Hela zinatengenezwaje? Tupeni Shule

Hela zinatengenezwaje? Tupeni Shule

Swadataa

Senior Member
Joined
Dec 9, 2013
Posts
161
Reaction score
65
Wakuu wanaJF, bila shaka tuna maarifa mbalimbali ambayo naweza sema hutokana na elimu zetu tofauti. Kwa maana hiyo tunaweza kubadilishana uelewa.

Tunajua fedha zinatengenezwa, na zingine zinachakaa. Sasa naombeni kujua ni namna gani fedha (note/coin) mpya zinaingizwa kwenye mfumo?
Na ni busara gani husaidia kujua ni fedha kiasi fulani mpya zitengenezwe?

Mabenki huwa yanatoa mikopo, lakini pesa zinarudi kwa riba. Maana yake ni nyingi zinazorudi benki kuliko zinazotoka (kuingia ktk mzunguko). Ni njia gani hutumika kuhakikisha zipo ktk balance?
Je kama ikitokea pesa zinazowekwa benki (deposit) zikawa chache, kuliko zinazotoka (withdrawal) ni mbinu gani hutumika kuzuia hilo?

WanaJF, najua tupo wengi tusiojua mechanism of money. Kwa wanaojua naombeni kusaidiwa hayo maswali. Na wasio jua km mm, tusaidiane kuongeza maswali.
 
note simetengenezwa kwa cotton ana linen sio karatasi ya kawaida japo sometimes material zinatofautiana baina ya ela ya nchi moja na nyingine lakini lazima cotton ihusike.
Mfano dollar ni 75% cotton na 25% linen
Note za tanzania 75% cotton. Sio karatasi kama watu wengi wanavyo fikiria ndiyo maana note uchukua muda mrefu kachakaa na kuchanika hata kama ukiikunja.
Note fake ambazo ni karatasi ni rahisi kuigundua na huchakaa haraka.
Kila note ina namba zake ambazo ni identical.
 
note simetengenezwa kwa cotton ana linen sio karatasi ya kawaida japo sometimes material zinatofautiana baina ya ela ya nchi moja na nyingine lakini lazima cotton ihusike.
Mfano dollar ni 75% cotton na 25% linen
Note za tanzania 75% cotton. Sio karatasi kama watu wengi wanavyo fikiria ndiyo maana note uchukua muda mrefu kachakaa na kuchanika hata kama ukiikunja.
Note fake ambazo ni karatasi ni rahisi kuigundua na huchakaa haraka.
Kila note ina namba zake ambazo ni identical.

Ha ha ha, mkuu umezungumzia raw material ya kutengenezea note.

Au nibadili swali: ni kanuni gani huongoza katika kuongeza au kuingiza fedha kwenye mzunguko?

Mfano, kuna uhusiano wowote kati ya inflation na idadi ya fedha (note) zilizo katika mzunguko. Naomba ufafanuzi ikiwa ni pamoja na maswali yaliyotangulia.
 
Hapo mchumi anahitajika, hata mimi kuna baadhi ya maswali umeuliza nilikua najiuliza siku nyingi lakini sikupata majibu. Wachumi tusaidieni majibu.
 
note simetengenezwa kwa cotton ana linen sio karatasi ya kawaida japo sometimes material zinatofautiana baina ya ela ya nchi moja na nyingine lakini lazima cotton ihusike.
Mfano dollar ni 75% cotton na 25% linen
Note za tanzania 75% cotton. Sio karatasi kama watu wengi wanavyo fikiria ndiyo maana note uchukua muda mrefu kachakaa na kuchanika hata kama ukiikunja.
Note fake ambazo ni karatasi ni rahisi kuigundua na huchakaa haraka.
Kila note ina namba zake ambazo ni identical.

Ya Tanzania sio kweli kwa asilimia 75 cottons, pesa inachoka mara moja ikipata joto tu la makalio
 
Ha ha ha, mkuu umezungumzia raw material ya kutengenezea note.

Au nibadili swali: ni kanuni gani huongoza katika kuongeza au kuingiza fedha kwenye mzunguko?

Mfano, kuna uhusiano wowote kati ya inflation na idadi ya fedha (note) zilizo katika mzunguko. Naomba ufafanuzi ikiwa ni pamoja na maswali yaliyotangulia.

Ok kwa uelewa wangu mdogo ni hivi.
Kila note ina namba identical ambayo huitambulisha note husika, hivyo benki kuu wanakuwa wanajua ni note kuanzia namba flani mpaka flani zilizopo kwenye mzunguko, na zikichokaa zinarudishwa BOT wana zireplace.
Kuhusu inflation, ela nyingi ikiwa kwenye mzunguko inapelekea demand ya ela kuwa ndogo na hii husababisha inflation hivyo kuzipunguza, serikali uwa issue bonds ili kupunguza ela iliyopo mikononi mwa wananchi maana watu watalipia ela kununua hizo bonds.
Ela ikiwa ndogo ikaonekana inahitajika kuongeza mzunguko serikali inanunua bonds kwa pesa nyingi zaidi ya ilivyowauzia wananchi hivyo ikilipa inaongeza mzunguko wa notes na coins.
 
