Nikiwa kama mteja napenda kuipongeza Benki ya CRDB kwa kuazimisha kwa mafanikio wiki ya huduma kwa wateja. Pamoja na kuwa na mambo mengi lakini suala la kutukaribisha kwenye matawi kwa bashasha, kuchukua maoni yetu, kupata muda wa kukutana na viongozi wa juu (mimi nilikutana na Dr.Kimei pale Lumumba) . Ni vitu vidogo lakini vyenye maana kubwa kwetu kuonyesha kuwa wanatujali. Juu la hilo nimefurahishwa pia kuona kupitia vyombo vya habari kuwa katika wiki hii, Benki ilitoa misaada mbalimbali kwa jamii ikiwemo madawa ya Kipindupindu na madawati kwa shule za msingi. Kwa hili nawapa 5 ya 5.
Hongereni sana CRDB.