Hela za MCC ni makusanyo ya masaa matatu tu kwa TRA

Hela za MCC ni makusanyo ya masaa matatu tu kwa TRA

kama unataka kusema hivyo ilitakiwa heading ibadilike na kuwa,"pesa ya MCC ni makusanyo ya TRA kwa masaa 3 kila siku kwa muda wa miaka mitano"
Mkuu sio mm nilie toa mada. Lakin ndivo ilivo. Hivo ndivo unavotakiwa kuelewa. Sio tofaut na hivo. Huo ndo ukweli wa hiyo hela ya MCC
 
Maandishi kibao lakini yamejaa porojo za kishamba sana ! Kwanza Tanzania haikunyimwa hela za MCC tu bali pia IMETIMULIWA ndani ya MCC , lakini pia kunyimwa misaada kwa sababu ya kusigina katiba ni aibu kubwa sana , kingine si kweli kwamba Tanzania inaweza kujitegemea na ndio maana mwandishi anapinga EU kujitoa , sasa kama hela za japan na wachina zinawapa faraja mmejiandaa nini ?
 
ati shs trilioni 1.4 ni makusanyo ya masaa 3 ya TRA? hujui kuwa ni zaidi ya makusanyo ya mwezi mmoja ya kodi ya nchi nzima? mkuu rudi kasome ngumbaru au memkwa.

Ni tr. 1.04 sio 1.4,
just a point of correction mkuu.
Pia inaonekana hukumwelewa aliposema masaa matatu, vipi kama mimi ntakwambia kwamba wakati MCC wanachomoa trilioni 1.04 uwezo wa serikali ya sasa kufidia pengo hilo ni mara 33 utasemaje?
Maana kwa hesabu za wazi ziko hivi:
Kama makusanyo yaliyoongezeka (ambayo hayakutarajiwa) kwa mwezi ni bil 550 hii ina maana pengo hilo litazibika kwa miezi miwili tu kati ya miezi 60 ya matumizi ya fedha hizo na chenji ya bil 960 bila kuathiri wastani wa makusanyo ya serikali ya Kikwete.
Kama pesa za MCC zingeingizwa katika bajeti ya kila mwezi serkali ingelazimika kukusanya bil 17.3kwa mwezi kama kiasi cha kuzibia pengo, hata hivyo kwa hesabu za sasa kiasi hicho kingeweza kukusanywa kwa siku 1 tu nje ya kiasi kilichokadiriwa, yaani fedha ya ziada ambayo inakusanywa kwa siku ni sh. bil 18.3
UMEELEWA?
 
MACHI 30, mwaka huu, gazeti moja la kila siku nchini liliripoti kuwa Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) la Marekani, limesitisha msaada wa zaidi ya dola milioni 700 kwa Tanzania, kiasi ambacho ni sawa na shilingi trilioni 1.4 zilizokuwa zitumike katika uboreshaji wa huduma ya umeme hususan vijijini.

Hata hivyo, kiasi halisi cha msaada huo siyo zaidi ya dola 700 kama ilivyoripotiwa na gazeti hilo, badala yake ni dola milioni 472.8 ambazo ni shilingi 1,040,160,000,000 ama trilioni 1.04 katika kiwango cha sasa cha ubadilishaji wa fedha.

Bodi ya Wakurugenzi ya MCC iliyokutana huko Marekani ilifikia uamuzi huo “kutokana na serikali ya Tanzania kutochukua hatua za kuhakikisha kuwa inaheshimu uhuru wa kujieleza na uhuru wa kujumuika katika utekelezwaji wa Sheria ya Makosa ya Mtandao”.

Mbali na hilo, bodi hiyo pia iliishutumu Tanzania kwa kuendelea na uchaguzi wa marudio wa Zanzibar “bila ya kushirikisha wote”, na pia “haukuakisi maoni ya wote licha ya kuwepo malalamiko kutoka serikali ya Marekani na jumuiya ya kimataifa”.

Msaada huo kwa Tanzania ulikuwa wa awamu ya pili baada ya dola milioni 698 za awamu ya kwanza, kiasi ambacho ni sawa na shilingi 1,535,600,000,000 au trilioni 1.53 za Tanzania na kupewa uhuru wa kuamua jinsi ya kuzitumia wenyewe.

