Nakubaliana na wewe kabisa, Kama tutawezesha vijana kwa Mitaji Kama ulivyotoa mfano wa hao ombaomba itakua poa, maana vijana wengine wanatoka kwenye mazingira magumu mnoo Hivyo inakua changamoto, tufanye empowerment kwa vijana both ya knowledge and capital, ukienda nchi za wenzetu wanafunzi wa vyuo vikuu wanasoma main course na course zingine za ziada mfano mtu anachukua Bachelor of Business Administration lakini pia anasoma course ya upambaji, upishi, ushinaji na n.k.Ni kweli lakini bado jukumu tunalo lazima tujiendeleze na kutumia fursa hizo pata picha miaka hiyo 1800 zama hizjo akina Alhaj Dantata babu wa babu wa Aliko Dangote alikuwa tajiri mfanyabiashara mkubwa kipindi hicho kulikuwa hali haiko kama sasa alitumia fursa vizuri na pia fursa huonekana kwenye macho ya yule aionaye mfano Mengi marehemu aliona fursa ya biashara ya kutajirika basi amehusle amekuwa hivyo ila changamoto ya watu wetu wengi ni walalamishi japo sio wote akili zao zinaona matatizo tu wanaweza kuzungukwa na mto mkubwa wa maji lakini juu hapo vijiji vinanjaa tunahitaji kusugua bongo na maarifa tuyakabili haya maisha with or without help ya serikali kwani maisha ni yetu na tutahukumiwa na jamii jinsi tutakavyoyaishi. Ikiwa ombaomba tu walishawahi pewa mikopo ya dola 5 hadi 10 na kufanya biashara hadi kuacha kuwa omba omba basi vijana watu wazima wasomi wasio wasomi wanaweza kabisa kuanzisha vitu kupitia uwezo wao na hicho kidogo na kufika mbali tukibadili mindset hata Mbuyu ulianza kama mchicha.
Maanake kijana Huyu Akihitimu Anakuwa na wigo mpana wa kuajiriwa na kujiajiri kwa sababu Anakuwa na option. Lakini pia Vijana wanafanya baadhi ya Gunduzi za teknolojia wanaishia wapi, hawapati support kutoka mamlaka husika, ni rahisi sana kuifanyia nchi chochote Kama mazingira Yana support, hata private sector ili zifanye vizuri lazima kuwa na mazingira rafiki