Mpaka sasa majibu bado hajajitosheleza… kama ni mvua sasa hii ni manyunyu… muuliza swali ameuliza swali linahotaji majibubna ufafanuzi wa kina…
 
Swali kaka zuri! Linahusu sana wanauchumi! Ila ni Zuri kwa kila Mwananchi angejua ili kuweza kujua impact tunazo sababisha katika uchumi wetu kama wananchi, companies, banks and Central bank.

Jibu lake sio Rocket science, ila linaitaji muda na a page or two ku lielezea. Ngoja Nikufungue macho kisha mafundi wengine watachangia kurekebisha ama kumalizia. jaribu ku google kitu inaitwa money circulation flow, then click pictures utapata idea jinsi gani pesa inazunguka. Hiyo circleinapo goma, kwa mfano mimi na wewe hatuna kazi ama kipato chetu kidogo, inamaana hata matumizi yetu yanakkuwa ya kubana. Mbele ya yote tutazungumzia whenand why does the central bank have toinject money into the society. Jaribu kugoogle yafuatayo kisha ntarudi tumalizie darasa. Supply and Demand, Inflation,Deflation, Money circle flow na hata overheated economy ili tukigusa export andimport usije kushangaa kwanini export can have negative impact, Huna haja yakuelewa sana ila jaribu kupata overview ili tukiendelea unajua ninitunazungumzia. Wacha tupige kazi kwanza tutarudi kama wengine hawajaweka ufunditayari………………………………….
 
kwa sababu jibu inabidi kuwa la kina ili mtu kuelewa..........
 
ngoja nimuite huyu aje kusaidia SUPU YA MAWE

Akija muulze tena 1. je idadi ya noti na sarafu hutengenezwa kulingana na idadi ya raia wa nchi husika? 2.Sisi raia tutajuaje kwamba sasa money circulation ipo balanced? 3.je hakuna uwezekano wa watu wachache wa BOT wakaagiza mibunda yao ya noti na wakaingza ktk circulation mbali ya zle zinaztamblika na system? 4.Wale wajomba wanaotngeneza pesa bandia ni vibaka wa manzese au ni wasomi flan hv...5.kile kipindi cha nchi kubadili noti mpya labda ya 10000 huwa kuna ulinzi kias gan kma wajomba wakitngneza zao bandia na wakaenda nazo mikoan kabla zle halis hazjazagaa? Tuanzie hapa kwnza lakn maswali ni mengi sn.
 
Last edited by a moderator:
Nadhani swali lako la msingi ni kwamba fedha mpya zinaingiaje na zinatokaje kwenye uchumi. Hayo maswali mengine naona kama yanarudia swali hili. Nitajitahidi kujibu swali kwa lugha inayoeleweka na mtu wa kawaida kabisa.

Kwa sasa Sahau benki zote isipokuwa bank kuu (bot) ili tuwe pamoja. BOT ndio inayojaza na kupunguza kiasi cha fedha kwenye uchumi. Kwanini BoT wapunguze au kuongeza? Ni kwasababu zikijaa bila ongezeko la uzalishaji kunakuwa na mfumuko wa bei za bidhaa. Zikipungua sana manake vitega uchumi vinapungua na kudidimiza uchumi. Kwa maana hii BOT wanajuwa kiasi cha fedha kilichopo kwenye uchumi na mwenendo wa shughuli za uchumi. Ila kumbuka mara nyingi huwa siri kwasababu ya kuhofia wajamaa wanaoitwa speculators kwa kimombo ambao wakijuwa kiasi cha fedha na mwenendo wake wanaweza kuutikisa uchumi au kuuangusha. Nadhani unapata wazo sasa kwamba kama kusingekuwa na usiri huu labda usingekuwa umeanzisha uzi huu.

BOT wapunguza vipi fedha wakishagundua kimahesabu kwamba zimejaa? Wapunguza kwa njia kuu tatu. Moja wanapandisha riba kwa mabenki ya kibiashara yanayokopa kutoka BoT. Kwa maana benki za biashara zitaweka ela zao BoT ili zipate riba kubwa bila jasho na zikifanya hivyo zinapunguza fedha kwenye mzunguko. Pili kwa kushirikiana na serikali BoT inauza bonds kwa matajiri na mabenki. Bonds zikiuzwa zinarudisha fedha BoT. Tatu, BoT inashirikiana na serikali kuongeza uzalishaji ili kufifisha ujazo wa fedha. Ili kuongeza kiasi cha fedha BoT itafanya kinyume cha hizo njia tatu hapo juu. Vile vile wanaweza kuchukua njia ya mkato ya kuchapisha fedha (borrowing/printing) njia ambayo sio nzuri na mara nyingi inatumika wakati wa vita au janga ambalo haliwezi kuvutiwa subira.

Sasa ifahamike kwamba BoT haina ujanja wa kufidia noti kadhaa zilizoharibika au kuchomwa moto. Yenyewe inashughulika na fedha kupwa na kujaa kufuatana na mwenendo wa uchumi. Uwapo wa noti mpya mtaani hauna maana wakati wote kwamba unafidia fedha iliyopotea kwenye uchumi. Kusanya fedha zote chakavu na zipeleke bank yeyote na utapata mpya bila maswali.