Siku chache baadaye, taarifa nyingine ziliibuliwa kutoka kwa mwandishi mmoja wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) zikidai kuwa nchi 10 wanachama wa Umoja wa Ulaya, nazo zimejitoa kuifadhili Tanzania katika bajeti ya serikali ya mwaka 2016/2017.

Uamuzi huo nao umeibua kauli mbalimbali zikiwemo za uchochezi, uchonganishi, ufitinishaji na upotoshaji utokanao na chuki za kisiasa dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), serikali yake na hata Rais John Pombe Magufuli.

Mathalani, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe anasema: “Sitakubali kuvishwa koti la uzalendo katika suala (hili) la MCC na hilo ni suala la CCM. Kukosa misaada ya Marekani ni matokeo ya ubabe wa CCM kuhusu Zanzibar”.

Kana kwamba haitoshi, Katibu Mwenezi wa Taifa wa chama cha NCCR – Mageuzi na mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini, David Kafulila naye anasema: “Ingekuwa tumenyimwa fedha kwa kukataa ushoga ingekuwa ni fahari kwetu, lakini katika suala la kuvunja demokrasia ni aibu”.

Hizo ndizo agenda kubwa zilizopo hivi sasa, zile ambazo hata hivyo zinakuzwa ili kukidhi malengo ya kisiasa baada ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2015.

Katika andiko lao lililowekwa kwenye mtandao wa facebook, saa 4.31 asubuhi Jumatano ya wiki iliyopita, Bukobawadau Entertainment Media walinukuu hotuba ya Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyoitoa Juni, 1991 mjini Rio de Janeiro, Brazil akisema:

“Democracy is not a bottle of Coca-Cola which you can import. Democracy should develop according to that particular country” au kwa Kiswahili kwamba: “Demokrasia siyo chupa ya Coca-Cola unayoweza ukaagiza. Demokrasia lazima ikue na kuendelezwa kulingana na nchi husika”.

Aidha, nukuu nyingine ya Baba wa Taifa inahusu hotuba yake ya Januari, 1968 aliposema: “No nation has the right to make decisions for another nation, nor people for another people” na kutafsiriwa kwamba “hakuna taifa (lolote) lenye haki ya kulifanyia maamuzi taifa jingine wala watu (wanaoweza wakafanya hivyo) juu ya watu wengine”.

Mbali na hotuba hizo mbili, busara za Mwalimu Nyerere pia zimo katika Kitabu cha Azimio la Arusha aliposema: “…Ni ujinga zaidi kufikiria kuwa tutajikomboa kutoka kwenye umasikini kwa kutegemea misaada ya kigeni badala ya juhudi zetu wenyewe” (mwisho wa kunukuu).

Nawashukuru wote waliojitokeza kuchangia maoni yao kuhusu hatua hiyo ya MCC ya kusitisha msaada wake huo wa dola milioni 472.8 na siyo “zaidi ya dola milioni 700” kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Ninawapongeza pia wanapotosha kwamba nchi 10 za Umoja wa Ulaya, bila ya kutaja ni zipi nazo zimesitisha msaada wake katika bajeti ya serikali ya Tanzania ya mwaka 2016/2017 inayotarajiwa kusomwa ifikapo Aprili 21 au wiki mbili tu zijazo.

Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania na mmoja kati ya wapinzani wakubwa wa CCM na serikali yake, Deus Kibamba anasema:

“…Kwanza hapa si kwamba tunawapigia magoti wafadhili, bali inabidi tupigiane magoti wenyewe kwa sababu tumekoseana kwa kukiuka misingi ya demokrasia huko Zanzibar”.

Naamini kuwa Kibamba haipendi CCM wala serikali yake ila ni mpenzi wa upinzani, lakini anaogopa kujitokeza waziwazi na huenda anatumiwa kisiasa na baadhi ya wafadhili wake wa ndani au nje ya nchi hata kama yeye mwenyewe hafahamu.

Ndiyo maana mtazamo wake upo kinyume cha hotuba za hayati Baba wa Taifa aliposema “demokrasia lazima ikue na kuendelezwa kulingana na nchi husika”, na kwamba “hakuna taifa lenye haki ya kulifanyia maamuzi taifa jingine wala watu (wanaoweza wakafanya hivyo) juu ya watu wengine”.

