Hekaya za Abunuwasi

Hekaya za Abunuwasi

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001

HEKAYA ZA ABUNUWASI


KISA CHA ABUNUWASI NA MFALME

SIKU moja alfajiri, wakati wananchi wa mji wenye wakazi wengi walipokwenda kuchota maji mtoni, walishangazwa kuuona mkono wa mtu ukiwa katikati ya mto. Mkono huo wa ajabu ulikuwa umenyoosha vidole viwili juu, kuonyesha alama ya mbili.

Wananchi walistushwa sana na kitendo hicho, wakaogopa hata kuchota maji mtoni, kwani hawakuwahi kuona tukio la kuogopesha kama lile. Wengine waliamini kuwa huo ulikuwa mwili wa mtu aliyetupwa mtoni.

Lakini ishara iliyoonyeshwa na mkono huo iliwafanya wananchi waamini kuwa huo ulikuwa mkono wa ajabu. Katika kiza kinene kilichozunguka ndani ya vichwa vya wananchi, habari zikamfikia Mfalme wao, naye akafika haraka eneo la tukio.

Mfalme wa nchi hiyo baada ya kujiridhisha kuwa ulikuwa mkono wa ajabu na uliwekwa na watu wenye imani za kishirikiana, alitoa siku tatu mkono huo uwe umeondolewe, vinginevyo ataleta wataalam kutoka sehemu mbali mbali duniani kwa ajili ya kubaini wahusika.

Siku tatu zilizowekwa na Mfalme zikaisha, wataalam wa mambo ya asili kutoka sehemu mbali mbali duniani wakaanza kuwasili mtoni hapo kwa lengo la kuundoa mkono huo wakashindwa.

Mfalme akatoa ofa nono, waganga wenye sifa na jeuri ya mambo ya jadi wakamiminika eneo la mto, wakafanya mitambiko na mambo yao kwa ufanisi zaidi, wengine wakalala mtoni kuonyesha umahili wao lakini wakashindwa na kuuondoa mkono huo wa ajabu...

Mfalme na wasaidizi wake wakakuna vichwa, wananchi hawana jinsi ya kupata maji. Maji mtoni hayachoteki, wananchi wanaogopa kutumia maji hayo. Ndipo Abunuwasi akajitokeza mbele ya Mfalme. Akamwambia Mfamle, "Mimi naweza kujaribu.

Mfalme akamfukuza Abunuwasi kwa hasira, akamwambia. "Mpumbavu sana wewe, hapa wameshindwa waganga na waganguzi, wewe Abunuwasi utaweza wapi, usitupotezee muda wetu".

Abunuwasi akaondoka, waganga wakazidi kumiminika mtoni wakitoka sehemu mbali mbali za dunia kutokana na sifa zao. Kila walichofanya kuuondoa mkono huo wakachemka na kuondoka eneo hilo kimya kimya.

Abunuwasi akamrudi Mfalme, akamwambia, "Wacha nijaribu mimi". Mfalme akamjia juu akamwambia. "Nimesema huwezi Abunuwasi, wameshindwa waganga wa dunia, utaweza wapi wewe?, Abunuwasi akasisitiza. "Wacha nijaribu mimi kama walivyojaribu wengine na kushindwa.

Mfalme kwa hasira akamwambia Abunuwasi, "Haya jaribu, maana unataka kutupotezea muda tu hapa, lakini ole wako ukishindwa, nitawaamru askari wakutie ndani".

Abunuwasi akaanza kuuzunguka mto huku umati wa wananchi ukimwangalia kwa makini, alipita huku na huku akikimbia kama mtu aliyepatwa na wazimu, Mfalme akaanza kuchukia, hatmaye Abunuwasi akakaa sambamba na mkono ule, Abunuwasi akachuchumaa chini na kuinua mkono wake juu mfano wa mkono ule.

Mfalme na wananchi walikuwa kimya wakifuatilia kwa makini tukio hilo, Abunuwasi aliuchezesha mkono wake kushoto na kulia, mkono ule ndani ya maji nao ukafanya vile, kama alivyofanya Abunuwasi. Wananchi wakashangazwa mno na kitendo kile.

Abunuwasi akauvuta mkono wake nyuma, mkono huo pia ukafanya hivyo, Abunuwasi akakunja kidole chake kimoja, mkono ndani ya maji nao ukafanya vile. Hatmaye Abunuwasi akaushusha mkono wake chini kama anaudhamisha, mkono ule nao ukadhama na haukuonekana tena.

