Yaani umeandika kwa hasira za wivu na hakuna fact hata moja.
1) Gamond hamna kitu kivipi? Yanga hawachezi mpira? Hawashindi? Kocha hana mbinu? Au ni lipi la ziada ya kumfanya awe hakuna kitu?
2) huyo Nabi ambaye wanasimba mnatumia kama kielezo cha kocha bora, alipoingia Yanga mliongea maneno mengi ikiwemo ya kumfukuzisha kazi Al Merrikh na wote mlisema hamna kocha humo ila mwisho saivi nyimbo nyingi Nabi Nabi. Na hata Nabi alipoingia Yanga hakupata mafanikio ya hapo kwa papo aliitengeneza timu kwanza.
3) Ngao ya jamii ni ufunguzi wa pazia jipya la msimu hivyo pazia limefunguliwa tuone nani atavuna kipi na mpaka sasa Yanga yupo kwenye mwenendo mzuri akiwa anaongoza ligi, hilo la ngao ya jamii ni furaha iliyopita tupo kwenye ligi sasa hakuna matuta ili kumpata mshindi bali ni mwendo wa point tatu na ukusanyaji wa magoli mengi tu.
Swala la Yanga kuingia 10 bora CAF ni swala la muda tu, Yanga ametoka kwenye nafasi ya 75 kafika hadi nafasi ya 18 katika ubora wa CAF ndani ya msimu mmoja tu. Kutoka 18 hadi 10 ni gap ndogo sana usije ukaongea ukamaliza ipo siku hiko kichaka cha rank ya CAF mtakuwa mmepoteana vile vile.