Ndiyo maana anataka tukubaliane na matakwa ya Marekani ya kusitisha msaada wake kwa sababu ya uchaguzi wa marudio wa Zanzibar, hivyo alitaka usifanyike kwa sababu tu chama cha Civic United Front (CUF) na baadhi ya wahisani hawataki.

Ndiyo maana anataka serikali pia iige jinsi Jukwaa la Katiba Tanzania linavyopewa misaada, lakini yote inaambatana na masharti ambayo likishindwa kuyatekeleza linafutwa kwenye orodha ya wafadhili wake.

Katika kuthibitisha agenda ya kutaka kuigeuza Tanzania kuwa moja ya vibaraka wake kiuchumi, Marekani kamwe haitaji ni kifungu gani cha Katiba ya Zanzibar ambacho kimevunjwa kwa kufanyika uchaguzi huo mkuu wa marudio wa Machi 20, mwaka huu.

Marekani na washirika wake wanataka wawe wanakutana katika miji kama ya Washington DC, Ottawa, London, Stockholm, Paris, Brussels, Rome au Madrid; kisha wanachukua karatasi na kalamu na kuandika mihtasari ambayo inaletwa Tanzania, Nigeria, Msumbiji, Botswana na kadhalika na kupewa maagizo ya utekelezaji ndipo tupewe misaada.

Wanataka ifike siku ambayo Tanzania kwa mfano tukichagua rais kwa kuzingatia Katiba ya nchi yetu na kutoridhika naye, mathalani hivi sasa ambapo Dk. John Magufuli amechaguliwa kwa mujibu wa Ibara ya 38(1) na 39(1)(a) – (e) wanashinikiza tumwondoe, kisha wanaelekeza nani wanataka atuongoze.

Wanataka wanapokutana iwe Ufaransa, Uingereza, Marekani, Hispania, Italia, Finland au Denmark wapange kwamba ni chama gani kituongoze na kutekeleza matakwa yao, vinginevyo wanatukatia misaada kama huo wa dola milioni 472.8 za MCC.

Mbali na hayo, ukweli kuwa MCC imesitisha msaada huo kwa sababu za maslahi ya Marekani unathibitishwa na ule wa awamu ya kwanza. Dola milioni 698 tulizofadhiliwa wakati huotulipewa uhuru wa kuamua jinsi gani tunavyotaka sisi wenyewe tuzitumie kwa maendeleo yetu.

Ndiyo maana Serikali ya Awamu ya Nne iliamua bila kuingiliwa kuwa zitumike hadi katika ujenzi ama ukarabati wa barabara, hali ambayo sasa ni tofauti kwa sababu ya utekelezwaji wa Sheria ya Makosa ya Mtandaoni na uchaguzi wa marudio wa Zanzibar.

Walitaka upotoshaji na uchochezi ulioanza kufanyika kuhusu uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2015 uachwe na kuleta vurugu kubwa nchini.

Walitaka uchochezi wa mitandaoni usidhibitiwe kwa sababu walipanga kuing’oa madarakani CCM kwa kushirikiana na wapinzani. Walitaka kuweka vibaraka wao ili watumike kupora raslimali za nchi yetu, kubwa kuliko zote ikiwa ni gesi inayotarajiwa kuanza kuvunwa katika kipindi kifupi kijacho.

Lakini katika upande wa pili, Marekani kupitia kichaka chake hicho cha MCC imesitisha msaada huo ili pamoja na mambo mengine, kushinikiza Tanzania iache kushirikiana kibiashara na China.

Taarifa kutoka vyanzo kadhaa vya habari zinaonyesha kuwa baadhi ya wafanyabiashara nchini Marekani kwa kushirikiana na maseneta, tena kwa shinikizo kwa serikali yao walihoji eti kwa nini inazifadhili mpaka nchi ambazo zinashirikiana kibiashara na China, hivyo kulinufaisha kwa kiasi kikubwa taifa hilo la kikomunisti.