Mayowe, vigelegele na shangwa vikasikika, Mfalme akasimama akamfuata Abunuwasi, akamuomba radhi, akamtukuza na kuonyesha kufurahishwa. "Ahsante sana Abunuwasi, umetuondolea aibu, nisamehe kwa kukudharau, sikutegemea kabisa".

Wananchi wakaja juu wanamtaka Abunuwasi apewe Ufalme. Maana ameweza kufanya jambo lililowashinda waganga na waganguzi. Mfalme akahamaki. Abunuwasi akaula...
 

KARAMU YA ABUNUASI​


Hapo zamani za kale aliondokea Abunuwasi. Abunuwasi huyo aliishi katika mji mmoja wenye watu kidogo. Katika mji huo Abunuwasi alikuwa mtu maarufu sana kwa sababu alikuwa mcheshi, mchangamfu, na mtu wa masihara sana. Alipenda kucheza na kufurahisha watu. Abunuwasi alijulikana na kila mtu. Siku moja Abunuwasi aliota ndoto. Katika ndoto hiyo aliota kuwa babu yake aliefariki miaka mingi amekuja kumpa ujumbe.

Ujumbe huo ulikuwa anamtaka Abunuwasi afanye karamu kubwa. Katika karamu hiyo Abunuwasi alitakiwa achinje ng`ombe mkubwa na kupika wali mwingi. Kisha alitakiwa awatafute vipofu arubaini katika mji ule waje kula chakula hicho. Bahati mbaya yule babu yake hakumwambia Abunuwasi wapi atawapata vipofu hao arubaini. Asubuhi Abunuwasi aliamka na kujiuma kichwa. Alijiuliza maswali mengi kisha akasema;`` Ndoto hii lazima iatakuwa ya kweli. Babu yangu hawezi kuja usingizini akaniambia uongo. Huu ni ukweli. Lazima niifanyie kazi haraka. Sasa nitatafuta mchele na yule ng`ombe wangu mkubwa nitamchinja kwa ajili ya karamu. Sawa!``.

Baada ya hapo Abunuwasi alimaliza. Siku ile Abunuwasi alikwenda madukani kutafuta mchele. Kisha alimchukuwa ng`ombe wake mkubwa na kumuweka tayari kwa ajili ya shughuli. Lakini Abunuwasi alikuwa hajuwi wapi atawapata vipofu arubaini kwa sababu katika mji ule kulikuwa na vipofu wasiozidi watano. Abunuwasi hakukujuwa la kufanya.aliendelea tu na matayarisho ya karamu mpaka alipokamilisha kila kitu.

Siku ya karamu ilipofika Abunuwasi alipita mji mzima na kunadi karamu yake. Alikuwa akisema;Hee! WANANCHI! leo ni leo asie mwana aeleke jiwe. Kutakuwa na karamu ya kukata na mundu nyumbani kwangu leo. Karamu hii ni maalumu kwa watu maalumu. Wahusika wote watapewa kadi za mwaliko. Kila atakaepata kadii ya mwaliko anaombwa kufika mapema bila kuchelewa. Abunuwasi alimaliza. Baada ya kutoa tangazo Abunuwasi alikata vipande vidogo vidogo vya karatasi.

Vipande hivyo vilikuwa ni kwa ajili ya mualiko. Kisha alichukuwa ngozi ya ng`ombe na kuanza kuiburura mitaani. Kila alipopita watu walimshangaa. Wengine walimuuliza Abunuwasi unaburura nini?. Abunuwasi hakujibu kitu ila alikuwa akimpa kadi ya mwaliko kila alieuliza suali hilo. Baada ya muda kupita karamu ilikuwa tayari kuliwa. Abunuwasi nae alimaliza kutowa kadi zake zote.

Wakati wa kula ulipofika,kila aliepewa kadi ya mwaliko alikuwa amehudhuria. Hapo Abunuwasi aliwakaribisha chakula. Watu walianza kula mpaka wakashiba.Walipomaliza kula Abunuwasi aliwashukuru sana na aliwambia;``Nawashukuru sana nyote mliohudhuria katika karamu hii. Kwani kabla a hapo nilikuwa sijui la kufanya. Nilitakiwa nifanye karamu hii na kuwaalika vipofu wa mji huu waje kula.Kama mnavyojuwa ndugu zangu mji huu hauna vipofu wengi au pengine wapo lakini hatuwajui.

