Hayo mamlaka kamili wanayapataje?
Kama ni kule kuingizwa kwenye serikali ya mseto ambayo wakitoa maoni yao Rais anawapinga, wanachoambulia ni viyoyozi vya kwenye v8 mimi nawaona bado wako mbali sana.
Mamlaka kamili watayapata wakiwa huru kifikra, wawe na wafuasi wa kutosha kuwaunga mkono ili mawazo yao yafanyiwe kazi kivitendo, na pawepo na uwanja sawa wa kufanya siasa.
Lakini sio kufichwa kwenye kivuli cha CCM halafu waseme wako kwenye safari ya kutafuta mamlaka kamili wakati wakijaribu kufungua mdomo tu, wanafungwa, bora waseme wanafurahia tu uwepo wa serikalini.
Kama uwezo wa kufanya hivyo wanao, kitu gani kinawachelewesha? Si waanze mchakato mapema! Imagine Ma Rais wa pande zote mbili ni Wazanzibari wenzao! Si watimize sasa hilo hitaji la mioyo yao?
Binafsi nitafurahi sana siku Tanganyika ikiwa ni nchi isiyo wajibika kuilea, kuitunza na kuilinda nchi nyingine.
Mimi nawaombea hayo mapambano yao yafanikiwe. Natamani kuona wakijitegemea kama nchi kwa 100%, badala ya ilivyo hivi sasa.Kibiriti kutikisika si ni sehemu ya harakati mkuu? Kwani sisi tunakohitaji Tanganyika yenye mamlaka kamili kiko wapi kinachotikisika?
"Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni."
Kina Jussa ni wapambanaji mahiri waliodhamiria kuikomboa Zanzibar.
Muhimu kututambua - Zanzibar si Tanganyika.
Na huo ndiyo ulio ukweli.
Mimi nawaombea hayo mapambano yao yafanikiwe. Natamani kuona wakijitegemea kama nchi kwa 100%, badala ya ilivyo hivi sasa.