DOKEZO Hekta 200 za misitu zimekatwa kupata mkaa Kijiji cha Makombe (Iringa), mamlaka zipo kimya tu

DOKEZO Hekta 200 za misitu zimekatwa kupata mkaa Kijiji cha Makombe (Iringa), mamlaka zipo kimya tu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Tanzania imeweka lengo la kupunguza utoaji wa gesi chafu kwa asilimia 10 hadi 20 ifikapo Mwaka 2030. Hii ni sehemu ya jitihada za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi. Taarifa hiyo niliiona kwenye madokezo ya Ofisi ya Makamu wa Rais.

Hata hivyo, katika baadhi ya maeneo kama Kijiji cha Makombe kilichopo Mkoani Iringa, hali ni tofauti.

Mabadiliko hayo ya kimazingira yanayolenga kuboresha hali ya hewa kwa ujumla yanakinzana na shughuli kubwa zinazofanywa na wakazi wa Kijiji cha Makombe, ambapo ukataji mkaa umeshamiri kwa zaidi ya miaka miwili na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira na maisha yao yanazidi kuathirika vibaya.
IMG_0008.JPG
Katika historia ya Kijiji cha Makombe, kilimo cha mazao ya biashara kama maharage na mahindi kilikuwa chanzo kikuu cha uchumi.

Wanakijiji waliweza kupata mazao mengi, na mavuno yao yalikuwa chanzo cha kujipatia kipato cha kutosha kwa mahitaji ya kila siku.
IMG_0013.JPG
Ardhi ya kijiji hiki ilikuwa na rutuba, ikitoa mazao kwa wingi bila kutumia mbolea ya ziada lakini mabadiliko ya hali ya hewa, pamoja na ongezeko la ukataji miti kwa ajili ya mkaa, yamegeuza hali hiyo.

Wakati nimetembelea kujionea mashamba yangu hivi karibuni maeneo hayo nimekuta zaidi ya hekta 200 za misitu zimekatwa miti mikubwa ili kupata mkaa, na athari za ukataji huu ni kubwa.
IMG_0015.JPG
Kwani asilimia kubwa waliokuwa Wakulima wote wamejiingiza kwenye shughuli hiyo ambapo bado haina faida kwani walanguzi hununua gunia la mkaa kuanzia Sh. 7000 ikipanda basi ni Sh. 8000.

Shughuli hiyo imebadili kabisa hali ya hewa, mvua za tabu na hata ikinyesha inaishia milimani tu, hali ya upatikanaji maji imeanza kuwa ngumu na bahati mbaya watu bado wanaendelea kuchoma mkaa na Serikali ya Kijiji wala haichukui hatua madhubuti kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Bahati mbaya sana hata watu wa Idara ya Ardhi na Maliasili, Mkoani Iringa wanashiriki moja kwa moja kutoa vibali kwa Kijiji kwa ajili ya shughuli hiyo, hata walipofanikiwa kukamata na kuzuia shughuli hiyo watu walirudi tena kuchoma mkaa bila kuchukuliwa hatua kali.

Hii imesababisha mazao kupungua kwa kiwango kikubwa na hivyo kuwaacha wakulima wakikabiliana na changamoto za ukosefu wa chakula.
IMG_0014.JPG
Mahitaji ya nishati ya kupikia yamekuwa sababu kuu inayochochea ukataji wa miti kwa ajili ya mkaa. Serikali ichukue hatua za haraka kukabiliana na hali hii ambayo imezidi kuhatarisha mazingira na kusababisha madhara yatokanayo na ukataji miti kiholela na kuchoma mkaa.

Kijiji cha Makombe ni mfano mmoja tu wa jinsi gani ukataji mkaa na uzalishaji wa gesi chafu vinaweza kuathiri vibaya jamii.
 
Back
Top Bottom