Sasa mimi niliposhindwa nilipita na hii ngozi.Sasa ninafahamu kuwa kila mtu anajuwa kuwa hii ni ngozi au sio?[ICODE].Watu waliitikia kwa pamoja Hiyo ni ngozi. Abunuwasi aliendelea;Sasa nilipoanza kuburura ngozi hii kuna watu waluniuliza; Hiyo nini Abunuwasi?[/ICODE].Mimi sikuwajibu sababu nilijuwa hao walikuwa hawaoni hivyo niliamuwa kuwaalika kama nilivyoelekezwa na babu yangu. Watu wote walishangaa
 
Abunuasi na hukumu ya kijana.

Hapo zamani za kale katika nchi moja Afrika, paliishi mama mmoja ambaye alikuwa mjane. Muda mfupi tu kabla ya mumewe kufariki walijaliwa mtoto mmoja wa kiume ambaye huyo mama alimlea kwa shida na taabu nyingi. Hata hivyo mama na mtoto wake walipendana ipasavyo. Hapo katika kijiji chao kulikuwa pia na tajiri mmoja ambaye alikuwa bahili na katili kweli. Yule kijana maskini alikwenda kwa tajiri kuomba kazi. Tajiri alimwambia kwamba alikuwa na kazi kwake na angemlipa vizuri sana.
Kijana alifurahi kusikia hivyo na akamwuliza tajiri kwa furaha.

"Kazi gani hiyo utanipa mheshimiwa? Mimi nitaifanya vizuri mpaka hata wewe utafurahia." Tajiri akamwambia, "Ukilala katika maji baridi sana usiku mzima, nitakupa shillingi laki moja." Ulikuwa wakati wa baridi sana kwamba maji ya ziwa karibu yagandamane kuwa theluji kwa baridi.

Lo! Kijana hakufikiria angeweza kuwa na pesa nyingi hivyo katika maisha yake. Tamaa ya kutaka kumsaidia mama yake ambaye wakati huo alikuwa mgonjwa na mzee, ilikuwa kubwa sana kwa hivyo akakubali bila kufikiria. Mama aliposikia habari hizo karibu azimie kwa wasiwasi na huzuni.

"Mwanangu sitaki uhatarishe maisha yako kwa sababu ya pesa. Mungu yuko nasi na hajatuacha hata siku moja tukalala njaa. Atazidi kufanya hivyo hivyo. Je, ukifa nitabaki na nani mwanangu? Mimi mzee sasa wala sijiwezi!" Kijana alimjibu,

"Mama usiwe na wasiwasi wala woga wo wote! Nitaweza kabisa kulala kwenye maji baridi mpaka asubuhi na siwezi kufa" Mama bado alizidi kubisha, lakini kijana alisisitiza kabisa kwamba lazima afanye hiyo kazi ambayo itawaondolea shida zote za kifedha, kama alivyoona yeye.

Kwa huruma ya mama na wasiwasi juu ya mtoto wake, alikwenda karibu na ziwa pale alimotumbukizwa mtoto wake kwenye maji baridi kama barafu, Alimwona kichwa tu kimelea juu ya maji. Mama aliwasha moto mkubwa karibu na ziwa lile kwenye ufa, ili aweze kumwangazia angalao mwangaza na kumwona. Usiku kucha mama mtu hakufunguka jicho hata dakika moja. Alimlilia Mungu amtunze mwanae asife kwa baridi.

Kwa huruma ya Mwenyezi Mungu, kijana alistahimili baridi yote ile mpaka alfajiri siku ya pili.

Alikwenda kwa tajiri kupokea malipo yake lakini tajiri akamwambia. "Hupati hata ndururu ng'o!"

"Kijana alishangaa akamwuliza, "Kwa nini mheshimiwa? Uliniahidi kunipa shillingi laki moja nikilala katika maji yabaridi usiku mzima. Usiku mzima nilikuwa ndani ya maji hayo na shahidi wako wameshuhudia na pia mama yangu."

"Ehe, hapo sasa umenena. Mamako aliyekuwashia moto ili upate joto usiku mzima. Hayo ndiyo yalikuwa maagano yetu? Sikumbuki tukiagana kwamba mama yako atakuja na kuwasha moto mkubwa wa kukupa joto kisha unidanganye umelala kwenye maji ya baridi. Unaniona mimi bwege sio? Nenda zako, sikulipi cho chote."

