SoC02 Hekima ya mchungaji

SoC02 Hekima ya mchungaji

Stories of Change - 2022 Competition

Rupia Marko D

Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
39
Reaction score
63
Palitokea mtu mmoja afahamikaye kwa jina la Marco Marcusio, kijana huyu mwenye asili ya kinyamwezi akiwa ni chotara wa kimakabila Babaye mnyamwezi mama yake mnyakyusa, kijana huyu alizaliwa Tabora liliko chimbuko la kabila la Baba yake. Na kwa kuwa Baba yake alipata kisomo cha juu kabisa na kufanikiwa kuajiriwa kama Afisa elimu katika mkoa wa Simiyu.

Basi Baba yake Marco aliyekua akifahamika kwa jina la Marcusio aliichukua familia yake ndogo hiyo na kuhamia Simiyu. Kama tujuavyo ukanda ule wa Simiyu wasifika zaidi kwa ufugaji, hivyo Marco akiwa bado ni Kijana mdogo tu alikimbia shule licha ya kuwa alikua na uwezo mkubwa darasani.

Basi jioni mmoja Marcusio ( baba yake Marco) akamwita Marco na kumhoji kwa nini hataki Shule?

Marco akajibu:- najua kwa hakika ya kuwa Elimu ni ufunguo wa Maisha, lakini mimi nilipo fikia hapa tayari nimefunguliwa maisha!

Baba yake akang'aka na kumwambia- umefunguliwa maisha? Kwa maisha yapi uliyonayo, kwa kipi umilikicho.

Marco : Baba nimejifunza basics (vitu msingi) kwangu mimi vyatosha kuwa muongozo tu, sasa najua kusoma, naweza mahesabu, jiografia pia naijua, yaani najua wapi ni kusi na wapi ni kaskazi, na elimu ya viumbe pia naifaham.

Baba : mwanangu unapotoka na dhairi unataka uipitie njia ya upotovu. Je haukuisoma ile hadithi ya mwana mpotevu?

Marco- niliisoma nakuelewa jinsi yule mwana mdogo alivoitapanya mali ya Babaye. Na badae kurudia na kutubu.

Babaye akamwambia sasa mbona wataka kuifuta njia hiyo mwanangu mpendwa hujui nawe utalitenda kosa hilo.

Marco- hapana baba, mi nikuombe jambo moja (huku akiinama chini)
Baba - jambo gani mwanangu (huku akimwangalia kwa shauku ya kujua ni jambo gani).

Marco- naomba unipe katika kundi la kondoo wako wanakondoo wawili jike na dume, kwa kua nimeamua kuwa mchungaji kwa uchungaji huu ntasafiri nakuijua dunia vizuri.
Basi baba yake Marco akampa kondoo wawili kama vile alivyotaka na hapo Marco akaingia ndani na kutoka na nguo chache tu, akibeba birika la maji na kiliba cha kuwekea Chakula.

MAISHA YA UCHUNGAJI
Basi Marco akaanza kuchunga kondoo zake, huku akitembea katikanyika na mbuga kubwa kubwa kwa lengo la kutafuta malisho na maji. Na ndani ya miaka miwili kundi la kondoo wake likaanza kupanuka na kuwa kubwa.

Yalikua yakifika majira ya kiangazi ilkuwa inambidi Marco kuwakwangua na kuwatolea Manyoya kondooo wake ili kupata sufu za kuuza. Na sufu hizi Marco alikuwa akiziuza kwa wafanyabiashara wa sufu wakubwa, pia kwa wale matajiri waliokuwa wakimiliki viwanda vya kutengenezea nguo.

UCHUNGAJI WAMSAIDIA KUIJUA NCHI KIUNDANI
Kwa kuwa majira na nyakati zilikuwa zikibadilika, kwani kulikua na kipindi ambapo sehemu moja inasitawi na sehemu nyingine kuzolota. Hii ilimbidi Marco kutembea sehemu mbalimbali na hivyo alifanikiwa kukutana na watu wa kila kabila Wafipa kwa wasafwa, wachaga kwa warangi, wairaq kwa wanyaturu.

Hivyo uchungaji ukamsaidia kuweza kuijua vema nchi yake ya Tanzania pia kuwajua watu wake pamoja na sifa zake.

Na Marco alipokuwa Malisho daima kondoo wake walikua wakiisikia sauti yake yeye na wala hawakuchanganywa na miruzi ya wachungaji wengine, hii ni sababu Marco aliwapenda na kuwajari kondooo wake, alijitoa kwa ajili yao pia alikuwa hodari katika kuchagua ni sehemu ipi ambako malisho bora hupatikana.

