TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

Kipindi hiki cha kampeni tumewapoteza wanasiasa muhimu:
1. Mohamedi Mtoi - Mgombea ubunge Lushoto (CHADEMA)
2. Celina Kombani - Waziri
3. Ernest Chale - Katibu CCM Ilala
4. Mch. Christoper Mtikila - M/kiti DP
5. Estomih Malla - Mgombea ubunge Arusha mjini (ACT)
6. Dr. Abdallah Kigoda - Waziri
7. Dr. Emanuel Makaidi - M/kiti NLD
8. Deo Filikunjombe - Mbunge Ludewa (CCM)

Tumtumaini Mungu kila saa na kila wakati. Sisi sote ni maua tu hapa duniani, tunachanua na kunyauka.
 
January kwa kweli nina hofu na uwezo wake wa akili,ni bora angekaa kimya kuliko kutweet habari za uongo,yaani ujinga sana tena sana
January si ndio think tanker wenu? au hujui ndio msemaji wa ccm? tulioikataa ccm haya tunayajuwa siku nyingi jishangae wewe usimshangae Makamba.
 
R.I.P Deo, R.I.P Capt Slaa na R.I.P wale wawili ambao hawajatambuliwa.

Mungu awape pumziko la amani na familia zenu faraja iliyo kuu. Amen
 
Yaan wale wazuri ndo wanaondoka mabazazi yanapeta tu pumzika kwa amani Deo
 
Tumepoteza jembe, RIP DEO na tuwaombee CCM Mungu awahurumie na kuwatia nguvu katika kipindi hiki kigumu cha kufiwa na kujiandaa kuachia ikulu
 
Members hebu muda mwingine tunapotafakali matendo ya Mungu basi tuweke Siasa Pembeni, Mimi ni mwanachama Hai wa ACT, lakini Kura yangu nilisha sema kwa LOWASA, kwasababu naijua vizuri Demokrasia.

Sasa Chama kingine kinapo pata Tatizo tunapaswa sote Kama Watanzania tushikamane kufarijiana, Hizi Kampeni zina mwisho wake lakini Utanzania wetu hauna mwisho,

Inasikitika sana watu wanapo furahia Kufa kwa kiongozi fulani eti kwasababu ametokea CCM, Please HUU SIO UTANZANIA WETU TUNAKIUKA MISINGI TULIYO ACHIWA NA MWALIMU NYERERE, WATANZANIA WOTE NI NDUGU

Nilihisi Unaakili Pale Ulipojijua Kuwa Hata Kura Yako Ukiweka ACT itapotea kwani hawatashinda na nivema ukaiweka CHADEMA kuongeza ushindi, kumbe unaakili za kuvukia barabara zinazokufanya unamuabudu JKN kwa kulinganisha uongozi wake katika kizazi cha tabulalasa na kizazi cha sasa.
 
January si ndio think tanker wenu? au hujui ndio msemaji wa ccm? tulioikataa ccm haya tunayajuwa siku nyingi jishangae wewe usimshangae Makamba.
Mimi sina chama,ila kura yangu nampa Magufuli bila kujari chama chake
 
HABARI ZILIZOTUFIKIA SASA NI KUA ALIYEKUA MBUNGE WA LUDEWA ...

Hakukuwa na haja ya kuanzisha thread nyingine wakati zipo ambazo zinahusu jambo hilo hilo zilizoanzishwa saa mbili zilizopita na zimeunganishwa. Kama umechelewa kuingia humu, jaribu kupitia title za page za mwanzo ujiridhishe kuwa uzi unaotaka kuuanzisha haupo mwingine kama huo. Hakuna haja ya kukurupuka, na si lazima ionekane wewe ni mwanzilishi. Ni tabia za kishabikishabiki ndio zinawafanya watu mkurupuke
 
Napenda niwe mkweli kutoka ndani ya Roho yangu...vifo hivi vimenisikitisha sana ila cha DEO FILIKUNJOMBE kimeniuma mno . alipokuwa ananzungumza kwa bunge nilitaka kusikia atakacho kisema kwani he was very different politician non partisan which I think had cost him positions in the cabinet. He was more interegent than some of the junior ministers but because he came from common family.

angekuwa ni vuvuzela mkosa adabu yaani leo NINGE KUNYWA SAFARI YA BARIDI SANA KUSHEREHEKEA
 
😢😢😢😢😢😢apumzike kwa aman
 
Back
Top Bottom