Kijana alikasirika kweli na akamweleza jirani yake mzee Abunuasi. Kama kuna watu Abunuasi aliowazira, ni matajiri waliopenda kuwaangamiza maskini badala ya kuwasaidia. Abunuasi akamwambia kijana asiwe na wasiwasi kwamba rafiki yake Sultan atamsaidia. Akamwambia aende kwake na kumweleza habari zote. Kijana alifuata ushauri wa Abunuasi, lakini Sultani aliposikia kisa chote kutoka pande zote mbili aliamua kwamba kijana asipate malipo kamwe. Abunuasi alishangaa na uamuzi huo wa Sultani mzima wa nchi akamwambia kijana bado asiwe na wasiwasi atapata hela zake. Kijana alimwahidi Abunuasi kumpa shillingi elfu ishirini akimsaidia.

Abunuasi aliandaa karamu kubwa na akawaalika watu wengi pamoja na Sultani na yule tajiri pia. Alichinja mbuzi akatayarisha vitu vyote, mchele, mboga zikakatwakatwa na kuwekwa kando. Moto mkubwa uliwahswa na kila kitu kikawekwa kando ya moto, nyama ya mbuzi katika sufuria pamoja na vitunguu na viungo.

Mboga, mchele, zote zikawekwa kando ya moto na Abunuasi akaenda kuwakaribisha wageni wake. Wageni walingojea chakula siku kutwa hawakuona hata maji ya kunywa. Abunuasi aliwaambia kwamba chakula bado kinapikwa jikoni na wala hakijawa tayari. Itabidi wangojee. Mwisho walikasirika na kuingia wote katika jiko. Walikuta moto unawaka vizuri na kando ya huo moto chakula chote walichokuwa wakikingojea kiko kando ya moto huo mkubwa. Sultani akiwa mmoja wa wale waliokuwa na njaa alisema.

"Abunuasi wewe akili zako zinafanya kazi? Hiki chakula ulisema kinapikwa? Mbona moto uko kando na chakula kando? Hakitaiva hata baada ya miaka elfu. Wewe mwehu kweli kama watu wanavyokusema. Unatulisha njaa siku nzima?"

"Usiwe na wasiwasi Sultan, chakula kitaiva tu! Subira huvuta kheri mheshimiwa."

"Acha upuzi na ubwege. Hiki chakula hakitaiva kamwe. Hakipati hata joto la moto huo hata kama mkali kiasi gani"

"Kwa nini kisiive mheshimiwa? Wewe uliamua kesi ya kijana maskini asilipwe na huyu tajiri nduli alipomlazimisha kulala kwenye maji baridi usiku mzima. Kwa njaa na umaskini wake, alikubali. Naye mama yake kwa upendo wa mwanae, alilala kando ya ziwa akimumlikia mwanae ili apate kumwona tu kama angali hai. Wewe uliamua asilipwe kwa sababu ya huo mwangaza aliyemlikiwa na mamake. Basi na hiki chakula kutokana na uamuzi wako lazima kiive hivyo hivyo moto ukiwa kando." Sultani aliona aibu kweli mbele ya watu hao wote, na akaamuru tajiri amlipe kijana pesa zake mara moja na Sultani akampa Abunuasi zawadi kubwa kwa sababu ya ubusara wake. Baada ya hayo yote kukamilika, chakula kiliwekwa juu ya moto, kikaiva na wote wakala.

Wote walimshukuru Abunuasi sana!
 

HADITHI: Abunuwasi na Kisa cha Mbuzi

Kuna wakati, Abunuwasi aliamua kuwa mfuga mbuzi. Alinunua mbuzi wa kufuga huku akiwa na lengo la kujiongezea kipato chake pindi mbuzi huyo atapoanza kuzaa, ili awafuge ndama wawe wengi na kumuwezesha kuwa tajiri kuliko wote waliokuwepo katika mji ule..
Siku moja Abunuwasi akipokuwa anampeleka mbuzi wake malishoni, alikuta kiatu kimoja kizuri sana katikati ya njia.

Alisimama na kukiangalia. Kiatu kilipendeza machoni mwake ila akasema “kiatu hiki ni kizuri lakini mbona kipo kimoja tu?” Alitafuta kiatu cha pili pembezoni mwa njia ila hakukiona. Alipoona hawezi kuvaa kiatu kimoja, aliamua kukiacha palepale.

