TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

Sitaki kuamini mpk sasa saa 7 mchana hakuna taarifa yeyote shame on you serikali ya CCM
 
Mkuu sisi hapa tunachokililia ni jinsi gani serikali hii ya magamba ilivyo kuwa ovyo linapotokeaga jangaa kwenye uokowaji ni zero kabisa!
Mv bukoba, mv spice etc majanga yote hayo uowokoaji ulikuwa zerooooo

Alafu yule mpuuzi January kazi kusema wako hai, hakuna majeruhi.. Bure kabisa hawa watu
 
EEEEEH Mungu,wapo wapi waja wako jamani?

Bora umejileta, kuna Uzi siukumbuki ila ulikua unaleta ubishi usio na maana na nikakwambia Nchi hii hakuna kilichofanyika mkajivunia na nikatoa mfano wa ajali ya Mv. Bukoba kua tulishindwa kuwaokoa ndugu zetu mpaka pale wazamiaji toka A. Kusini walipofika hivyo kupelekea vifo vingi kutokea.

Swali langu kwako wewe Gamba wa kike ajali imetokea tangu jana usiku je mpaka sasa ni muda gani umepita? Hakuna taarifa yoyote ile ya kueleweka,
Ajali ya Helicopter moja tu inawatoa kamasi kufika eneo la tukio na kujua kama kuna majeruhi au ndugu zetu wamepoteza maisha.

Je Nchi yetu ingekua imepata janga hata moja la aina ambayo tunayasikia kila siku yakitokea katika Nchi za Bara la Asia kuna Mtanzania hata mmoja atasalimika(Mungu atuepushie mbali)
Tatizo mmekalia siasa tu hata kwa mambo ambayo hayahitaji Siasa.
Miaka 54 ya Uhuru Nchi haina Kikosi Madhubuti cha uokoaji aidha wa Majini au Nchi kavu?

Halafu bado mnataka muendelee kuiongoza Nchi hii?

Mwaka huu hatudanganyiki ingawaje mnatuona ni Malofa na Wapumbavu.
 
Alafu yule mpuuzi January kazi kusema wako hai, hakuna majeruhi.. Bure kabisa hawa watu
Mimi nikiwa kma mwana ukawa ila filiponjombe nlikuwa namkubali sana!
Ila vp mzee wa kutuita malofa+wapumbavu alikuwemo humo au??
 
Yani tuache kabisa hata ingekua Baiskeli masaa yote hayo hujaokolewa lazima uende, ,, hata KIU huwa Inaua, ,, sembuse Chopa. ...wale makomandoo wa Jeshi tunaowaonaga na Paratute si watumike jaman, ,, achanenni na makamba anaokoa watu kwa wall ya twitter
 
Hii serikali hopeless kabisa..., mpaka sasa hivi no updates.. Halafu tuwape nchi tena nyie... Kalagabhao..!!
 

Huyo anachokijua ni kuwa anataka "mabadiliko"
 

Unajua kinachoendelea huko on ground muda huu kwenye hiyo operation?? Kama unajua, tujuze basi. Kwa kweli wavaa katakei na mihemko yenu tunawavumilia sana. Uchaguzi uje, upite tupumzike.
 
Jeshi linatuangushaga sana linapotokeaga suala la kufanya uokoaji
 
Mimi nikiwa kma mwana ukawa ila filiponjombe nlikuwa namkubali sana!
Ila vp mzee wa kutuita malofa+wapumbavu alikuwemo humo au??

Ningekuwa Mungu ningemtoa Filikunjombe na abiria Wengine na kumweka Lofa, Nepi na Mwinguru wafie huko
 
I don't think kama kuna usalama hapa kama kweli ajali hiyo imetokea.

Helkopta iko mita mia kadhaa juu halafu ghafla iporomoke chini na watu wawe salama!!??

Kama ndege tu yenyewe haionekani mpaka sasa, hao watu (abiria) watakuwaje salama jamani?

Au tunazugwa tu hapa, pengine jamaa walitua kwenye moja camp sites za Selous wanakula good time tu!!?
 
Taarifa za ajali ya helkopita aliyokuwa akisafiria aliyekuwa mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe mpaka sasa ni za kutatanisha.

Muda mfupi uliopita nimeongea kwa njia ya simu na Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Mahamoud Mgimwa amesema mpaka sasa hakuna taarifa rasmi kuhusu tukio la kuanguka kwa Helkopita iliyokuwa na abiria kadhaa akiwemo Deo Filikunjpmbe.

Mgimwa ambae yuko Handeni kuhudhuria mazishi ya waziri wa zamani wa viwanda na biashara Dk Abdalah Kigoda amesema ajali hiyo imetokea eneo la Selou ng'ambo ya mto Rufiji ambako hakuna mtu anaeweza kufika kwa sasa na hakuna hata abiria yeyote kati ya waliokuwemo kwenye helkopita hiyo ambae amethibitisha kuwa wako salama.

Amesema taarifa kutoka Selou zimeeleza kwamba helkopita hiyo iliomba kutua katika moja ya maeneo ya pori la Selou lakini ilipoteza mawasiliano kabla ya kutua na mpaka sasa haijulikani iliko ingawa juhudi zinaendelea kufanywa ili kufika kwenye eneo la tukio lakini itakuwa ni asubuhi kwasababu sasa tayari ni usiku.

Nae Meneja wa pori la akiba la Selou, Benson Kibonde amesema amepata taarifa za kutokea kwa ajali hiyo na hakuna taarifa zozote kuhusu usalama wa abiria na helkopita waliokuwa wakisafiria.

Kibonde amesema taarifa kutoka Selou zimeeleza kuwa ulisikika mlio kama vile helkopita hiyo iligonga kitu na baadae ulionekana moto angani na mpaka sasa hakuna taarifa kuhusu hali ya abiria na iwapo helkopita hiyo imeharibika kwa kiwango gani.
 
Unajua kinachoendelea huko on ground muda huu kwenye hiyo operation?? Kama unajua, tujuze basi. Kwa kweli wavaa katakei na mihemko yenu tunawavumilia sana. Uchaguzi uje, upite tupumzike.

Hujui thamani ya Mtu na utu, , mbafuu
 
Inashangaza sana kama hadi muda huu hakuna tamko la uhakika kuhusu ajali hii toka mamlaka zinazohusika, ina maana hajafika eneo la tukio? Au taarifa ni mbaya kiasi ambacho wanasita kuzitoa????????
 
Mh unanitisha iligongana na Kitu! My God isije ikawa mtimanyongo
 
deo amefariki dunia ..mda mfupi uliopita imethibitishwaaaa..habari kamili itafuata...hakuna aliyepona ....RIP DEO
 
Mtoto wako akikaa chini ni upumbavu wako. Miti yote hii huioni?

Hizo dharau zenu zitawatokea puani mwaka huu.
Kwahiyo wazazi wa hao watoto ndio wenye jukumu la kuhakikisha Shule inakua na Madawati ya kutosha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…