Habari hizo zinadai kuwa kutokana na hali hiyo ndipo ilipoletwa hoja ya kuitaka Marekani ijikite zaidi kuifadhili sekta binafsi barani Afrika, hatua ambayo utekelezaji wake ni pamoja na kusitishwa kwa msaada huo wa dola milioni 472.8 za MCC kwa nchi yetu.

Sitaki kuamini kuwa baadhi ya watu ambao ni pamoja na wabunge na viongozi waandamizi wa vyama vya siasa wanadhani kwamba Tanzania, tena kwa dunia ya sasa inaweza kuendelea kwa kutegemea misaada ya mataifa yanayodai ni wafadhili huku yenyewe nayo yakiomba.

Kila nchi inapaswa kujitegemea huku ushirikiano wa kiuchumi na nchi nyingine rafiki ukiwa wa hiari na siyo wa shinikizo. Inabidi kila taifa liwe lina haki ya kushauri, kusema na kueleza mahitaji, maoni na hata vinginevyo kulingana na hali halisi na siyo kushinikizwa ili kutekeleza matakwa ya taifa jingine.

Mfano ni uchaguzi huo wa marudio wa Zanzibar hapo Machi 20, mwaka huu, uliofanyika kwa kuzingatia Katiba yake yenyewe, hivyo taifa lolote linaloshinikiza vinginevyo ikiwemo Marekani kupitia ‘kichaka’ chake hicho cha MCC ni sawa na kitendo cha uhaini.

Akihutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani hapo Septemba 13, mwaka jana, kwenye Uwanja wa Polisi mjini Nzega, mkoa wa Tabora, Mwenyekiti wa Chadema wa Taifa, Freeman Mbowe alisema:

“…Nchi hii ni tajiri sana, lakini kutwa kucha kulialia msaada MCC. Watanzania (hivi) leo hawapati umeme hadi tukaombe MCC, (kwani hao) wamekuwa wabunge wetu? Ichagueni Chadema (kwa sababu) hatutategemea wafadhili wala masharti yao (ya ovyo), tutajenga nchi ya kujitegemea”.

Naomba nigusie mfano wa hotuba hiyo kuhusu jambo hili kwa sababu, baadhi ya viongozi wa Chadema wameishutumu CCM na serikali yake kwa kusababisha msaada huo usitishwe, hivyo huenda ukakwamisha miradi iliyotarajiwa kutekelezwa Wakala wa Umeme Vijijini au REA.

Tayari wamesahau kuwa miezi saba tu iliyopita, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama chao aliponda utegemezi wa misaada ya umeme ya MCC, kauli ambayo walianza kuiimba mikutanoni ili kutaka CCM ing’olewe madarakani na kuwekwa Chadema.

Lakini wakati wakidanganya, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Lutengano Mwakahesa amenukuliwa akisema Wakala huo haujawahi kupata fedha kutoka MCC, (badala yake) umekuwa ukiendeshwa kutokana na fedha za serikali kwa asilimia 90 na hivyo zinazotoka kwa wahisani ni karibu asilimia 10 pekee.

Anasema shughuli za REA haziwezi kusimama na serikali inatarajiwa kutoa fedha nyingi kutoka kwenye bajeti ya mwaka 2016/2017, hivyo anaamini miradi iliyopangwa kufanyika yote itakwenda vizuri.

Nimesema tangu mwanzo kwamba msaada uliositishwa na MCC ni dola za Marekani milioni 472.8 na siyo zaidi ya milioni 700, fedha ambazo ni sawa na shilingi 1,040,160,000,000 (au trilioni 1.04) kwa miaka mitano na siyo za mkupuo.

Hesabu zinaonyesha kuwa mgawanyo wa fedha hizo ni shilingi bilioni 208.032 kwa mwaka ama shilingi bilioni 17.336 kwa mwezi, kiasi kinachoweza kukusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa saa tatu tu.

Kwa mfano, wakati makusanyo ya TRA yalikuwa ni wastani wa shilingi bilioni 850 kwa mwezi hadi Oktoba 31, 2015, kiwango hicho kilipanda hadi shilingi trilioni 1.4 ilipofika Februari 29, 2016, fedha ambazo ni sawa na ongezeko la shilingi bilioni 550 kwa mwezi.

