Bibie pole sana kwa hilo jaribu unalolipitia. Pia nikupe hongera ya kuwa jasiri na kumdokezea juu ya ndoa na maisha yenu ya baadaye. Nikupongeze pia kuwa muwazi na kutafuta hekima za watu wengine hapa JF, ninaamini tatizo limefika kwa wenyewe na utapata mawazo mengi tu mazuri, pengine hata huyo mwandani wako anaweza bahati mbaya au nzuri akapita hapa na kusoma hata kama hatajua ni wewe lakini atafaidika na mawazo ya hapa na hivyo kujikagua tena na tena then akaamua lilojema.
Hata hivyo naomba nikuangalize mambo kadhaa:-
1. Fahamu kwamba mke au mume ni zawadi aipatayo mtu kutoka kwa Mungu.Nina amini yupo mume ambaye ushaandaliwa, yawezekana ni huyo uliyenae au siye, Jaribu kumuomba au umshirikishe Mungu juu ya hili.
2. Naamini kuwa ndoa nio kwa faida ya mume na mke na ni kitu kizuri cha kujivunia kama wote wawili mioyo yao imeamua kwa hiari bila kusukumwa sukumwa wala kubembeleze sanaaa.Huwa nashindwa kuelewa wakati mwingine mume anavyofika mahali na kuona kwamba amemfanyia mwanamke favor (kaupendeleo flani) kwa kumuoa. Au mwanamke eti kakubali ndoa kwa sababu tu eti kamuonea huruma mkaka au wazazi wamempiga mkwara aolewe. Mambo hayo husababisha maisha ya ndoa kuwa magumu na machungu sana.
Maoni yangu ni kwamba hadi sasa umeshafanya sehemu yako, imetosha. Anza kuufundisha moyo wako kuwa na kiasi, Isijekuwa labda mnakutana kimwili, basi yeye anafurahia hilo tendo kwamba akiwa na wewe kitandani anajisikia safiii na unajua kumpagawisha basi.Si kama anakupenda kwa ajili ya maisha ya baadae kama mkewe kutokana na sababu mbalimbali ambazo kimsingi kwake ndio vigezo vikuu vya yeye kuamua kuoa na sio sex tu.
3. Naomba nikukumbushe kuwa mara nyingi wanaume hasa (wabongo) huwa ni wagumu sana kumwambia mwanamke kuwa mahusiano yameisha na kwamba haoni kama wewe waweza kuwa mkewe, hasa pale ambapo unakuwa hujawahi kumkosea, na anatambua kwamba unampenda kwa moyo wote. Atakachofanya ni kuendelea kukutumia (kwa sex) hati wewe mwenyewe ujitoe ili yeye asilaumiwe. Pengine mwenzio tayari ana mchumba na hawezi kukwambia. Usipojua kujikaza na kukabiliana na maisha utajikuta huwezi kumuacha hata pale utakapogundua ameoa na ataendelea kukudanganya kuwa kaoa tu lakini moyo wake upo kwako na hivyo ukaendelea kumuhudumia vile vile eti kwa neno la kwamba nimempenda sana siiwezi kumuacha.
4. Naamini sana wewe bado kijana na bado una chance kubwa ya kupata yule atakayeusuuza moyo wako zaidi. Sisemi ukurupuke uanze kutafuta mwingine hapana, ushauri wangu ni kwamba rudi kwenye daftari lako la tabia na uanze kujiachunguza tabia zako moja hadi nyingine tangu asubuhi uamkapo hadi ulalapo. Jicheck heshima, ukarimu, upole, kujitoa, usikivu, mahusiano na jamii inayokuzunguka, ndugu za jamaa, usafi wa mwili, akili na roho, ucheshi, huruma, uvumilivu, je upo reasonable? unaweza kusamehe na kusahau?, bidii katika kazi si nyumbani au ofisini tu bali hata kwenye jumuia. angalia watu wanapenda na wanasema nini juu yako? kama kuna baya lolote jaribu kurekebisha. Hapa kwa ujumla namaanisha ujaribu kuwa na mvuto fulani kitabia na kimuonekano.
Ukifanya haya na mengine wanayokushauri hapa ninahakika jamaa atabadili mawazo na kusisitiza ndoa haraka au kama si yeye basi waungwana kibao watamiminika kwako kuomba mkono wako katika maisha yao. But this time kuwa muangalifu usigawe kitumbua bila heshima!!! I mean usiendekeze ngono kabla ya ndoa.
Samahani sana wazee ninausongo sana na binti yetu apate ndoa ndio maana nimeandika saaaana.