Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
Na Elius Ndabila
0768239284
Zitto Kabwe ni moja ya vijana waliojizolea sana umaarufu kwenye siasa za 2005-2015.Alikukuwa ni kijana alikuwa anajenga hoja. Uzito wa hoja zake ulimpa mashabiki wengi na kujipatia umaarufu mkubwa. Ninamzungumzia Zitto yule si huyu mlopokaji, mubwatukaji na mzushi. Ninamzungumzia Zitto SMART aliyeshawishi vijana wengi kuipenda siasa hasa za hoja na si vihoja.
Jana nilipoona habari za Prof Assad zikienea kuwa katekwa nilishituka sana. Lakini baadae nilijiuliza maswali mengi, kwa nini habari za Prof Assad anayetoa ni Zitto? Twitter, Instagram, fb na jf alikuwa analipoti Zitto tu. Nilijaribu kuuliza kwa nini Zitto amekuwa front sana kutoa habari za Prof Assad? Nilijibiwa kuwa ni family friend. Nikasema basi sawa kwa kuwa hata yeye kwenye thread yake alisema ameongea na familia yake.
Baada ya muda mfupi Zitto alitwitte kuwa Prof Assad yupo salama na si muda mrefu tutawajuza kinachoendelea. Nilirudi tena kwenye group la whatsapp nikauliza ZITTO anatuachia maswali zaidi. Niliuliza Zitto ameongea na watekaji na wakamwambia Assad yuko salama au ameongea na Prof Assad? Kama ameongea na watekaji amepata wapi namba za watekaji? Nilisema issue hii ni kama ya kutengeneza na Kabwe anaweza kuwa program manager. Niliandika hivyo kutokana na mtiririko wa maandiko yake kwenye mitandao.
Baada ya muda mfupi usiku niliona Twitter ya Prof Assad ikikanusha kuwa yeye yupo na hajatekwa bali yupo na familia yake. Ujumbe huu ulijibu maswali yangu ya aya hii hapa juu kuwa Zitto ni mchochezi, mnafiki na mwingi. Lakini nilijiuliza kwa nini ameandika hivi na kuzua taharuki? Sikupata majibu.
Rai yangu ni kuliomba jeshi la polisi kumkamata Zitto na asaidie kutoa maelezo kuwa alipata wapi uhalali wa kumzushia Prof Assad? Je Zitto alikuwa anafanya mpango wa kumteka Assad ili aisingizie serikali na kukwama au? Ninadhani vyombo vya usalama vinaweza kuanzia hapa. Amefanya kosa kubwa kwa mjibu wa sheria za kimtandao.