikize Bosio uwanja wa ndege ili arudi kwao.

Safari hii Hamida hakuonesha uso wa ‘makasiriko’ bali alikuwa kawaida ilhali sasa ndio ameonjewa kuliko pale mwanzo alipokuwa amekasirika kwa hisia. Sijui akisoma hii post atakuwaje, ila ‘mavi ya kale hayanuki’ na nilishatubu dhambi hizi. Hakika kwa mwanamume rijali mke mmoja hatoshi.

Nilipata shukrani nyingi kutoka kwa mama yake Janeth kwa kuwafanya wanawe (kaka zake Janeth) kuwa ‘active.’ Eti tangia nimeondoka mazungumzo yao yamekuwa ya kikazi zaidi kuliko starehe. Nilisoma ule ujumbe wa mama Janeth kupitia simu ya Janeth mwenyewe akinishukuru pia kwa kuwapatia pesa kama ahsate ya kutafuta lori. Kwa ujumla safari ya kwenda Goma pamoja na kadhia nilizopata zilizotokana na uviko19 lakini imenipa ‘connection’ iliyonisaidia sana katika kipindi cha ‘kiangazi cha hela’.
===

Hatimaye Rwanda lockdown ikaisha na mpaka ukafunguliwa, ingawaje kwa masharti ya kuwa umechanjwa moja ya chanjo za uviko19 pamoja na tahadhari zingine, biashara zikafunguka na nikapata taarifa za ujio wa Janeth na kaka yake mmoja kuja Tanzania kununua bidhaa za dukani. nikaona hii ni fursa ya mimi kurudisha fadhila ya ukarimu niliooneshwa Kigali na pia kuondokana na ile hali ya kuzubaa tu nyumbani kukaribisha magonjwa yasiyo ambukiza.

Kwa kuwa nilimdokeza machimbo ya bidhaa kutoka China na Thailand pale Kariakoo, akaniomba niwepo Ubungo siku akifika na kumuononesha hayo machimbo na namna ya kupunguza matumizi pasi na kuhatarisha maisha yao huko mitaani. Tarehe husika nilifika Ubungo nikiwa na Hamida kwa ajili ya kuwapokea wageni kutoka Kigali nikiwa na gari yangu ya 'shamba' Toyota Hilux 2.8D, na punde si punde likaingia basi kutokea Bukoba ambalo ndilo alisema wamepanda.
===


ITAENDELEA...
 

Attachments

  • BOSIO2.jpg
    38.7 KB · Views: 69
  • BOSIO4.jpg
    38.5 KB · Views: 59
(iii). Cute Eyes – Macho mazuri ‘analia’ juu ya mapenzi.


Bosio ni mtoto wa pekee katika uzao wa tumbo la mama yake, hana kaka wala dada na baba yake alishafariki wakati akiwa mdogo. Baba yake alikuwa ni kabila la wabembee na mama yake ni kabila la myombe. Ilikuwa familia yenye maisha ya chini, baba yake alifariki migodini huko katika harakati za kutafuta ugali wa mke na mtoto wao wa pekee.

Ingawaje Bosio alikuwa katika maisha ya dhiki lakini uzuri wake haukujificha ukichagizwa na macho yake mzuri hata wazazi wake waliliona hilo tangia utoto na kumpatia jina la Beaux yeux, aka Bosio. Mama yake alimlea kwa shida binti yake ili apate masomo vizuri na kwa kudra za mwenyezi Mungu Bosio alimaliza masomo ya sekondari.

Katika kupitapita akakutana na kijana ambaye alikuja kumuoa na kuzaa naye watoto wawili mmoja wa kiume na mwingine wa kike. Mume wake huyo alikuwa ni askari ya jeshi la nchi yao na katika harakati za kuilinda nchi alifariki kishujaa akiwa kazini. Faraja kwa Bosio ikawa na wale watoto na mama yake. Kwakuwa mume wa Bosio alikuwa katika ‘mission’ ya kimataifa, alipata kifuta machozi kiasi fulani cha fedha ambacho sehemu ya hiyo hela ndio alianzisha biashara ya kunua na kuuza vitenge jijini Kishasa. Biashara zake ziliendelea vizuri kwakuwa Bosio alikuwa na nidhamu ya hela na historia ya hali ngumu kulikomfanya azidi kuwa makini katika kila jambo ili awatunze watoto na kumlea mama yake kipenzi.

Katika harakati za biashra ndipo alikutana na mpenzi huyu sasa aliye muumiza kiasi cha kutotamani tena kusikia neno mapenzi.

“…tulikalaga naye tunatumikisha biashara mzuri lakini kumbe mwenzangu ako na mambo ya mingi… “ ilikuwa na sehemu ya maelezo ya Bosio.

Kwanza jamaa huyo alikuwa Mario, yaani alikuwa hapendi kujishughulisha kutafuta bali alikuwa akimtegemea Bosio kwa kila kitu, alikaa kama kupe. Pili alikuwa anatembea na wanawake wengi…

“…aliikala kwangu, akawa mupinki muzuri lakini akaanza kutomboka tomboka juu ya madamee wengine…”

“…Kuna siku moya nimetoka Bukavu nikamuta ako na madamee mwingine mu nyumba yangu bako banabukana…”

“…iiii nililia siku hiyo na kumfukuza atoke ku nyumba yangu aendage…”

“…aendage tu iko na mambo ya mingi sana…” kilio kikaanza…

Hapa ilikuwa ni pale sleep in hotel Kariakoo Dar akinihadithia, ndipo akaweka kichwa chake kwenye bega langu na kuangua kilio tena chenye kwikwi.

Baada ya kubembelezana, peleka moto kidogo na kurudi kawaida akaendelea kusimulia…

“..Ndo vile nikaamua basi tena, nitakaa peke, juu nimeishi maisha magumu tangia niko mudogo, kila siku kunidanjere danjere nimechoka!...”

“…Alitoka na baadhi ya faranga zangu, sikujali, nilitaka atoke tu aende, yani aende!...”

“…Ndiyo nikaanza kupiganisha biashara ya vikwembe (vitenge), nikaanza kuchukuwa vikwembe vyenyewe vya byee ndio niko nakuza mutaji na sasa naweza kamata kontena moja peke ndio napiganisha biashara iende muzuri…”

Tangia apate pigo hilo aliamua kupambana, na hakika amefanikiwa katika kupambana kwakuwa hakuwa na mambo mengi tena, yeye na mama yake na watoto wake akisomesha katika shule nzuri huko Kinshasa.

Nikampachika swali la kizushi.

“Sasa Bosio, unakula unashiba, viungo vingine havisikii njaa?!”

Baada ya kulielewa swali alicheka kisha akajibu ya kuwa anajisaidiaga mwenyewe, hapati magonjwa wala ‘stress’.

Ukimya ulitawala na hatimaye tukajaribu kumwagilia bustani kwa maji hafifu ‘though’.

Nikawa kama nimechokoza vilivyo lala ingawaje sikuwa na mpango wa kuchonga mzinga bahati nzuri muda wa yeye kusafiri ndio ulikuwa umefika na tulimsindikiza na Hamida airport kama nilivyoeleza huku nyuma.
===



ITAENDELEA…



(fupi fupi tamu eee)
 

Attachments

  • BOSIO3.jpg
    34.3 KB · Views: 70
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…