Helena Ceausescu mwanamke mpenda shahada aliyejiponza na kumponza mumewe

Helena Ceausescu mwanamke mpenda shahada aliyejiponza na kumponza mumewe

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
7,672
Reaction score
9,039
Kwa wana JF ambao wako kwenye miaka yao 50 kwenda juu, watakuwa wanamkumbuka Helena mwanamke habithi mke wa rais wa Romania aliyeuawa pamoja naye Nicolae Causescu.

Huyu mama alipenda udaktari. Alitumia madaraka ya mumewe kulazimisha vyuo vimtunuku shahada za heshima.

Hakuishia hapo, aliwalazimisha waandishi wa vitabu kuandika vitabu tena kwa kitaaluma na kuweka jina lake ili ajulikane kama mwandishi.

Kila nchi alikofanya ziara mumewe, mabalozi walijitahidi kushawishi vyuo vimpatie bi mkubwa shahada za heshima. Vihiyo hawa wawili walipenda na kufurahia uongo huu wasijue una mwisho.

Taratibu, tamaa na ugonjwa wake yaani maniac alimwambukiza mumewe. Walifikia mahali kujiona kuwa wao hawakosei na lazima wasifiwe na kuwakosoa kulijibiwa kwa adhabu ya kifo.

Taratibu, walijisahau kuwa umma nao una akili na mipango yake. Walipozidisha mbwembwe, utawala wao ulipinduliwa kupitia maandamano ya umma nao wakauawa pamoja na kufunga kesi hii ya kipumbavu ya kulewa madaraka na kutaka sifa bila kustahili. Uchawa haukuza jana.

ceausecu-execution.jpg

Picha: Nicolae na Helena Ceausescu siku waliyouawa​
 
Back
Top Bottom