Help!... Aliyeigiza kwenye tangazo hili nimpate wapi?!

donlucchese

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Posts
17,128
Reaction score
21,885
niaje wana jamii? natumaini wakuu wote mpo salama. kubwa langu ni msaada wa kumpata yule dada alieigiza kwenye tangazo la ishi la vunja ukimya zungumza na mwenzio. kuna siku nilipNda nae daladala kwelekea posta bahati mbaya nikaangusha Id yangu na atm card yangu. kwa bahati nzuri yule dada aliokota ivo vitu n kumwambia konda kwamba mwenyewe akipatikana atamrudishia. sasa najaribu kumtrack bila mafanikio so naomba wenye kumfahamu full name or maeneo anapoishi niweze kupata vitu vyangu. asanteni!
 
Nadhani ungeanzia na vituo vya televisheni idara ya matangazo/marketing vinavyorusha hilo tangazo, watakupa mawasiliano ya marketing agency iliyotengeneza hilo tangazo na hatimaye huyo dada atapatikana;
 
ukimpata akikurudishia vitu vyako mpige ofa ya bia na kitimoto kidogo huku mkibadilishana mawazo
 
kwani havina namba ya simu hivyo vitambulisho na atm card angevipeleka kwenye bank yako..
 
Nadhani ungeanzia na vituo vya televisheni idara ya matangazo/marketing vinavyorusha hilo tangazo, watakupa mawasiliano ya marketing agency iliyotengeneza hilo tangazo na hatimaye huyo dada atapatikana;

shukrani mkuu
 
pole kama ni kweli,
acha wakuu wapitie hapa,
bila shaka utampata jf ni kila kitu.
 
mkuuu kweli wewe creative daaa never seen mbinu hii!
 
Mkuu pole sana.. Jamaa amekuja na idea nzuri ya kutafuta agency iliyotengeneza tangazo. Kwa kifupi walioshinda ile tenda ya ile campaign walikuwa wajanja wachache wa mjini kampuni yao siikumbuki jina vizuri. But ule mchongo walipewa na mtu wa ndani bdae kikanuka kuwa pesa ilitafunwa vibaya mno ndo maana phase two ilizengua, hivyo kuwapata hawa jamaa I dnt knw.. Kukusaidia call this number ya master tracker maarufu kama una shida ya msanii yoyote bongo wa maigizo... Kwa kifupi he knows everyone usimzengue tu maana atakuharishia mbaya. 0713458445
 
Nirushie password za hiyo atm card nikusaidie kumsaka huyo bibie.
 

Huyu Dada inaelekea ni mwaminifu aliona afadhali wewe umtafute kuliko angemwacha konda, tulia kaka utapata tu.

 
Mkuu si useme tu..umefall in love..unaanza kusema ID na ATM ha ha ha ha ha ha ha!! sawa mkuu watakupa contact..mimi sina.
 
Lile tangazo ni la champion ambayo ipo chin ya engenderhealth so anzia hapo.
 
me najiuliza ni kwanini ameamua kubaki navyo na asivipeleke bank esp iyo atm?...usikute she is dying to meet you!..ndo baati zenyewe izooo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…