Kutokana na hali hiyo, dola milioni 472.8 ama shilingi trilioni 1.04 kwa ongezeko la shilingi bilioni 550 kwa mwezi katika makusanyo ya sasa, kiasi hicho cha juu katika hesabu hiyo kinaweza kukusanywa kwa miezi miwili tu huku chenji ya shilingi bilioni 60 ikibaki mkononi.

Wale wanaodai eti kusitishwa kwa msaada huo kutasababisha kukwama kwa miradi ya umeme wa REA wana gubu lao wenyewe, chuki zao za kisiasa na waongo wakubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam alipokuwa akitangaza makusanyo ya shilingi trilioni 1.5 yaliyofanywa na TRA kwa Januari, mwaka huu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile alisema serikali hivi sasa ina mfumo mzuri zaidi wa kubana matumizi na kuelekeza fedha nyingi kwenye miradi ya maendeleo.

Alitolea mfano kwamba mwezi huo, serikali iliweka vipaumbele vyenye tija na kutumia fedha nyingi zaidi zilizokusanywa Desemba, mwaka jana katika kutekeleza miradi hiyo, kazi iliyofanyika huku misaada ya wahisani ikichangia kidogo sana.

Alisema miradi iliyopewa kipaumbele ni ya barabara, afya, elimu, maji, umeme, ulipaji wa madeni na pensheni kwa wafanyakazi wastaafu, na kwamba jumla ya shilingi bilioni 318.406 zilikuwa ni za ndani huku fedha za wahisani zikiwa shilingi bilioni 71.2 tu.

Kabla sijahitimisha ninaomba kuzigusia nchi 10 za Ulaya ambazo pia zinadaiwa kuondoa misaada yake kwa nchi yetu, hatua iliyokuja siku chache tu baada ya MCC kutuondolea ufadhili wa dola milioni 472.8 za Marekani.

Lakini je, ukweli kuhusu jambo hili unasemaje? Anajibu mwanaharakati kijana wa maendeleo, Humphrey Polepole na kunukuliwa na mwandishi wa habari kutoka katika jiji la Mbeya, Solomon Mwansele kupitia mtandao wa kijamii wa facebook, Ijumaa iliyopita:

“Kumekuwepo na upotoshaji kwamba wahisani karibu 10 wamesitisha misaada yao kwa serikali ya Tanzania. Taarifa hizi ni za uongo na upotoshwaji na zinalenga kuleta taharuki miongoni mwa Watanzania.

“Binafsi kama raia ili kujiridhisha nimewasiliana na Wizara ya Fedha na balozi mbili kupitia maaofisa wao waandamizi na kote taarifa hizi hazina ukweli wowote.

“Kilichotokea ni mwandishi wa shirika moja la habari la nje kunukuu vibaya mazungumzo ya kiongozi (mmoja) wa Wizara ya Fedha wakati wa shughuli ya kutiliana saini msaada uliotolewa na serikali ya Japan kwa Tanzania.

“Kilichotakiwa kuripotiwa ni kwamba wafadhili hapa nchini wanaisadia serikali kwa njia mbalimbali ikiwemo (a) Mfuko wa Pamoja wa Kusaidia Bajeti au General Budget Support (b) Misaada ya Kisekta kama vile kilimo, nishati na usafirishaji na (c) Misaada kwa Miradi.

“Kilichotokea ni kwamba nchi wahisani sera zao zimekuwa zikibadilika kipindi hadi kipindi na kupelekea kubadilika kwa mtindo wa kutoa msaada kwa nchi yetu.

“Nchi kadhaa zimeonelea (kwamba) zisiendelee kuisaidia Tanzania kwa mtindo wa GBS (au Mfuko wa Pamoja wa Kusaidia Bajeti), badala yake wataendelea kuisaidia (moja kwa moja) katika sekta na miradi husika. Sekta hizi na miradi hiyo iko katika vipaumbele vya serikali.

“Mwandishi huyo wa habari alijikanganya na kuchanganya maelezo (yake) wakati wa kukijulisha chombo chake cha habari na hatimaye (pia ukauchanganya pamoja hata) umma wa Watanzania, taarifa ambazo siyo za kweli.