Abunuasi akachukuwa mbuzi wake na mbele kidogo akaona kile kiatu cha mguu wa pili. Abunuwas alishangaa na akaona bora angelikichukua kile cha mwanzo kwa sababu cha pili kimepatikana.

Aliporudi pale mwanzo kukitafuta alichokiacha awali lakini hakukikuta tena, alijaribu kukitafuta lakini hakukiona. Basi akadhani kuna mtu amekiokota. Akarudi haraka alipomfunga mbuzi wake nako pia hakumkuta mbuzi wala kile kiatu kimoja. Mwisho akawa amemkosa mbuzi na viatu, Ndoto zote za Abunuwasi kupata utajiri zikaruka na akabaki na umasikini wake kwa sababu ya tamaa yake.
 
ABUNUWASI NA MALAIKA

Abunuasi Aliwaambia Watu Ya Kuwa Kila Siku Anatembelewa Na Malaika Na Taarifa Hizo Zikaenea
Zikamfikia Mfalme, Mfalme Akamuita Na Kumuuliza Na Abunuasi Akakubali Mfalme Akamwambia Ataenda Kwa Abunuasi Kumuona
Malaika Na Endapo Anamdanganya Anamtia Gerezani, Basi Mfalme Akaenda Mpaka Nyumbani Kwa Abunuasi Na Abunuasi Akampa Masharti Mbele Za Watu "mfalme Usijali Utamuona Malaika Ila Kuna Masharti Ya Kumuona Kama Wewe Ni Mtoto Haramu Huwezi Kumuona Kabisa Na Pia Ukiingia Lazima Uweke Dhahabu Mlangoni" Mfalme Akakubali Na Abunuasi Akaingia Ndani Akachukua Kiti Chini
Ya Kiti Akaweka Viatu Na Juu Kofia Na Akatandika Vazi Zuri Yani Kama Mtu Amekaa Halafu AkamkaribishaMfalme, Mfalme Alipoingia Hakumuona Malaika Ila Alishindwa Kusema Hajamuona Aliogopa Kuonekana Yeye Ni Mtoto Haramu Hivyo Akatoka Mle Ndani Na Kusema Amemuona Malaika Na Abunuasi Akawa Amepata Dhahabu Kiulaini.
 
Abunuasi Aliingia Kwa Kinyozi Na Mtoto, Akasema Anyolewe Nywele Na Ndevu Alipomaliza Akasema Na Mtoto Naye Anyolewe,
Wakati Mtoto Ananyolewa Yeye Akaaga Anaenda Kumnunulia Mtoto Juisi, Masaa 3 Yakapita Bila Abunuasi Kutokea Kinyozi Akamwambia Dogo "Vipi Baba Ako Amekusahau?" Mtoto"Yule Sio Baba Angu Alinikuta Njiani Akaniambia Tuingie Hapa Tunyolewe Bure."
 
ABUNUWASI NA PUNDA

Abunuasi Alinunua Punda Ila Hakuwa Na Sufuria Kubwa La Kumnyweshea Maji Ikabidi Aende Kuazima Kwa Jirani Na Akapewa Baada Ya Siku 3 Akalirudisha Kwa Mwenyewe Huku Akiwa Ameweka Sufuria Nyingine Ndogo Ndani Yake, Abunuasi Akamwambia Yule Jirani Wakati Anaichukua Ile Sufuria Ilikuwa Na Mimba Kwahiyo Imezaa Yule Jirani Akashangaa Na Kufurahi Kusikia Sufuria Imezaa, Siku Nyingine Abunuasi Akaenda Kuazima Yule Jirani Akampa Akijua Itarudi Imezaa Lakini Siku Nyingi Zikapita Bila Sufuria Kurudishwa Ndipo Alipoamua Kumfata Abunuasi Akamwambia "Samahani Jirani Ile Sufuria Imefariki Wakati Inajifungua." Jirani "Haiwezekani Sufuria Haiwezi Kufa." Abunuasi "Kila Kinachozaa Pia Hufa." Yule Jirani Alirudi Kwake Bila Sufuria..
 
ABUNUWASI NA NYUMBA YA MAJARIBIO

Abunuasi alijenge nyumba
Lakini Kila mtu akipita anamwambia
Huu mlango ungekaa pale hii nyumba ingependeza
Abunuasi baada kuona nyumba yake Imejaa viraka akaamua
Kujenga nyumba nyingine hii pia jamaa wakaanza kutoa ushauri tena Abunuasi akasema nyumba ya marekebisho ile pale
 
Back
Top Bottom