Heko Zanzibar kwa kuwa na dira ya ukombozi wakati sisi tukitapa tapa gizani

Heko Zanzibar kwa kuwa na dira ya ukombozi wakati sisi tukitapa tapa gizani

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Walisema waungwana ukiona vyaelea vimeundwa.

Siyo siri wenzetu Zenji wako vizuri na katika njia yao salama ya ukombozi iliyo wazi:

"Zanzibar wanataka mamlaka yao kamili na wamejipanga kwa ajili ya hilo."

Kwenye mapambano yao wanapigana bega kwa bega na bila ya tashwishi.

Sisi hatukujifunza JKNIA wala Kiluvya? Kwani wabara wale walifikaje huko pamoja na vitisho vyote vya Sirro, mwendazake na yale magenge yao ya wasiojulikana?

Tunapopapasa gizani, ni vyema kurudi nyuma kupatambua kwa usahihi ni wapi tulipokwamia.

Walisema waungwana kuteleza si kuanguka.

Jussa.PNG
 
Wanatikisa tu kibiriti hao ili waongezewe mgao unao tokana na kodi za Watanganyika. Uwezo wa kujitegemea na kuwa Taifa kamili, hawana. Siku zote wanaishi kama kupe tu wa Taifa la Tanganyika.

Kama uwezo wa kufanya hivyo wanao, kitu gani kinawachelewesha? Si waanze mchakato mapema! Imagine Ma Rais wa pande zote mbili ni Wazanzibari wenzao! Si watimize sasa hilo hitaji la mioyo yao?

Binafsi nitafurahi sana siku Tanganyika ikiwa ni nchi isiyo wajibika kuilea, kuitunza na kuilinda nchi nyingine.
 
Hayo mamlaka kamili wanayapataje?

Kama ni kule kuingizwa kwenye serikali ya mseto ambayo wakitoa maoni yao Rais anawapinga, wanachoambulia ni viyoyozi vya kwenye v8 mimi nawaona bado wako mbali sana.

Mamlaka kamili watayapata wakiwa huru kifikra, wawe na wafuasi wa kutosha kuwaunga mkono ili mawazo yao yafanyiwe kazi kivitendo, na pawepo na uwanja sawa wa kufanya siasa.

Lakini sio kufichwa kwenye kivuli cha CCM halafu waseme wako kwenye safari ya kutafuta mamlaka kamili wakati wakijaribu kufungua mdomo tu, wanafungwa, bora waseme wanafurahia tu uwepo wa serikalini.
 
Wazanzibari wako vizuri labda kuliko hata sisi. Zaidi sana ni wamoja. Hao ni hawa hapa katika ubora wao:

Wanataka mamlaka kamili si kwa maana finyu kama unazoziongelea au hata tunazoziongelea huku bila ya kuwa na ufahamu wa kutosha. Ndiyo maana tukidhani wao wanalamba asali na kuwa eti hizi tozo tunazozilalamikia wao haziwahusu.

Nimewasikiliza hawa ndugu na kuwaelewa. Kwa hakika tunayo mengi ya kujifunza kutoka kwao zaidi ya kula ulojo. Elimu haina mwisho.

Bwana Zawadini ni mmoja wa miamba ya mashariki. Heshima kwako mkuu na Aluta Continua!

IMG_20220826_094511_270.jpg

Suala la Tozo limekaaje Kwa Bara na Zanzibar?
 
Kama uwezo wa kufanya hivyo wanao, kitu gani kinawachelewesha? Si waanze mchakato mapema! Imagine Ma Rais wa pande zote mbili ni Wazanzibari wenzao! Si watimize sasa hilo hitaji la mioyo yao?

Binafsi nitafurahi sana siku Tanganyika ikiwa ni nchi isiyo wajibika kuilea, kuitunza na kuilinda nchi nyingine.

Kibiriti kutikisika si ni sehemu ya harakati mkuu? Kwani sisi tunakohitaji Tanganyika yenye mamlaka kamili kiko wapi kinachotikisika?

"Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni."

Kina Jussa ni wapambanaji mahiri waliodhamiria kuikomboa Zanzibar.

Muhimu kututambua - Zanzibar si Tanganyika.

Na huo ndiyo ulio ukweli.
 
Mimi nawaombea hayo mapambano yao yafanikiwe. Natamani kuona wakijitegemea kama nchi kwa 100%, badala ya ilivyo hivi sasa.
 
Mimi nawaombea hayo mapambano yao yafanikiwe. Natamani kuona wakijitegemea kama nchi kwa 100%, badala ya ilivyo hivi sasa.

Sala zako ni za kheri. Bila shaka na wao wanatuombea hivyo hivyo ili nasi tujitegemee kama nchi.

Swali la msingi: "Kwenye utashi wetu nasi wa kujitegemea kama nchi, juhudi zetu wewe waona zinatosha?"

Si kuwa sisi tuko kama wakazi wa DRC hatutaki shida? Tunawategea Zenji wakomae peke yao ili nasi humo humo tupate vya kupata?

Kwani furaha yako ya kuwa Tanganyika huru ni ipiganiwe na wengine tu ili wewe uipate bila maumivu?

Hii si ndiyo ile janja ya nyani kula mahindi mabichi sasa? Kumbe kwa kumfanya mjinga nani?

Wanasema, hebu tuwe objective japo kidogo wandugu?
 
Back
Top Bottom