Nimalize kwa kusema kwamba BoT kimsingi inaongeza ela na kupunguza kwa kutumia mahesabu ya hali ya juu na ya usiri. Wala kimsingi hatutakiwi kujua ni lini ela zimeongezwa na kiasi gani. Labda zinapotangazwa bonds kuuzwa tu lakini hatujui zinaponunuliwa. Ukisoma uchumi wa money and financial institutions utafundishwa mahesabu ya kupima ujazo wa fedha na mahesabu yake, lakini bado huwezi kutumia nadharia hiyo ukajuwa kiasi kilichopo na kama ni sahihi au sio sahihi hadi uwe ndani ya BoT maana huko kuna factors nyingi ambazo unatakiwa uzitumie kimahesabu.
 
Elimu tosha ya uchumi thanks MgonjwaUkimwi, ila nikusahihishe tu mara nyingine na pia kwa nchi zilizoendelea money supply kwa njia ya printing serikali inatangaza kabisa kwamba watafanya quantitave easing mfano Uingereza walitangaza wanaongeza pesa kwenye mzunguko kiasi cha £160 bn kwa ku print na walifanya hivyo mara mbili wakati wa credit crunch. £160bn each haikuwa siri walitangaza kabisa. Kumbuka budget yetu kwa mwaka haizidi hata £20bn !
 
Last edited by a moderator:
Asante Mtanganyika kwa ufafanuzi, nichangie tu kwa kutetea point ya usiri nyakati za kawaida. Uchumi unapokuwa taabani of course central bank ndio zinazopokea kilio na hapa economic actors wote wanajuwa kwamba central bank itachukuwa hatua. Katika hali hii central bank itatangaza ili ku restore business confidence na hivyo ku neutralize negative impact ya speculators. Na hii imetokea USA miaka ya 2006 ambapo bank ilitakiwa kufanya bailouts kufuatia anguko la uchumi. Lakini nisisitize kwamba kama upungufu au ujazo wa fedha hauna immediate implications kwenye uchumi, basi kinachoweza kutangazwa ni monetary policy na sio kiasi kilichopo na kinachotakiwa kuongezwa au kupunguza.

Nitakuwa mchoyo wa shukrani kama sitakubali utofauti wa nchi zilizoendelea na nchi masikini kama yetu kama ambavyo umebainisha. Kweli kabisa kwamba usiri huu wa central bank unaweza usilete maana kwenye nchi ambazo zina wafanyabiashara na wawekezaji wanaoweza kufanya economic forecasting na wakautikisa uchumi kwa faida yao. Kwa mantiki hii bora nchi ikafanya partial disclosure kuliko kuwa na usiri 100 ambao unaweza kuugharimu uchumi. Sambamba na hilo kwenye nchi zilizoendelea wawekezaji wanatakiwa wapunguziwe uncertainty kwenye shughuli zao na hivyo central ina jukumu la kuwahakikishia wadau hawa kwamba something will always be done to reduce uncertainty kwenye biashara zao.
 
Tunajua fedha zinatengenezwa, na zingine zinachakaa. Sasa naombeni kujua ni namna gani fedha (note/coin) mpya zinaingizwa kwenye mfumo?
Na ni busara gani husaidia kujua ni fedha kiasi fulani mpya zitengenezwe?
__________________________
Nianze kufafanua kua,kazi kubwa ya mabenki ni kukusanya fedha zilizo kwenye mzunguko ambapo kwa njia ya mzunguko,tukisema mzunguko tunamaanisha kutoa na kupokea (kupokezana). Katika mzunguko huu,benki hupokea pesa kutoka kwa Benki kuu,nazo benki hugawa fedha kwa watumiaji.
Pia ieleweke kua sio kila benki hupokea fedha kutoka Benki Kuu,benki nyingine hupokea fedha kutoka benki nyingine.
Njia hii ya kupokezana fedha (Yaani mzunguko) husaidia kutambua fedha chakavu,fedha chakavu upokelewa na benki kwa njia ile ile benki huzipeleka Benki kuu. Benki kuu ndio yenye jukumu la kutoa Hela chafu kwenye mzunguko na kuleta fedha mpya. Benki kuu huwa inakusanya hizi fedha chakavu na kuziteketeza (Kwa njia zao sahihi) na kutengeneza fedha mpya. Benki kuu,kwakutumia takwimu za Kibenki hujua mzunguko halisi wa fedha,wana takwimu za fedha chakavu na wao ndio hutoa hizi hela kwa utaratibu usiku. Benki Kuu au kwa lugha ya kukopa (Central Bank) ndio inakaa kama muhimili wa Bank Zote,na mwisho wa siku fedha zote hurudi kwao.
Busara gani 👈 Sio Busara bali takwimu husika,zinajua hitaji la mzunguko na wanahakikisha wanapeleka kiasi sahihi.
Kumbuka hela yako haina thamani kama umeichimbia tu Chini na haipo kwenye mzunguko
 
Back
Top Bottom