HEKO: Coca wameongeza ubora, Pepsi wamepunguza bei!

HEKO: Coca wameongeza ubora, Pepsi wamepunguza bei!

Usedcountrynewpipo

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,636
Reaction score
2,728
Napenda kuyapongeza makampuni makubwa ya vinywaji hapa nchini, kila moja kwa kuchukua hatua mbali mbali yenye manufaa kwa walaji (Wanywaji).
Kwa wale wapenzi wa soda, mtakuwa mmenotice kuwa ladha ya soda ya koka imeboreshwa kuliko kipindi cha nyuma, kitu kinachowafanya watu ambao tulikuwa hatupendi soda zao kuzipenda like never before.
Pia mtagundua kuwa kampuni ya Pepsi imepunguza bei ya vinywaji vyao kitu ambacho kimewafanya walaji (wanywaji) kuweza kumudu na hivyo kununua kwa wingi bidhaa zao. Leo nimetoka dukani kuulizia soda za Pepsi mwenye duka kaniambiza soda ziko kwishney ati watu wanazinunua sana.
Cha muhimu ni serikali kupunguza maushuru kwenye vinywaji baridi visivyo na kilevi ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kumudu bidhaa hizi.
 
Wapi huko zimeshuka bei maana Pepsi zipo all over the world
 
Naona Meneja Masoko kwenye majukumu yako, kwanza thibitisha ubora wa coca kabla hujakandia Pepsi!
 
Naona Meneja Masoko kwenye majukumu yako, kwanza thibitisha ubora wa coca kabla hujakandia Pepsi!

Sijakandia Pepsi. Nimewasifu kila kampuni kwa maamuzi waliyofanya. Nimewasifu Pepsi kwa kupunguza bei na pia nimewasifu koka kwa kuboresha soda yao...
 
Pepsi wamepunguza bei sababu na size ya chupa imekuja ndogo zaidi, ila sio mbaya!
 
Kwani Pepsi zilikuwa zinauzwa tsh ngapi wakuu?
 
Sijakandia Pepsi. Nimewasifu kila kampuni kwa maamuzi waliyofanya. Nimewasifu Pepsi kwa kupunguza bei na pia nimewasifu koka kwa kuboresha soda yao...
Hiyo Coca awali ilikuwaje na sasa ikoje? na hao coca wameboresha lini soda yao baada ya Pepsi kushusha bei?
 
Coca-Cola nao wameshusha ila hazijaingia Sokoni.
 
Back
Top Bottom