UONGOZI KWENYE CHAGGALAND
Katika miaka ya 1950's, Chaggaland ilikuwa na utawala ambao tayari ulikuwa unaelekea kwenye nchi inayoweza kujitawala.
Kihistoria, Chaggaland ilikuwa ina tawala mbalimbali za kijadi zilizokuwa zikiongozwa na watawala wao wa kimaeneo, mfano, Machame (Mashami), Kibosho, Uru, (Old) Moshi, Kirua, Kilema, Marangu, Keni, Mkuu, Mashati, n.k. Kwa mfano, mwaka 1887, msafiri mmoja wa Kijerumani, Ludwig von Höhnel, aliyetembelea uchagani, aliandika kwamba uchagani kuna tawala za kichifu 28.
Wenyeji (Wachaga) waliziita tawala hizi kama nchi. Machame tokea siku za nyuma, waliita mtawala wao kuwa ni Mangi. Hicho cheo cha Mangi kilitumiwa pia na Wameru kwa watawala wao wa jadi, kwani Wamashami na Wameru walikuwa na asili moja. Upande wa Mashariki mwa Uchagani, yaani Vunjo na Rombo, walitumia cheo cha Mkumbe, ingawa baadaye jina la Mangi lilikuja kuzoeleka uchagani na kuchukua nafasi ya Mkumbe.
Ilipofikia mwaka 1946, utawala wa Kiingereza Tanganyika uliigawa chaggaland kwenye majimbo matatu ya kiutawala, ambayo ni Hai, Vunjo, na Rombo. Haya majimbo yaliwekwa chini ya Wamangi walioitwa Waitori. Kwenye baadhi ya majimbo hayo, Waitori walisaidiwa kiuongozi na Wamangi ambao walikuwa watawala wa jadi wa maeneo ya kiutawala tokea zamani. Wamangi hao walikuwa wakisaidiawa na wakuu wa vitongoji waliokuwa wakiitwa Wachili (Washili) ambao walihusika zaidi na ugawaji wa ardhi kwa niaba ya Mangi.
Jimbo la Hai mipaka yake lilikuwa inaanzia Kibong'oto mpaka Old Moshi. Hili liliongozwa na mtawala wa Machame Mwitori M.H Abdieli Shangali. Jimbo la Vunjo mipaka yake ilikuwa kuanzia Kirua hadi Mamba. Hili liliongozwa na Mwitori Petro Itosi Marealle wa Marangu. Jimbo la Rombo mipaka yake ilianzia Mbengeni hadi Tarakea. Hili lilikuwa likiongozwa na Mwitori Selengia Kinabo wa Mkuu-Rombo. Mabadiliko yalitokea kwa Rombo ambapo mwaka 1949 baada ya Mwitori Selengia Kinabo kufariki, Jonh Ndaskoi Maruma wa Mashati, Rombo alitawazwa kuwa Mwitori wa Jimbo la Rombo.
Harakati za kisiasa zilizojengeka kwenye hisia za wakoloni kunyang'anya wazawa ardhi ili kuleta wazungu wenzao kulima mashamba makubwa, zilishika kasi miaka ya mwisho ya 1940's, zikiongozwa na chama cha KCCU.
Mlengwa mkubwa wa harakati hizo alikuwa ni Mwitori M.H. Abdieli Shangali wa Hai ambaye alishutumiwa vikali kutumiwa na wazungu kuchukua ardhi ya wazawa. Chama cha KCCU, kikisaidiwa na vigogo wa kisiasa uchagani akina Petro Njau, Hassan A. Nkya, na Joseph Merinyo, walichochea wachagga kuchagua Mangi Mkuu juu ya waitori ambao walitupiwa lawama kwamba wamekuwa vibaraka wa wakoloni.
Harakati hizo zilikuwa kubwa na kusababisha serikali ya kiingereza kukubali uchaguzi ufanyike ili wachagga wapate mtawala mmoja atakayekuwa juu ya wengine.
Hata hivyo, KCCU ilicharuka baada ya serikali ya kiingereza kutoa tamko kwamba imekubali madai ya wananchi kupata Mangi Mkuu na kupendekeza Wamangi Waitori ndiyo wawe wagombeaji wa nafasi hiyo. KCCU walisema wana mtu wao mahiri na makini anayetambulika na kupendwa na watu, ambaye ni Thomas Lenana Marealle, mpwa wake na Mwitori wa Vunjo, Petro Itosi.
Kwa vile Thomas Marealle alikuwa ametokea kwenye ukoo wa kimangi pia, wakoloni waliridhia, hasa ikitiliwa maanani kwamba alikuwa ndiyo kijana zaidi na Msomi kupita Waitori wote waliokuwepo. Uchaguzi ulifanyika mwaka 1951 na Thomas Lenana Marealle akachaguliwa kwa kishindo kuwa Mangi Mkuu wa Wachagga.
Kieneo, Hai ndiyo ilikuwa jimbo kubwa kuliko majimbo mengine ya Chaggaland. Mwitori Abdieli Shangali ambaye alishaipa Siha utawala wa kujitegemea mwaka ule wa 1947, aliamua pia kuifanya Masama kuwa utawala wa kujitegemea na pia Machame ikawa utawala wa kujitegemea. Kwa mara ya kwanza katika historia ya uchagani, Masama na Machame zikawa ni tawala (nchi) mbili tofauti.
Mtawala wa Siha alikuwa ni Gideon Nasua Mushi, aliyeweka makazi yake Kashashi-Lawate alipohamia kutokea Machame, mwaka 1927 aliyetawazwa kuwa mtawala wa Masama ni Charles Shangali, mdogo wake na Mwitori Abdieli. Mwaka wa 1952, Abdieli Shangali akamtawaza mtoto wake, Gilead, kuwa Mangi wa Machame, huku yeye akibaki kuwa Mwitori wa Hai.
Yote haya majimbo yalikuwa na Washauri wa Mangi, jeshi likiongozwa na majemedari wa vita na Wachili waliokuwa wakiongoza vitongoji. Makao madogo ya Hai yalikuwa Maili Sita. Makubwa yalikuwa Machame, Isareni.
Miaka michache tu ya uwepo wa Serikali moja kuu maendeleo makubwa yalipatikana Moshi na kuifanya kuwa sehemu ya kutiliwa mfano Afrika ya Mashariki
Na hata baadhi ya watafiti wa kingereza walidai kuwa endapo ChaggaLand ingejitawala kwa miaka 20 pekee ingelikua nchi iliyoendelea kama zilivyo nchi za magharibi au kasi ya singapore ya leo
Wamangi wa serikali mpya walijituma sana kuwaletea wananchi maendeleo makubwa ya kijamii na kiuchumi kwa kuwekeza kwenye elimu,afya,maji,uchumi,na hata mambo ya kijamii na kitamaduni
My take:Wakuu hii issue inasisimua mno aisee
Pichani ni mheshimiwa Rais wa Chaggaland na mkewe pichani walipohudhuria sherehe za uhuru wa Ghana[emoji1313][emoji1313][emoji1313][emoji1313]
Sent using
Jamii Forums mobile app