Yaani elimu yetu TZ taabu tupu!

Walimu wamekaririshwa, wanafunzi wanakaririshwa hapa hatuchomoki!

Kwa taarifa yako kama ulivyouliza swali, hapo hakuna jibu lake sahihi. Lakini kwa vile mwalimu mwenyewe amakaririshwa aliyeweka Capital atakuwa alipewa vema. Jibu sahihi lilikuwa Owner's Equity. Hii ni pesa ambayo mwenye biashara mwenyewe atakuwa anaidai biashara. Na katika kukokotoa balance sheet lazima ionekane kwenye current au short term liabilities. Liabilities ni madeni yote ambayo biashara inadaiwa ndiyo maana hata hiyo tunayoita Owner's Equity imo kwenye kundi la madeni.

Pia lazima ujue kwamba biashara haina undugu na mwenye biashara, ndiyo maana unapoweka Mtaji (Capital) ambao umeuhalalisha kuwa ni kwa ajili ya hiyo biashara moja kwa moja unamilikiwa na hiyo biashara (Mtaji huo unatoka kwenye milki yako), wewe utakuja kunufaika pale mtaji huo utakapotengeneza faida, lakini hutaugusa mtaji. Lakini pale utakapochukua fedha mfukoni mwako ukanunua bidhaa kuongezea kwenye ule mtaji msingi wa biashara bila kutarajia, hiyo fedha utakuja ichomoa wakati wowote (maana utakuwa umeikopesha hiyo biashara).

Kwa hiyo majibu uliyoweka hapo juu kwa ajili ya kuchagua ulikuwa umechemka, au kama ni mwalimu wako alikuwa amechemka. Ila kwa kiwango cha Form II ambao bado wanakaririshwa wangejijibia tu na kuchukua marks zao!