“Rai yangu kwa wananchi wenzangu ni kuwa ni kweli misaada ni jambo jema, lakini ni bora (kabisa) isije kama itakuwa inakuja katika masharti yanayotweza utu na heshima ya taifa letu.


“Humprey Polepole

Raia wa Tanzania” (mwisho wa kunukuu).

Nani ana swali?

Mwandishi wa makala hii ni Katibu Msaidizi, Idara ya Itikadi na Uenezi katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Anapatikana kwa Simu Na. 0659 220 220 na 0787 088 870
http:// kwako wewe kila alilosrma nyerere ni sahihi haahaa unaabudu akili ya mtu kama wewe .hiyo statement ya nyerere kuhusu coca cola is a false statement . Democrasia ni moja tu alieshinda ndio mshindi .eti unajidai eti demokrasia ina mila zake mara unajidai inadesturi zake mara inautamaduni wake mara unajidai inamatambiko yake acga kudanganya watu .demokrasia ni demokrasia tu .kwa hiyo ili uwe mzalendo ndio unajisi demokrasia .tumezikosa kwa sababu ya utapiamlo wa madarakavya chama kimoja kati ya zaidi ya vyama ishirini
 
Labda isemwe hivi, bajeti ya 16/17 ni tirioni 39.5. kati ya hizo misaada ni titooni 12. hela ya MCC tulionyimwa no trioni 1.4 ndio watu wazima wanavimba shingo ati nchi itayumba.
39-12 unapata 27!
TZ bado inategemea sana misaada ktk bajeti na hatukutakiwa tuipuuze hata Milion 100

Kumbuka na majigambo haya ya serikali hii lkn zaidi ya 30% ya bajeti yetu itategemea kuomba omba!Tungepata hii 1.4 ya bure % ya utegemezi ingeshuka kwa karibia 2%!Hii ni % kubwa sana kwa uchumi wa nchi
 
ati shs trilioni 1.4 ni makusanyo ya masaa 3 ya TRA? hujui kuwa ni zaidi ya makusanyo ya mwezi mmoja ya kodi ya nchi nzima? mkuu rudi kasome ngumbaru au memkwa.
Au kama ni kwa saa ni hivi:
Fidia ya fedha za MCC ni mil. 24 kwa saa,
Lakini fedha ya ziada inayokusanywa kwa dakika 1 mil 12.7 hiyo ina maana fidia ya fedha za MCC inayohitajika kwa saa 1 inafidiwa kwa chini ya dk2, kengele wewe
 
I see katika watu waliomnukuu baba wa taifa vibaya wewe unaongoza, demokrasia aliyokuwa anaisema Nyerere yakutokuamliwa na watu wengine sio hiyo ya kuwadhulumu wananchi walichoamua au kuwa nyima haki wengine kisa hawakubaliani na CCM. Angekuwa na mawazo kama yako ktk demokrasia nadhani mpaka leo tusingekuwa na vyama vingi. Msipindishe mawazo mazuri ya Nyerere kwa kuhalalisha dhuluma zenu.Uchaguzi wa meya wajiji la dsm umechukua miezi zaidi ya mitatu ili kujaribu kupindisha haki iliyo wazi, znz demokrasia inaminywa bado unataka kuhalalisha demokrasi yako ya kipeasant kwa kumnukuu nyerere, Msipotoshe upeo mkubwa aliokuwa nao nyerere kwa mawazo yenu ya mgando kiasi hicho.
 
Ni sawa na kusema
Baada ya MCC kuchomoa trl 1.04 shirika la Kitanzania liitwalo TM limejibu kwa kuipa Tanzania sh. tr 33 karibu mara 33 ya msaada wa MCC ulioondolewa.
Ndicho kiilichotokea ndugu
 
security guard
Hata hesabu ndogo kama hii hauijui?TZ inakusanya Trilion 1.3 KWA MWEZI na hela ya bure tuliyo nyimwa na MCC ni Trilion 1.4

Hela ya bure tuliyo nyimwa ni zaidi ya makusanyo ya TRA ya mwezi mzima na ndiyo maana hata Rais wetu inamuuma sana
na katika hio makusanyo ya mwezi tr. 1.3, je vipi matumizi ya mwezi ya serikali yanalipwa kutoka wapi?
 
