Elections 2010 HELiCOPTOR YA DR. SLAA YAPOTELEA ANGANI, YASHINDWA KUTUA NSHAMBA- MULEBA

Ta Muganyizi

R I P
Joined
Oct 19, 2010
Posts
5,355
Reaction score
2,736
Ni katika hali ambayo wananchi wa Nshamba Wilaya ya Muleba bado wanajiuliza na kushangaa hadi hivi sasa ambapo baada ya Mgombea kwa tiketi ya CHADEMA , Dr. Slaa kufunika Bukoba kwa wale walohudhuria kuwa mara mbili au tatu ya wale waliokuwako siku J.K yuko Bukoba, Wananchi wa Nshamba wilaya ya Muleba walimsubiri sana Mh. Slaa na kufanya watu watoke vijiji vya mbali kuja kumuona Dr. Slaa ambaye walidai huwa wanamsikia kwenye redio zao hata zile za mbao hasa kipindi cha Bunge jinsi anavyo tetea maslahi ya nchi hii. Watu hao walofurika hapo Nshamba walisubiri Tangu saa nane mchana hadi saa 12 jioni wakitegemea kuwa Dr. Slaa angejitokeza hiyo tarehe 15/10/2010 lakini hakutokea. Baada ya kufuatilia sababu ya Dr.Slaa kutoonekana ikasemekana kuwa Helcopter ya Dr. Slaa ilipotelea angani na kujikuta iko ndani ya eneo jingine liitwalo NGOTE badala ya Kutua Nshamba Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera. Baada ya Tukio hilo zikafuatia habari mbali mbali na maoni tofauti kuwa helicopter hiyo ilijikuta maeneo ya Geita mkoa mpya badala ya Nshamba Wilayani Muleba.Wengine wanasema rubani hakuwa na direction za Nshamba na sababu kibao. Hali hii imewaweka roho juu juu ya kutaka wajue ni lini mgombea huyo anarudi ili wahakikishe kuwa baiskeli na pikipiki zao hazipati pancha na kushindwa kumuona na kumsikiliza mgombea huyo. Watu wa Nshamba wanasema Kura za urais kwa Dr> Slaa ni nyingi lakini kufika kwake kungewaongezea imani zaidi na kujionea na kuhakikisha kura atakazopata. Wachache wanaanza kujiuliza kuwa kama ahadi yake ya Kuwafikia inashindikana , vipi zile anazoahidi kuifanyia nchi? Ndipo wakatulizwa kwa kuambiwa kuwa tarehe 24/10/2010 Dr. Slaa atakuwa ndani ya Kagera ila isijulikane ni lini atakanyaga hapo Nshamba. Nilipododosa kuhusu Kura za Mbunge walisema zilizo nyingi anapewa mpiganaji mwingine kwa jina la Prof. Anna Tibaijuka ambaye wanaamini kuwa wakiungana na Dr. Slaa (endapo ataingia ikulu) mambo yatakuwa shwari. Maana wanaamini U DR. wa Slaa si wa heshima bali ni wa kula kitabu ki-ukweli, pia Prof . Tibaijuka vilevile, hivyo kuamini kuwa hiyo itakuwa combination ya Ngassa na Mgosi!!!!!!(hahahahahaaaaa) wananchi bwana!! Sasa mwenye mawasiliano na DR. Slaa au kamati yake ya Kampeni watangaze mapema kuwa Dr. Slaa anarudi lini Nshamba?

UTANI ULIOENEA MKOANI KAGERA

Eti kwa kuwa Mke wa Dr. Slaa ni Kutoka Kagera basi wana Kagera woote ni Shemejiiiiiii wa Mgombea. hahahaaaaaaaaa, yaani nikacheka sana, ni kauliza kwa hiyo???? Wakasema mwaka huu watataka ""first lady atokee hukuhuku""!!!!!!!LOh. Kwa hiyo hawafanyi kosa kabisaaa. Sasa ngja tuoneeeeeee . Picha ya mwaka huu kali. niulizeni zaidi niwaelezee. 0754918212
 
Hongera wana kagera kupata First Lady mwaka huu. Lakini kazi bado kazi ipo ya kumtoa Salma (F. Lady wa sasa) ikulu.
 
 
Pia katika ziara ya dr ajitahidi awezavyo atue kilolo iringa maana amengojewa kwa hamu sana na hakupita!
 
