Hekaheka

Hekaheka

Shengesha

Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
5
Reaction score
0
Siku za hivi karibuni katika kijiji cha Kizito mtaa wa Hakibebeki kulitokea jambo la ajabu sana ambapo kijana mmoja aitwae Kifo alisababisha kustopisha shughuli za watu wote na majirani wakaribu wa kijiji cha Kizito mtaa wa Hakibebeki.

Hii imetokea baada ya tajiri mmoja aitwae Nduli kumtuma Kifo kwenda kuziba mirija ya pumzi ya Hakiepukiki wakati akiwa katika harakati za patashika nguo chanika.

Akipambana na adui yetu Shiba, kwa ghafla baada ya Kifo kufika alianguka nakulala fofofo huku akipitwa na mashuzi makali.

Sekunde chache baadae ubaridi ulitawala katika mwili wa Hakiepukiki na hapo ndipo shughuli za wana mtaa wa Hakibebeki walipositisha shughuli zao nakukusanyana katika kijiji cha Kizito.

Baada ya muda, wote walionekana wakielekea katika viwanja vya Tujihadharini ambako ndipo hitimisho la mkusanyiko ule utafanyika.
 
Back
Top Bottom