TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

TANZIA Helikopta yaanguka, aliyekuwa Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe na wengine wapoteza maisha!

Hakuna anekodi chombo cha usafiri ili kije kiue, kama unataka kulaumu chama, jua chama kilikodi chopa nne, ambazo zipo salama mpaka sasa, lkn pia uelewe huenda aliekodi ni marehemu mwenyewe, maana chopa ilikuwa na picha yake na ya mgombea urais, sasa unamlaumu aliezikodisha sikuelewi unamaanisha nini!!!

Mambo ya kujiliwaza tu! Nasubili nione hizo nne zilizobaki, nani atazipanda na kuweka manjonjo ya kuiga.

Hii ni nchi isiyo na viwango. Tumecheza na viongozi chini ya viwango, hospitali chini ya viwango, barabara chini ya viwango na sasa nikiambiwa chopa zote zilizoletwa ni chini ya viwango, sitaona ajabu. Mambo yote tunawaza dili tuuuuu!
 
Nimesoma.mada humu hata kabla ya kuhakikishiwa vifo kuna watu wa aina humu ndani

1))WAKATILI
2))WENYE WIVU
3))WASIOMWOGOPA MUNGU
4))MUNGU AWASAMEHE NA DEO UWASEMEHE UKUPENDA KUUNGUA DEO LEO TUNATUMIA DNA.KUKUTAMBUA.LUGALO
 
Hii chopa ilikuwa imepambwa kwa picha ya Deo na Magufuli, si Magufuli na Suluhu. Hii inaonesha kuwa, Deo ndiye aliyekuwa amekodi chopa hiyo na si CCM kama ambavyo Makamba anataka tuamini.Tafsiri yangu ni kwamba ama Deo, kama ilivyo kwa wenzake, alishaukwaa ukwasi.Au alikuwa karibu sana na wenye nazo, na sijui alikuwa anawalipa nini.Watu wa Ludewa wanaweza kuwa na majibu.

Dogo alianzia Galanosi.
 
Nimesoma.mada humu hata kabla ya kuhakikishiwa vifo kuna watu wa aina humu ndani

1))WAKATILI
2))WENYE WIVU
3))WASIOMWOGOPA MUNGU
4))MUNGU AWASAMEHE NA DEO UWASEMEHE UKUPENDA KUUNGUA DEO LEO TUNATUMIA DNA.KUKUTAMBUA.LUGALO

Mkubwa, usiogope kifo hadi kikufanyishe usiyopenda. Mbona TZ tulikuwa tukifurahia na kumtakia kifo Idd Amin? Kila mtu ana shujaa wake, na kama wewe si shujaa wangu, nitakuombea balaa lolote.
 
kwaheri Deo,kwaheri member mwenzetu jf.Ishu moja watz mnielewe,kuna jambo kubwa sana linatokea na linaendelea kutokea nchini,and it's more spiritual...
 
Nadhani baada ya Mwandosya kususa na Mwakyembe kushindwa kuwa na ushawishi Nyanda za Juu kusini, walitaka kumtumia huyu bwana ili wapate kura huko maana ukimtoa Prof Mwandosya sidhani kama kuna mwingine mwenye ushawishi pande za kule. Nadhani ndiyo akapewa mpaka hiyo Helikopta atembee pande zote huko kumnadi Magufuli.. Sijui kwanini na yeye aliingia kwenye mkenge wa wahuni safari hii..
Si walijiapiza kwamba hawatatumia chopa kwa vile barabara wametengeneza na wanaizionea fahari?Filikunjombe si alipita bila kupingwa sasa safari za giza za nini,na likuwa anakwenda mtunuku mungu yupi huyo juhudi zake? Lazima aingie mkenge kwa vile hakuwahi kuwa mtu wa wapenda haki..polisi ni polisi km wengine laana haiwaachi..hujifanya wema palipo na kula na sifa za kuwapandisha vyeo...gizani ni waovu tuu hawana dini wala utu....ripoti ya escrow ni laana kwa nchi yetu..ni Mungu aliiokoa nchi DKK za Mwisho... ni toppings ya kufuru.....polisi kuwatumia ni rahisi sana....niliangalia video yake ilikuwa laana tupu..kajenga office ya walimu kwa gharama kubwa sana ili awatumie walimu...badala ya kujenge jengo imara na simple ili fedha nyingine ziongeze madarasa ktk hiyo hiyo shule wanafunzi wengi zaidi wapate madarasa na wanafunzi wakae wachache....Mungu anajua kilichofanyika watanzani wenzetu tuwaambie waache upuuzi wawe na mipaka ya sifa kwa marehemu
 
ImageUploadedByJamiiForums1445034153.381043.jpg
 
Filkunjombe ni mzalendo makini. Taifa bado linamhitaji.
Kwanini hilo Taifa likampandisha chopa ?....Neno TAIFA kwa wamalawi ni km ugaidi...TAIFAS ni washika watumwa , wamamizi na wauaji kutoka mbali kupitia ktk pwani,fuko na ardhi ya Tanganyika....ndio hicho unamaanisha kinamhitaji huyo jamaa?
 
