Heko CRDB Bank kwa Wiki ya Huduma kwa Wateja

Heko CRDB Bank kwa Wiki ya Huduma kwa Wateja

Hakeem makamba

Senior Member
Joined
Apr 15, 2011
Posts
123
Reaction score
41
Nikiwa kama mteja napenda kuipongeza Benki ya CRDB kwa kuazimisha kwa mafanikio wiki ya huduma kwa wateja. Pamoja na kuwa na mambo mengi lakini suala la kutukaribisha kwenye matawi kwa bashasha, kuchukua maoni yetu, kupata muda wa kukutana na viongozi wa juu (mimi nilikutana na Dr.Kimei pale Lumumba) . Ni vitu vidogo lakini vyenye maana kubwa kwetu kuonyesha kuwa wanatujali. Juu la hilo nimefurahishwa pia kuona kupitia vyombo vya habari kuwa katika wiki hii, Benki ilitoa misaada mbalimbali kwa jamii ikiwemo madawa ya Kipindupindu na madawati kwa shule za msingi. Kwa hili nawapa 5 ya 5.
Hongereni sana CRDB.
 
Wateja gani hao unao wazungumzia mkuu..?
maana mie niliowaona ni vibopa na wanene watupu...
sijaona mama ntilie au fundi masufuria akikutana na hao viongozi wa hiyo benki.
Kwanza watu wanaoenda kukutana nao wanapewa mialiko na kadi juu.
Fatilia waliokuwepo pale wote ni ngozi zinzong"aa tuu (kutokana na upepo wa AC).
 
Mimi ni mteja wa tawi la Lumumba na nilikuwepo tawini na nikalishwa keki na Dr.Kimei, Alhamisi tarehe 8/10/2015 mida ya mchana. Si mimi tu bali pamoja na wateja wengi tuliokuwa kwenye foleni. Sijui definition yako ya vibopa, lakini kila aliyekuwa tawini alipata wa saa wa kuongea nae na kula keki.
 
Back
Top Bottom