Mwandishi wa Tanzania Daima angeeleweka na HEKO zake kama angechambua Usalama wa Taifa kwa miaka yote 40.
Katika intaneti kuna masuala ya Usalama wa Taifa, kushindana na majasusi wa Kireno toka Mozambique, majasusi Weupe wa Rhodesia(Zimbabwe), makaburu (South Africa) n.k n.k ndio maana hata leo hicho kituo cha polisi salender bridge DSM ni kutokana na usalama wa Tanzania kutishiwa na makomandoo majasusi kutaka kulilipua daraja kuiadhiri kisakolojia Tanzania.
Kina Samora Mache, Nujoma, Savimbi, Kabila, Chissano, Che Guevara n.k waliishii Tanzania kwa kutegemea ulinzi wa Usalama wa Taifa, inagawaje mara moja moja kulitokea changamoto kama la Eduardo Mondlane raisi wa kwanza wa Frelimo kuletewa kifurushi cha bomu DSM na kikamlipukia na kuchukua uhai wake.
Pia huko kusini mwa Tanzania, helikopta za mreno zilikuwa zinatua na kuleta kashikashi.
Mbali ya hilo 'vetting' wa viongozi wa umma Tanzania ilikuwa inafanywa kwa uzalendo wa hali ya juu, wazee wetu kabla ya kupewa uongozi sisi watoto barabarani tulikuwa tunaona 'vijana' tusiowajua wakifuatilia mienendo ya wazee wetu vigogo kwa kushinda mtaani na 'gari bovu' geresha ya kusubiri mafundi, mzee akitoka na gari mara 'gari bovu' limepona linawafuata wazee wa umma mienendo yao.
Hivyo kama Usalama wa Taifa bado wanafanya hivyo kwa staili mpya ya 'sayansi na technolojia' basi HEKO, lakini siamini hilo maana mafisadi kibao sana sasa.
Juzi juzi yule mjamaica aliyeleta kasheshe alikatiza toka kusini mwa Tanzania mpaka Tanga na kuingia Kenya, bila Usalama kushugulikia huko kusini mwa Tanzania, labda ndio changamoto hizo.
Hivyo kichwa cha habari kingekuwa 'Usalama wa Taifa wanakabiliwa na Changamoto kubwa''