Ta Muganyizi
R I P
- Oct 19, 2010
- 5,355
- 2,736
Ni katika hali ambayo wananchi wa Nshamba Wilaya ya Muleba bado wanajiuliza na kushangaa hadi hivi sasa ambapo baada ya Mgombea kwa tiketi ya CHADEMA , Dr. Slaa kufunika Bukoba kwa wale walohudhuria kuwa mara mbili au tatu ya wale waliokuwako siku J.K yuko Bukoba, Wananchi wa Nshamba wilaya ya Muleba walimsubiri sana Mh. Slaa na kufanya watu watoke vijiji vya mbali kuja kumuona Dr. Slaa ambaye walidai huwa wanamsikia kwenye redio zao hata zile za mbao hasa kipindi cha Bunge jinsi anavyo tetea maslahi ya nchi hii. Watu hao walofurika hapo Nshamba walisubiri Tangu saa nane mchana hadi saa 12 jioni wakitegemea kuwa Dr. Slaa angejitokeza hiyo tarehe 15/10/2010 lakini hakutokea. Baada ya kufuatilia sababu ya Dr.Slaa kutoonekana ikasemekana kuwa Helcopter ya Dr. Slaa ilipotelea angani na kujikuta iko ndani ya eneo jingine liitwalo NGOTE badala ya Kutua Nshamba Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera. Baada ya Tukio hilo zikafuatia habari mbali mbali na maoni tofauti kuwa helicopter hiyo ilijikuta maeneo ya Geita mkoa mpya badala ya Nshamba Wilayani Muleba.Wengine wanasema rubani hakuwa na direction za Nshamba na sababu kibao. Hali hii imewaweka roho juu juu ya kutaka wajue ni lini mgombea huyo anarudi ili wahakikishe kuwa baiskeli na pikipiki zao hazipati pancha na kushindwa kumuona na kumsikiliza mgombea huyo. Watu wa Nshamba wanasema Kura za urais kwa Dr> Slaa ni nyingi lakini kufika kwake kungewaongezea imani zaidi na kujionea na kuhakikisha kura atakazopata. Wachache wanaanza kujiuliza kuwa kama ahadi yake ya Kuwafikia inashindikana , vipi zile anazoahidi kuifanyia nchi? Ndipo wakatulizwa kwa kuambiwa kuwa tarehe 24/10/2010 Dr. Slaa atakuwa ndani ya Kagera ila isijulikane ni lini atakanyaga hapo Nshamba. Nilipododosa kuhusu Kura za Mbunge walisema zilizo nyingi anapewa mpiganaji mwingine kwa jina la Prof. Anna Tibaijuka ambaye wanaamini kuwa wakiungana na Dr. Slaa (endapo ataingia ikulu) mambo yatakuwa shwari. Maana wanaamini U DR. wa Slaa si wa heshima bali ni wa kula kitabu ki-ukweli, pia Prof . Tibaijuka vilevile, hivyo kuamini kuwa hiyo itakuwa combination ya Ngassa na Mgosi!!!!!!(hahahahahaaaaa) wananchi bwana!! Sasa mwenye mawasiliano na DR. Slaa au kamati yake ya Kampeni watangaze mapema kuwa Dr. Slaa anarudi lini Nshamba?
UTANI ULIOENEA MKOANI KAGERA
Eti kwa kuwa Mke wa Dr. Slaa ni Kutoka Kagera basi wana Kagera woote ni Shemejiiiiiii wa Mgombea. hahahaaaaaaaaa, yaani nikacheka sana, ni kauliza kwa hiyo???? Wakasema mwaka huu watataka ""first lady atokee hukuhuku""!!!!!!!LOh. Kwa hiyo hawafanyi kosa kabisaaa. Sasa ngja tuoneeeeeee . Picha ya mwaka huu kali. niulizeni zaidi niwaelezee. 0754918212
UTANI ULIOENEA MKOANI KAGERA
Eti kwa kuwa Mke wa Dr. Slaa ni Kutoka Kagera basi wana Kagera woote ni Shemejiiiiiii wa Mgombea. hahahaaaaaaaaa, yaani nikacheka sana, ni kauliza kwa hiyo???? Wakasema mwaka huu watataka ""first lady atokee hukuhuku""!!!!!!!LOh. Kwa hiyo hawafanyi kosa kabisaaa. Sasa ngja tuoneeeeeee . Picha ya mwaka huu kali. niulizeni zaidi niwaelezee. 0754918212