Tuweke hivi,kwenye makadirio ya bajeti,matumizi ya kawaida ya serikali yamezidi makusanyo ya TRA.Miradi ya maendeleo itategemea misaada na mikopo!Tunashabikia nin hapa?
Bajeti trilion 29
pesa itakayokusanywa makadirio max ni trilion 17
matumizi ya kawaida ni trilion 17.8
mikopo na msaada trilion 12

hapo tunachekelea nn
 
Hatuchekelei ila ukweli usipindishwe.

Mimi pia nakubaliana na wanaosema bado tunahitaji misaada ili kufikia hatua ya kujitegemea bila kuombaomba, ila ukweli wa hesabu ndio huo
 
Sijui kwa nini Humphrey anajitia UJUHA namna hii...
Ni kwa nini ccm walikubali mchezo huu wa siasa za "demokrasia" ikiwa hawataki demokrasia ktk chaguzi zetu...?!
Ni kama vile, wao CCM ndio "alfa na omega" ktk siasa za nchi hii.... Wanatumia Mahakama watakavyo, ndio maana walitaka kutakatisha uhalifu wao wa kufuta uchaguzi wa Zanzibar, kwa kuwashawishi CUF waende Mahakamani huku wakijua walishamaliza kila kitu huko...
Kama vyombo vya kisheria kweli vipo Zanzibar, kwa nini hawachukui hatua kwa vijana wake wanaochochea ubaguzi ktk maskani ya kisonge...?!
Ya nini kutunga sheria za kudhibiti wahalifu wa mitandaoni wakati hawa walio wazi kabisa mchana kweupe wanaopita na mabango ya uchochezi wao wanasindikizwa na Polisi wasibugudhiwe....?!
MCC si kwa ajili ya nyie ccm kupata fedha tuu, ni kwa ajili pia ya kuonyesha mnawatendea WANANCHI kwa HAKI kama mlivyokubaliana na MCC...
Sasa mmeshindwa masharti, mnaanza kusema "HATUZITAKI MBICHI HIZI"....
Hii ni aibu yenu peke yenu ccm...., haituhusu sisi wananchi.., Pole pole acha porojo zako...!
 
kinachofanywa na ccm ni kualalisha wakati ukifika wa kulipa kisasi watu wasiwe na huruma na lolote litakalokuwa linafanyika yaani itakuwa kama vike mtu anavyoua nyoka. mwenye masikio na asikie
 
MACHI 30,
“Humprey Polepole

Raia wa Tanzania” (mwisho wa kunukuu).

Nani ana swali?

Mwandishi wa makala hii ni Katibu Msaidizi, Idara ya Itikadi na Uenezi katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Anapatikana kwa Simu Na. 0659 220 220 na 0787 088 870
Habari imejaa upotoshaji sana. Nilifikiria numjibu hapa au kwingineko.

Kipande nilichonukuu kama sikosei kinaonyesha katibu msaidizi idara ya uenezi.
Kwa muda mrefu huyu bwana amejitambulisha kama mwananchi na Raia.

Hata 'alipobwanwa' hakuwahi kusema nyadhifa zake ndani ya chama.

Huyu alikuwa mjumbe wa tume ya Warioba, tunaona kwanini maoni ya tume yalishindwa kwa kuwa na ''double agent''

Hata hivyo, nimpe kionjo kidogo. Kumnukuu Mwlalimu Nyerere kibubusa ni matusi

Nyerere aliposema hayo alimaanisha demokrasia tunayoikubali wenyewe ndiyo ituongoze.Nyerere hakusema uhuni wa demokrasia ndio uongoze

Pili, anasema Marekani haijaonyesha kifungu cha katiba ya ZNZ kilichokiukwa

Huyu bwana ameshaulizwa, ni kifungu gani kilichompa Jecha mamlaka ya kufuta uchaguzi?Hakuwahi kuonuesha hata siku moja

Huyu bw hajaonyesha ni kifungu gani cha sheria kinachozungumzia uchaguzi wa marudio katika katiba ya SMZ? Hajawahi kuonyesha hata siku moja

Mwandishi anawatuhumu Marekani kuingilia mambo ya ndani.