Ok asante kaka Rutashubanyuma. Lakini hata nikifa kivuli kitaishi!!!! Binadamu akichoka kachoka mabadiliko nayaona hivihivi. Usiku wa kuamkia leo nimeota (hii ni ndoto yangu) Slaa kawa kashinda uchaguzi, nikaona tume wanakuwa na utata kutangaza matokeo, ghafla mambo ya ajabu yakaanza mara nikaona eti jeshi ndo liko ikulu, ile najiandaa kuja Dar es Salaaam kuhoji kulikoni ahh nikaamka usingizini sijui maanake nini, naomba ufafanuzi!!!Pia kati ya ndoto hiyo nikaona Anna Kilango Waziri wa Maliasili na Utalii, Zitto Waziri Sheria na katiba , Mnyika waziri wa Uchumi, Mwakyembe- NIshati na Madini, Ole Sendeka, Mgana Msindai, Lucas seleliii akawa mbunge wa kuteuliwa, naye kapewa uwaziri yaani ndoto pamoja niliwataja hapo juu ila sikukariri vitengo vyao.Nikaona Mafisadi wamedakwa waliorudisha ela za epa nikaona wanabanwa kuwa wajitokeze wapewe risit za fedha walizorudisha , ghafla nikaona wanajitokeza lakini wana viwiliwili tu hawana vichwa, maana ningewaona laiv ningewataja lohhh!!!! Ndoto nyingine bwana zinatishaaaaa
 
hahahaaaaaaaaaa!! ukabila wa chadema mstake kutuambukiza wahaya! kama chopa imepotea njia na kwenda geita hata maendeleo yataenda kutua moshi badala ya tanzania!! heheheeeee!
 

Rostam hakuwepo?
 
Rostam hakuwepo?

ni wengi mno wanomngoja kwa kweli mkombozi wetu Dr. WEAPON, ilikuwa ni fikra zangu mwanzo kuwa Mh.Dr. WEAPON (Slaa) hatambuliki vijijini ila ajabu juzi nimetoka kusalimia kwetu singida vijijini hadi bibi yangu kesha sikia habari zake nlipomuuliza kuhusu yupi anatarajia kumchagua mwaka huu.,.



JAMANI NAOMBA MSAADA WENU MWENYE MAWASILIANO NA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ARUSHA MJINI Bw LEMA, AMTAARIFU MBINU ANAYOTUMIA HUYU MAMA WA CCM BAADA YA KUONA KILA ANAPOKWENDA ANAZOMEWA, SASA ANAINGIA VIWANDANI NA KUKUTANA NA WAFANYAKAZI KISHA KUZUNGUMZA NAO NA KUACHA FEDHA NYINGI KWA UONGOZI WA KIWANDA ILI WAGAWIWE KILA MFANYAKAZI KUSHAWISHI WAMPIGIE KURA, JANA ALIKUWA VIWANDA VYA SUN FLAG NA A TO Z ARUSHA AKIFANYA HAYA..HAIKUNIPENDEZA KWANI MIE BINAFSI SIKUHITAJI HATA KUONA SENTI YAO PINDI TULIPOANZA KUGAWIWA NA UONGOZI WA KIWANDA
 
JAMANI NAOMBA MSAADA WENU MWENYE MAWASILIANO NA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ARUSHA MJINI Bw LEMA, AMTAARIFU MBINU ANAYOTUMIA HUYU MAMA WA CCM BAADA YA KUONA KILA ANAPOKWENDA ANAZOMEWA, SASA ANAINGIA VIWANDANI NA KUKUTANA NA WAFANYAKAZI KISHA KUZUNGUMZA NAO NA KUACHA FEDHA NYINGI KWA UONGOZI WA KIWANDA ILI WAGAWIWE KILA MFANYAKAZI KUSHAWISHI WAMPIGIE KURA, JANA ALIKUWA VIWANDA VYA SUN FLAG NA A TO Z ARUSHA AKIFANYA HAYA..HAIKUNIPENDEZA KWANI MIE BINAFSI SIKUHITAJI HATA KUONA SENTI YAO PINDI TULIPOANZA KUGAWIWA NA UONGOZI WA KIWANDA[/QUOTE]

Mamamaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, yaani mwana kumbe hali ni hivi, sasa tufanyeje jamaniiiiiii?????????? AGGHHH wewe kula hiyo hela alfu kura yako mpe umpendayo.
 
Utani mwingine utaua watu kwa pressure? Heading haiku kaa vizuri!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mimi Ta Muganyizi sijambo, Sijui Muganyizi na Rutashubanyumaaaa, WEWE je? Dr. Slaa juu. Loh! Sijui tutapata fist lady mpya!!!??
 
dalili za mikosi kwa huyu jamaa.
hatoweza kutua ikulu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…