Nimesoma.mada humu hata kabla ya kuhakikishiwa vifo kuna watu wa aina humu ndani

1))WAKATILI
2))WENYE WIVU
3))WASIOMWOGOPA MUNGU
4))MUNGU AWASAMEHE NA DEO UWASEMEHE UKUPENDA KUUNGUA DEO LEO TUNATUMIA DNA.KUKUTAMBUA.LUGALO

Mkuu, Aina Hii Ya Watu Kumbuka Unakutana Nao Toka Ukiwa Primary....Umejisahau,!!
 
Deo Filikunjombe aliwahi kufanya kazi World Vision,lile shirika la Jesuits? Well,I hope hakugombana nao. Wale jamaa ni very nasty characters. Nimeandika katika posting mojawapo jinsi World Vision walivyopeleka AIDS Haiti. AIDS maana yake Ukimwi.
 
RIP Jembe aka Deo Fulikunjombe
RIP Captain Slaa
Poleni wote tulioguswa na Misiba hii,


(UPDATED 13:30 - October 16, 2015)

Kwa mujibu wa Jerry Silaa (aliyekuwa Meya wa Ilala):

=========
KUHUSU MAREHEMU FILIKUNJOMBE:

- Deo Filikunjombe alimaliza shahada yake ya Mass Communication Makerere University Uganda

- Alikuwa Ripota wa Radio One na ITV kwa muda mrefu akitumia jina la " Deo Haule" akiripoti toka Kampala

- Alijiunga na Jeshi la Polisi na kufanya kazi kwa mwaka mmoja kisha akaacha kazi sababu alipangiwa kitengo cha Habari makao makuu ya Polisi na kufanya kazi chini ya Mohamed Mhina ambaye alikuwa chini yake kielimu.

- Alipotoka Polisi, alijiunga na World Vision kama Communication/ Information Officer na kufanya kazi kwa miaka kama minne hivi akiwa Makao makuu Arusha na baadae akahamishiwa tawi la dar es salaam

- Alipotoka World Vision akajiunga na MKURABITA ambapo alifanya kazi kwa muda usiozidi miaka miwili akaacha.

- Baada ya kuacha MKURABITA, akafungua duka lake la electronics lipo Benjamin Mkapa Tower, opposite na Posta Mpya ghorofa ya kwanza, akafungua vituo vyake vya kuuzia mafuta Ludewa na ndipo akaanza harakati za kuingia kwenye siasa na kuchaguliwa kuwa mbunge mwaka 2010.

=========
Previously:


Heshima kwenu Wakuu,

Kuna habari zinasambaa kwamba kuna Chopa ilikua imebeba Makada wa CCM imepotea ikiwa inaelekea Njombe.

Taarifa zinasema, wakati inaondoka ilishindwa kupaa lakini mwisho wa siku ikawa imepaa.

Hadi sasa sijajua kipi ni kipi. Hivo nimeileta hii habari kama tetesi ili mwenye taarifa za mwanzo atujuze.

Asanteni sana.

========
UPDATES:

- JamiiForums imejaribu kumtafuta Filikunjombe kupitia simu yake ya mkononi bila ufanisi
- Taarifa zinabainisha kuwa kweli kuna ajali ya helikopta imetokea lakini mpaka sasa hali za waliokuwa kwenye chombo hicho hazijajulikana
- Baadhi ya abiria wanaodaiwa kuwa ndani ya chombo hicho ambacho kinasemekana kilikuwa kikirushwa na Kapteni Silaa ambaye ni baba Mzazi wa Jerry Slaa, ni Haule (ndugu yake Filikunjombe), Deo Filikunjombe, Mtumishi mmoja wa Halmashauri mojawapo ya Mkoa wa Njombe...
- Jitihada za kufika eneo la ajali zimekuwa ngumu kwakuwa ni eneo ambalo si rahisi kufikika nyakati za usiku; juhudi zinaendelea
- Helikopta iliruka saa tisa ilitakiwa itue saa 11 Iringa. Status ni MISSING. Casualties sio CONFIRMED kwa kuwa ni porini mpaka kesho gari likifika eneo la tukio sababu kuna mto na watu wa camp na rangers hawawezi kuvuka usiku huu.

=> Katika Kituo cha Luninga cha ITV taarifa ya habari saa tano usiku wamethibitisha kutokea kwa ajali ya helkopta ambayo Deo Filikunjombe alikuwa anasafiria lakini wanadai yuko salama

================

- Ndege inayodaiwa kuanguka leo katika Hifadhi za Selous...

View attachment 299341View attachment 299342View attachment 299343View attachment 299344
 
aisee kuna newz kuwa kuna ajari ya Gari imetokea huko iringa.ni ya kampeni ya ccm.
 
kwaheri Deo,kwaheri member mwenzetu jf.Ishu moja watz mnielewe,kuna jambo kubwa sana linatokea na linaendelea kutokea nchini,and it's more spiritual...

Fafanua mkuu utufungue wengine.
 
Deo Filikunjombe aliwahi kufanya kazi World Vision,lile shirika la Jesuits? Well,I hope hakugombana nao. Wale jamaa ni very nasty characters. Nimeandika katika posting mojawapo jinsi World Vision walivyopeleka AIDS Haiti. AIDS maana yake Ukimwi.

World Vision ni ya JESUITS..!!!!!!
 
Ludewa kuna nuksi mpaka sasa wabunge waliofia madarakani ni4, waliohai ni3 tu cjui kwa nini?
 
Back
Top Bottom