Na vichwani mwa kondoo kitu na jambo msingi ilikua ni chakula na maji tu, hawakujua habari ya maeneo na utofauti wa sehemu kwao ni ubora wa malisho tu, kwani walipolishwa jana kwao ni sawa wanapolishwa leo.

AKUTANA NA MWANAMKE WA NDOTO YAKE.
Basi ilipofika kipindi cha kiangazi kama kawaida yake Marco aliliongoza kundi lake hadi katika mji mmoja uitwao Mtakuja, huko akaelekea katika duka la mfanyabiashara wa sufu, alipofika na kubisha, kijakazi akamwambia kwa sasa boss yupo na mkutano na wafanyabiashara wenzake hivyo amsubirie kidogo.

Marco akakubali, wakati ameketi kumsubiri akapita Binti mzuri Mashallah kaumbwa kaumbika, mwanaume lijali akimuona lazima adondoke kwake, waimbaji mashuhuri wakimuona lazima wamtungie Mashairi ya kuusifu uzuri wake, kwa picha tu akitembea mwendo wake kama wa twiga mvivu atembeaye kwa maringo, akiongea sauti yake kama wimbo wa kubembelezea watoto wakati wa usiku, kiuno chake kama cha nyigu kikiufanya mwili wake utengeneze umbo namba nane,tuishie hapa.

Yule Binti alikuwa akiitwa Juliet basi wakati anatembea ilimanusura adondoke ndipo Marco alipomuwahi na kumuokoa na hapo ndipo ulipo kuwa mwanzo wa kufamiana kwao, wakaongea maswala mengi takribani masaa mawili.

Stori zao zilikatishwa kwa ujio wa Baba yake Julliet, alipokuja wakaelewana na Marco kiasi gani cha Sufu alikua akikihitaji. Basi Marco akawatoa Kondoo zake manyoya walipomaliza wakaagana, japo Marco alizamilia kurudi katika kijiji cha Mtakuja kwani tayari alikua amezama katika uzuri wa Julliet.

UKARIMU WAMTUNZA
Basi ulipita Mwaka mmoja toka atoke katika kijiji cha Mtakuja na sasa yalikua yamefika majira ya kiangazi hivyo kwa sasa Marco alikua na shauku kubwa sana ya kufika katika kijiji cha Mtakuja, hii ilikuwa si kwa sababu ya biashara ya Sufu pekee bali na kueleza nia yake ya kumuoa Juliet.

Basi wakati wa safari akaweka hema la kupumzikia katika kijiji cha Ukombozi, pindi anapumzika akapita kikongwe. Marco alimsalimia Babu yule na kumwalika japo apumzike katika hema lake, hapo kikongwe yule alipoingia mazungumzo yao yalikua hivi.

Marco: Shikamoo Babu, na pole kwa safari, ningependa kujua unaitwa l nani!
Kikongwe: Mimi naitwa Yeroboam, nikitokea katika falme iliyositirika, sina Baba wala mama.

Basi Marco akamchinjia mwanakondoo nao wakamla usiku ule, na asubuh ilipofika yule kikongwe aliyejitambulisha kwa jina la Yeroboam akamwambia Marco, kwa sababu ya ukarimu wako ishike njia hiyo iendayo Kijiji cha Mtakuja huko utakuta zawadi yako tayari nimeindaa. Wakaagana Marco akielekea Mtakuja na yule kikongwe akishika njia yake walipoachana tu takribani hatua mbili tu Marco akageuka amuone kikongwe yule na wala asimuone. Marco alishitushwa sana na kutoweka kwa kikongwe yule basi akaelekea mwelekeo alioelekezwa na alipofika alishangaa alichokiona. Lilikua ni jiwe la dhahabu. Na alipowasili kijijini Mtakuja kisha kuuza Sufu yake akaeleza wazi nia yake ya kumuoa Juliet.

KUPOKELEWA KWA SHANGWE NYUMBANI
Na sasa ilimbidi arudi nyumbani, sasa akiwa na kundi kubwa la kondoo pamoja na jiwe la dhahabu akiwa na Julliet, alipofika nyumbani baba yake Marcusio alifurah na kumfanyia sherehe kubwa na sasa mahali ikaandaliwa na kupelekwa kijijini Mtakuja na kisha Marco akafunga ndoa na Julliet. Sasa akawa amestawi amestawika naye akaishi kwa raha msatarehe.

Ni mimi Marko Rupia.
 
Upvote 14
I like falsafa ulizo nazo juu ya utunzi naami I Kuna wakati tutaona vitabu vyako pia keep hard my bro
 
Kazi nzuri inajengwa na vijana bora wenye mtazamo chanya
Endelea kupambana kaka sisi tupo na wewe
 
Back
Top Bottom