Hatuelezi kwanini Rais JK akiwa mwenyekiti wa CCM pia alifanya safari za kwenda kusaini mikataba Washington

Hivi nani alishinikiza, sisi tuliokwenda au walioweka masharti tukayafuata?

Rais Magufuli yupo katika rekodi akisema MCC ina manufaa.

Mwandishi atueleze lini Rais alifuata kauli hiyo na kama hajafuta, mwandishi anataka kutueleza nini kuhusu serikali iliyopo madarakani?

Polepole yupo katika rekodi akisema Taifa letu linaongozwa kwa viongozi kuwa waongo. Pengine alijua siri hiyo maana yale ya sisi kuishi kama Taifa la waongo yanaonekana wazi katika bandiko lake

Hoja zake hazinisumbui, kinachonisumbua ni kuona vijana wadogo wa umri kama huu wanapoingia katika siasa za kulihadaa Taifa. Kwamba tunaishi kama Taifa la waongo, na uongo sasa ni fani. Kwamba, hatuwezi kuweka mkate mezani hadi tutunge uongo

Taifa hili lina safari ndefu, kuondoa umasikini, maradhi , ujinga na kizazi cha waongo
 
na katika hio makusanyo ya mwezi tr. 1.3, je vipi matumizi ya mwezi ya serikali yanalipwa kutoka wapi?
Statistically we do not save anything!
Mishahara tu inakula karibia nusu ya makusanyo haya,bado mgao wa ZNZ na malipo ya nishati kwa wizara za serikali na taasisi zake

Ukiweka hapo na huduma ya majeshi yetu utaona bado tunahitaji tuongeze nguvu ya kukusanya au tukope kwa "wakubwa" ambao leo tunawaita majina yasiyofaa
 
security guard
Hata hesabu ndogo kama hii hauijui?TZ inakusanya Trilion 1.3 KWA MWEZI na hela ya bure tuliyo nyimwa na MCC ni Trilion 1.4

Hela ya bure tuliyo nyimwa ni zaidi ya makusanyo ya TRA ya mwezi mzima na ndiyo maana hata Rais wetu inamuuma sana
Nadhani watu wengi pamoja na wewe haujaelewa hiyo pesa ya MCC hutolewa kwa miaka 5 na sio kila mwezi. Hesabu halisi the ni takriban 1.04 Trillion na sio 1.4 mkuu. Hiyo pesa kwa mwaka 1 ni 208Bil. Ni Sawa na bil 17.3 kwa mwezi, kwa wiki ni bil 4.3. Hivyo sio pesa nyingi sana ya katisha kwa serikali kama tunavyoaminishwa. Usinielewe kuwa namaanisha hatuhitaji hiyo pesa, HAPANA. Kila shilingi ni muhimu kuipata kuliko kukosa hata kama ingekuwa mil 1 kwa mwezi maana kuna kazi itafanya. Ila nataka tu tuelewe sio pesa nyingi kiivyo.
 
Lo! Mada yako imekaa vizuri, imeeleweka na umeipangilia vema, nami nakuunga mkono 1% kwa sababu haiwezekani jasho tunalohenyekea kukusanya kwa mwezi unalidharau kwamba linaweza kukusanywa kwa masaa, hapo umeongopa au hesabu haipandi. Hata ukiwatumia Al-Shaabab, Boko Haram, Taleban, Islamic State, Al Qaida, Ant Baraka n.k huwezi kuikusanya trilioni 1.4 kwa masaa matatu, never.

Mimi binafsi kunyimwa msaada wa 1.04 trilioni hakunitishi chochote, kinachonitisha ni aina ya siasa na demokrasia tuliyoamua kufuata kuhusu Zanzibar.
 
security guard
Hata hesabu ndogo kama hii hauijui?TZ inakusanya Trilion 1.3 KWA MWEZI na hela ya bure tuliyo nyimwa na MCC ni Trilion 1.4

Hela ya bure tuliyo nyimwa ni zaidi ya makusanyo ya TRA ya mwezi mzima na ndiyo maana hata Rais wetu inamuuma sana
Mkuu ume tumia neno BURE
Ktk hii dunia BURE ni ghali sanaaaa tu.Nyara za inchi ndio zimewekwa RUHANI Na hiyo BURE
 
Back
Top Bottom